Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wakenya waingia mitandaoni kuyakemea makanisa yao
Baada ya mbunge wa upinzani anayemuunga mkono naibu wa rais Perezida William Ruto na baadhi ya viongozi wengine wa Muungano tawala wa chama cha Jubilee kuzua vurugu ndani ya kanisa, wakenya wameambua kuingia mitandaoni kile wanachosema ni maovu yanayofanywa katika makanisa.
Ni jambo la kawaida kwa viongozi wa kidini nchini Kenya kutoa fursa kwa wanasiasa kunadi sera zao makanisani au kuwasuta mahasimu wao kisiasa.
Mbunge huyu wa eneo bunge la Kiharu Ndindi Nyoro Jumapili aliingia katika kanisa katoliki la kumwaambia waumini kuwa watu wanaotoka chama cha Jubelee cha rais Uhuru Kenyatta waliopo upande wa kundi linaloitwa Kieleweke hawapaswi kutoa ajenda zao katika eneo bunge lake la Kiharu.
Kauli hiyo ilizusha vurugu ndani ya kanisa baina ya wafuasi wa Jubelee na wafuasi wa William Ruto wanaotambuliwa kama Tangatanga, hadi pale makabiliano hayo yalipozimwa na maafisa wa polisi.
Kutokana na vurugu hizo , Wakenya waliamua kutoa hisia zao kuhusu makanisa kupitia #ShameOnTheChurches ama AibuKwaMakanisa:
Mfano huyu anayejiita KALEKEH kwenye ukurasa wa twitter anasema : "Makanisa ya Kenya yanapaswa kukaa na kutafakari ikiwa kweli yanafundisha injili ya Yesu Kristo Jau injili ya ufisadi na kufumbia macho uovu ".:
Nae That Classy Nurse ameandika : "Mapenzi yapesa ndio laana ya makanisa ya siku hizi. Ndio maana siku hizi mchungaji atakuombea kulingana na fungu lako la kumi ".
Mjengo Specialist yeye ameandika kuwa ni heri ashuhudie mapigano ndani ya baa kuliko kushuhudia uwenda wazimu kama huu wa kanisani:
Boring Tweep amempa Ushauri rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwamba anapaswa kuiga mfano wa Kagame wa kufunga makanisa yote na kuwaagiza wanahitaji shahada ya THEOLOGIA kufungua kanisa. Makanisa yanachanua kila uchao kutengeneza mamilionea na kupokea rushwa kupitia jina la kutakasa. #ShameOnTheChurches: