Romelu Lukaku: Mchezaji wa zamani wa Man Utd ameshutumu tabia ya ubaguzi dhidi ya wachezaji weusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku anadai kuwa sasa mpira unarudishwa nyuma na ubaguzi "Tunarudi nyuma" alisema hayo mara baada ya mashaiki wa Cagliari kumtukana wakati akichezea timu ya Inter Milan siku ya jumapili.
Tukio limetokea mara baada ya wachezaji wa Manchester United Paul Pogba na Marcus Rashford pamoja na mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham kutukana katika mitandao ya kijamii.
" Sisi kama wachezaji tunapaswa kuungana na kutoa taarifa ya kukeme tabia hii," Lukaku alisema.
Mashabiki walisema kuwa wamejithatiti kutokomeza laana inayoathiri soka na ulimwengu kwa ujumla".
Klabu ambayo mashabiki wake walitoa kauli ya kibaguzi imetoa tamko la kukemea tabia hiyo na kusema kuwa wanamuunga mkono Lukaku na udai kuhaidi kupiga marufuku na kumchukulia yeyote atakayehamasisha tabia hiyo ya ubaguzi kwa sababu iko kinyume kabisa na miiko ya klabu yao.
Lukaku alianza kutukana mara baada ya pili na kusababisha ushindi wa goli 2-1.
Katika dakika ya 72, Lukaku alipofunga kwa goli penati ndio wakati wa maneno ya matusi yalipoanza.
"Wachezaji wengi walikabiliwa na matusi ya kibaguzi mwezi uliopita … na mimi pia nimekutana nayo jana," Lukaku alisema.
"Soka ni mchezo ambao unawataka watu waufurahie na sio sehemu ya kunyanyapaliwa , tabia hii inautia aibu mchezo wetu .
"Mabibi kwa mabwana, mwaka 2019 badala ya kusonga mbele lakini sisi tunarudi nyuma.
Nina matumaini kuwa chama cha mpira wa miguu duniani vitachukulia hatua visa vyote ubaguzi ."
"Mitandao ya kijamii kama Instagram, Twitter, Facebook inapaswa kufanya kazi vizuri na klabu za mpira wa miguu kila siku ili kuona namna wataweza kuwakabili watu wanaohamasisha ubaguzi wa rangi.
Tumekuwa tukilalamikia vitendo hivi kwa miaka mingi na hakuna hatua yoyote iliyochaguliwa."
Lukaku ambaye ni mchezaji wa zamani wa United pamoja na Pogba na Rashford, wote wamelengwa katika mitandao ya kijamii.
Mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma alitukana siku ya jumamosi baada ya kuifunga Sheffield United , wakati huohuo mchezaji mwenzake Abraham na Yakou Meite wote walipokea ujumbe wa kibaguzi katika mtandao baada ya kukosa penati mwezi uliopita.
Bosi wa Chelsea Frank Lampard amezitaka kampuni za mitandao ya kijamii kufanya kazi zaidi ya kukomesha tabia hiyo.
Ubaguzi dhidi ya Pogba: Wito watolewa wachezaji kususia mitandao ya kijamii

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa timu ya soka upande wa akina dada nchini England Phil Neville amesema kuwa wachezaji wanapaswa kususia mitandao ya kijamii ili kutuma ujumbe mzito kwamba ubaguzi wa rangi hautakubaliwa.
Matamshi ya Neville yanajiri baada ya kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba kupokea machapisho ya ubaguzi wa rangi mitandaoni kufuatai hatua yake ya kukosa penalti wakati wa mechi iliotoka sare ya 1-1 dhidi ya Wolves siku ya Jumatatu.
''Lazima tuchukue hatua mwafaka sasa kama jamii ya kandanda. Tumeona na wachezaji wangu katika mitandao ya kijamii, ligi ya Premia na mabingwa wameona'' , alisema Neville.
''Sijui kama jamii ya soka tunafaa kususia mitandao ya kijamii , kwa sababu Twitter haitachukua hatua yoyote, instagram haitafanya lolote - wanakutumia barua pepe wakisema kwamba watachunguza lakini hakuna kinachofanyika''.













