Kenya: Filamu iliyofungiwa ya wapenzi wa jinsia moja yashinda tuzo

Still from Rafiki film

Chanzo cha picha, Rafiki

Maelezo ya picha, Samantha Mugatsia alicheza kama Kena, ambaye alivutiwa kimapenzi na Ziki ambaye alicheza kama Sheila Munyiva
Muda wa kusoma: Dakika 1

Tamasha kubwa la filamu barani Afrika limetoa tuzo kwa muigizaji wa Kenya licha ya kuigiza tabia za mapenzi ya jinsia moja katika filamu iliyofungiwa kuonyeshwa nchini mwake.

Tamasha hilo lijulikanalo kama 'Fespaco film festival' lilifanyika nchini Burkina Faso na kumpa tuzo Samantha Mugatsia kama msanii mahiri katika filamu ya Rafiki.

Bodi ya filamu nchini Kenya ilifungia filamu hiyo kuonyeshwa mwaka jana kwa madai ya kuchochea mapenzi ya jinsia moja.

Kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni jambo ambalo halikubali nchini Kenya, tangu sheria ya enzi ya utawala wa ukoloni wa Uingereza.

Chini ya sheria za Kenya, mapenzi ya jinsia moja ni hatia iliyo na hukumu ya miaka 14 gerezani.

Bodi ya filamu ilitoa onyo kwa yeyote atakayebainika anafanya

Rafiki ni filamu ambayo imeangazia simulizi ya mapenzi kati ya wanawake wenye umri mdogo ambao walikutana na kupendana.

Mahusiano hayo yalikuwa yana vipingamizi vingi kutokana na ubaguzi dhidi yao licha ya familia zao kupinga kile ambacho siasa kimetenganisha.

Filamu hii imelenga imelenga mti ujulikanao kama Jambula, na simulizi hii iliandikwa na mwandishi kutoka Uganda aitwaye Monica Arac de Nyeko.

Mara baada ya muigizaji huyo kushinda , mkurugenzi wa Wanuri Kahiu aliandika katika kurasa yake ya Tweeter: Tamasha kongwe zaidi la filamu barani Afrika limemtambua uigizaji ambao haukubaliki...ninajivunia

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

.

Tamasha hilo lilimtunuku muigizaji bora wa kiume Marc Zinga kwa kushiriki katika filamu ya 'The Mercy of the Jungle', ambayo alicheza kama askari aliyepotea porini wakati wa vita nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya kongo.

Muongozaji wa filamu hiyo ni Mnyaruanda Joel Karekezi,ambaye alishinda zawadi kubwa zaidi katika tamasha la filamu ijulikanayo kama 'golden stallion of Yennenga'.