Inawezekana wanawake na wanaume kuchangamana kwenye kikosi kimoja?

Stephanie Labbe

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Stephanie Labbe ni mwanadada maarufu sana kwenye kwenye mchezo wa kandanda kutokana na uwezo wake mkubwa kwenye nafasi ya mlinda mlango.

Ushindi wa Canada wa 1-0 dhidi ya Cameroon kwenye michuano ya Fifa ya kombe la dunia mwaka 2019 siku ya Jumatatu ilifanya kufikia mchezo wake wa 30 kuwa na hati safi, ikimaanisha kuwa hakuruhusu mpira kuingia golini katika takribani nusu ya michezo aliyoicheza kuiwakilisha nchi yake.

Lakini Labbe alitawala kwenye vichwa vya habari kutokana na jaribio lake kujiunga na timu ya wanaume mwaka 2018 katika klabu ya Calgary Foothills nchini Canada inayochezea lihi ya pili

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Mlinda mlango huyo alifanikiwa kukichezea kikosi hicho na hata mechi ya kirafiki kabla ya msimu, kabla mamlaka kupiga marufuku ushiriki wake kwa maelezo kuwa ligi ya USL ni ligi inayohusisha ''jinsi maalum''.

Maribel Dominguez

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa sasa akiwa na miaka 32, Labbe amekuwa akipambana na ubaguzi wa kijinsia kwenye mchezo wa kandanda.

Mwaka 2004, shirikisho la soka duniani,FIFA, lilielekeza kuwa. ''Lazima kuwe na utofautishaji wa wazi kabisa kati ya soka ya wanawake na wanaume.Ilikuwa ni majibu yaliyofuatiwa na kura ya veto

Marta akikabiliana na mpinzania wa kiume

Chanzo cha picha, Getty Images

"This is laid down in league football and in international matches by the existence of gender-specific competitions, and the Laws of the Game and Fifa's regulations do not provide for any exception," the governing body said at the time.

That also seems to be the general public opinion and a common argument is that men and women have different physical characteristics and abilities.

Mabadiliko Olimpiki

Moja ya mechi za jinsia mchanganyiko

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika michezo ya Olimpiki ya majira ya joto walishindana kwenye mbio za farasi na mashindano ya boti, na pia kuna matukio michezo inayofanyika kushirikisha jinsia zote mbili katika tennis na mpira wa vinyoya-mwaka 2017, kamati ya Olimpiki ilitangaza kuwa michezo ya Tokyo ya mwaka 2020 itakuwa na mchanganyiko wa jinsia katika michuano ya mbio za kupokezana vijiti, kuogelea na mbio za baiskeli(triathlon)

Lakini kandanda si mchezo wa kuhusisha jinsia ya kike na kiume kwa wakati mmoja, kwa sababu zilizoelezwa kuwa za kisayansi.

Paul Bradley, mwanasayansi wa michezo katika Chuo kikuu ch John Moore mjini Liverpool, amefanya tafiti kadhaa kwa wacheza kandanda wa kike, ikiwemo utafiti wa mwaka 2013 ukionyesha takwimu kati ya wanaume na wanawake walioshiriki michuano ya ligi ya Uefa.

Wavulana na wasichana mafunzoni

Chanzo cha picha, Getty Images

Bradley na jopo lake wakapata tofauti muhimu kwenye upande wa nguvu, na umbali wanaoufikia wanapokimbia.

Lakini utafiti umegundua kuwa wanawake wanafanya vizuri kuliko wanaume.Na wanasayansi wanaamini kuwa mchezo wa wanawake kwa ujumla unakuja juu

''pamoja na mabadiliko makubwa katika ligi ya wanawake katika kipindi cha miaka michache iliyopita, tunatarajia mapinduzi kwenye mchezo huo kwa upande wa wanawake,'' Bradley aliiambia BBC.

''Hasa kwa upande wa sayansi ya michezo, nguvu, chakula na kufundisha.''

Mwanadada akiwa mafunzoni

Chanzo cha picha, Getty Images

Akili dhidi ya misuli

Wachezaji wafupi, wasio na nguvu na wasio na kasi ni uthibitisho kuwa uwanja huohuo unaweza kuchezwa na wanawake na wanaume.

Mchezaji ambaye amekua mwanasoka bora wa dunia mara sita, Marta kutoka Brazil mwaka jana mwezi Disemba alisema hatakataa mwaliko wa kujiunga na kikosi cha wanaume.

''Nimecheza mara nyingi na wanaume na baadhi yao walikua na nguvu na warefu zaidi yangu.Ninajua kwa maumbile walinitishia uwanjani lakini nilipambana nao kwa kutumia akili,'' Alieleza Marta.

Mchezaji akiwa amejeruhiwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Akizungumza mwezi uliopita kuhusu uzoefu wake na timu ya Calgary Foothills,Stephanie Labbe alikiri kuwa alijisikia dhaifu mbele ya wanaume wengi.

''Kwa nafasi ya mlinda mlango nafikiri ni vizuri kwa kuwa unapambana na mikwaju ya haraka, mikwaju ya nguvu, na kasi ya mchezo ni ya haraka,'' aliliambia shirika la habari la Ufaransa, France Presse.

Hata hivyo,angeweza kuchezea timu hiyo kama asingezuiwa na mamlaka za ligi.

''Ilikua vigumu kuambiwa kuwa huwezi kucheza kwa sababu ambayo iko nje ya uwezo wako.Anasema Labbe.

Makao makuu ya Fifa, Zurich

Chanzo cha picha, Getty Images

''Si kitu ambacho ninaweza kwenda nyumbani nikafanyia kazi na kubadili.Jinsia yangu ni jinsia yangu.''

Federico Luzzi,mhadhiri wa filosofia chuo cha Aberdeen (Scotland) ameita ubaguzi wa Fifa kuhusu jinsia ni ''makosa ambayo hayajabainika kwenye soka''.

Hata kama ilikua kweli kuwa hakuna mwanasoka wa kike aliye mzuri sawa na wa kiume, si sawa kwa mashirikisho kuamua kuhusu wanawake kutokua bora,'' aliandika.

Wanaharakati wamedai kuwa ni ''salama'' kwa wanawake, kujadili tafiti zinazoonyesha kuwa wanawake wacheza soka wako hatarini zaidi kupata majeraha kuliko wanaume, kama vile kubanwa misuli, kuumia miguu au vifundo vya miguu.

Wacheza soka wakiwa mafunzoni

Chanzo cha picha, Getty Images

''Hata kama wastani wa wanawake wako hatarini kupata majeraha, kuwapiga marufuku wanawake ni jambo ambalo haliwezi kuwa sababu.Kama ingekuwa hivyo wanaume ambao wako hatarini kupata majeraha nao wangepigwa marufuku pia kucheza,''Luzzi anaeleza.

Vizazi vipya vinaweza kukua vikiwa vimezoea kuchaza soka la mchanganyiko

Chanzo cha picha, Getty Images

''Soka la mchanganyiko wa jinsia litasaidia kizazi kijacho kutokubali ubaguzi kwenye mchezo huo, alieleza.

''Tunapaswa kuona wacheza kandanda wanawake wakipinga ubaguzi na vikwazo katika soka.Mabadiliko makubwa yatajitokeza katika kipindi cha miaka kumi ijayo.''