Ezekiel Mutua, mdhibiti maadili ya sanaa chafu Kenya ni nani?

Ezekiel Mutua
Maelezo ya picha, Ezekiel Mutua hamepewa jina la "polisi wa maadili''
Muda wa kusoma: Dakika 5

''Polisi wa maadili nchini Kenya'' Ezekiel Mutua anakabiliana na ukosoaji baada ya kupiga marufuku nyimbo mbili maarufu, ingawa mwandishi wa habari huyo wa zamani anafurahia kazi yake.

Mwandishi wa BBC Ashley Lim anasimulia jinsi alivyokutana naye mjini Nairobi.

'Nililpokutana na bwana Mutua kitu cha kwanza nilichobaini ni ndevu zake zilikuwa zimechorwa na kalamu na alikuwa na tabasamu la ukarimu.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya udhibiti wa maudhui ya usanii nchini Kenya (KFCB) alinipokea kwa ukarimu katika ofisi yake , lakini nyuma ya ukarimu huu ana sifa ya kuwa '' polisi wa maadili " ambaye huweka marufuku dhidi ya filamu, nyimbo, na matangazo ya televisheni yenye maudhi ya kingono au mauhusiano ya jinsia moja.

Wimbo wenye maudhui ya ngono, matangazo ya biashara ya ngono yanayohamasisha watu kushiriki ''sherehe za ngono'' na filamu zilizowahusisha wapenzi wa jinsia moja zote zimekabiliwa na nguvu ya hatua za Bwana Mutua.

Lakini mwandishi huyo wa habari , ambaye amejitolea kuwa mkristo, anapinga kuitwa mdhibiti.

" Neno mdhibiti lina maana ya mtu kuwa na tabia za kidikteta au kikoloni ," Bwana Mtua aeleza.

Kwa sasa bwana Mutua anasema anaridhika na jina la "polisi wa maadili ''alilopewa, ingawa ilimchukua muda kulikubali.

Kwa ujumla , Kenya inafuata misingi ya utamaduni , lakini utamaduni huo umekuwa ukikosolewa na vijana.

Ezekiel Mutua
BBC
This country need me, but it needs more people to act as moral champions"
Ezekiel Mutua
Chief Executive, KFCB

Kupanuka kwa matumizi ya mitandao ya kijamii kumechochea mijadala ya wazi juu ya ngono, na wasanii wamekuwa wakifanya kazi zinazoelezea hayo.

"Kwa mara ya kwanza nilihisi mwenye mashaka sana wakati wakosoaji waliponiita polisi wa maadili, lakini mashaka yaliisha baada ya muda nilipobaini kuwa nchi hii inanihitaji na kwamba inahitaji kuwa na watu wanaofanya mambo kwa kuzingatia maadili ," alisema.

'Uchafu usiofaa'

Akiwa kiongozi wa KFCB tangu mwaka 2015, mara kwa mara Mutua amejipata katika malumbano na Wakenya wanaoelezea hisia zao mbalimbali juu ya maagizo yake

Kazi inayompa mamlaka ya kuweka viwango na makundi ya filamu na hakuna filamu yoyote inayoweza kuonyeshwa nchini Kenya bila kupitia viwango vinavyohitajika.

Pia anaamini kuwa ana mamlaka ya kusimamia matangazo yaanayopita kwenye Televisheni na mtandaoni, lakini kuna hisia tofauti kuhusiana na wapi mamlaka yake ya udhibiti yanafika.

katika hatua yake ya hivi karibuni Jumanne , bwana Mutua alipiaga marufuku miziki miwili maarufu ambayo ni Wamlambez na Tetema kuchezwa katika sehemu za umma, isipokuwa kwenye vilabu na baa.

Katika ujumbe wake wa Twitter alisema kuwa nyimbo hizo mbili zilikuwa ni "ponografia halisi "na "uchafu ambao si mzuri kusikilizwa palipo na wa watu rika mchanganyiko.''

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Presentational white space

Maneno ya nyimbo za Wamlambez, yalitolewa Aprili, yakiwa kwa lugha ya Sheng (lugha ya mtaani) ambayo hutumiwa na vijana kote nchini Kenya , yakijumuisha maneno ya ngono.

Wimbo huo ulioimbwa na kikundi cha Kenya 'Sailors' ni maarufu kuliko maneno yake "wamlambez" na "wamnyonyez" - maneno ya mafumbo yenye maana "lamba" na "nyonya" - yamekuwa ni maneno ya kawaida katika mikusanyiko ya vijana..

Video ambayo imekuwa ikiangaliwa na watu karibu milioni nne kwenye mtandao wa YouTube, pia ina staili chafu za kucheza.

Bwana Mutua Mutua pia aliwakosoa viongozi wa kitaifa kwa kuimba nyimbo "za aibu katika umma ".

Diamond Platnumz
Maelezo ya picha, Maneno ya wimbo wa msanii wa Tanzania uliitwa "uchafu " na mdhibiti huyo wa Kenya

Maneno ya wimbo Tetema wa msanii wa Tanzania Diamond Platnumz, yametajwa na Bwana Mutua kama uchafu.

Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa Twitter alituma ujumbe huu akiunga mkono marufuku dhidi ya Wamlambezi ambapo alisema wimbo huo ni "aibu.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Presentational white space

lakini kuna mwingine ambaye alimkosoa Mutua kwa kufanya maamuzi kwa ajili ya watu wazima.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Presentational white space

Miongoni mwa watu wengi ambao niliozungumza nao katika mji mkuu , Nairobi, waliunga mkono hatua ya Bwana Mutua . Baadhi waliniambia kuwa wanafikiri angechukua hatua hiyo mapema kwa sababu sasa hivi hata watoto tayari wameshaanza kuziimba nyimbo hizo.

Mwezi Aprili , alipiga marufuku wimbo wa mwanamuziki wa Kenya Alvin, ambaye anafahamika kama Alvindo, unaoitwa 'Takataka' , akisema ulichochea ghasia dhidi ya wanawake kukataliwa na wanaume.

The music group Sailors

Chanzo cha picha, @Sailors254

Maelezo ya picha, Kikundi cha muziki cha Sailors kilichoimba wimbo ''Wamlambez''

'Nyimbo za ushetani'

" Wimbo wa Takataka umeimbwa kwa lugha katili unaowafanya wanawake kuonekana kama vifaa na kuhimiza wanaume waumizwe ," alisema Bwana Mutua katika mkutano na waandishi wa habari.

Pia alisema kuwa ni jambo la kuhofia kuwa kwanza wimbo huo haukuwasilishwa kwenye mamlaka hiyo ili uweze kukaguliwa.

"Kuanzia leo, wimbo Takataka haupaswi kuchezwa mbele ya hadhira wala kwenye chombo chochote cha utangazaji eneo lolote katika jamuhuri ya Kenya. Hakuna Dj anayepaswa kucheza iwe katika kituo cha utangazaji au katika burudani yoyote ," ilieleza sehemu ya taarifa.

Bodi hiyo ilisema kuwa kumekuwana vifo vingi vya wapenzi katika siku za hivi karibuni na muziki wa aina hiyo, ujumbe uliomo unachochea aina hii ya uhalifu.

Bwan Mutua pia alikosoa mwanamuzki mwingine maariufu nchini Kenya, Akothee, mwezi Februari baada ya picha zake alipozopiga akiwa kwenye shoo ya muziki , akiwa amevalia nguo za ndani kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema kuwa zilikuwa ni "uchafu", "ujinga " na za "kishetani".

Ruka X ujumbe, 4
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 4

Presentational white space

Mwaka 2016, alipiga marufuku matangazo ya picha yaliyokuwa yakisambaa mjini Nairobi yakisema "hakuna mtu atakayerudi nyumbani na ubikra ", na itakuwa "moja ya usiku wa kupoteza akili ".

Sherehe hiyo iliandaliwa na ili watu waweze kuuza na kununua filamu za ponografia na matumizi ya dawa za kulevya , Alisema Bwana Mutua wakati huo.

Samantha Mugatsia and Sheila Munyiva in Rafiki

Chanzo cha picha, Rafiki

Maelezo ya picha, Samantha Mugatsia (kushoto) na Sheila Munyiva wakicheza kama Kena na Ziki katika filamu ya rafiki

Moja ya maamuzi aliyoyachukua yaliyomfanya afahamike zaidi duniani ni yale aliyoyachukua ,mwaka 2018, ambapo bodi yake KFCB ilipiga marufuku filamu 'Rafiki', iliyoongozwa na Wanuri Kahiu.

Filamu ambayo ilikuwa ni karibu ishiriki katika tamasha la Cannes Film Festival, ilielezea hadithi ya wasichana wawili , Kena na Ziki, waliokutana na kuoana.

lakini bodi hiyo ilisema kuwa imezuwiwa kutokana na "kuwa na jina la wapenzi wa jinsia moja na ililenga kuboresha mapenzi ya jinsia moja ya wanawake ". Kitendo ambacho ni kinyume cha sheria nchini na mhusika huhukumia miaka 14 jela.