Tales Soares: Mwanamitindo wa kiume aliyefariki baada 'catwalk' São Paulo

Paramedics attend to Tales Soares, who collapsed on the catwalk at Sao Paulo Fashion Week. He was later confirmed to have died

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamitindo Tales Soares akisaidiawa na maafisa wa usalama
Muda wa kusoma: Dakika 1

Mwanamitindo wa kiume wa miaka 26 amefariki alipokua akifanya onyesho la mavazi katika tamasha la mitindo la São Paulo.

Tales Soares aliripotiwa kuanguka baada ya kutegwa na kamba za viatu alivyokuwa amevalia.

Waliyohudhuria tamasha hilo awali walifikiria kuanguka kwake kulikua sehemu onyesho lake.

Lakini walishtukia amebebwa kutoka ukumbini hapo na walinda usalama akiwa ameziraia.

Alipelekwa hospitali lakini madktari hawakuweza kuyaokoa maisha yake.

Kanda za video zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinamuonesha Soares akitembea kwa mwendo wa madaha kisha akageuka na kuangalia nyuma kabla ya kupatwa na kisunzi na kuanguka chiini

"Tunasikitika kumpoteza Tales na tunatuma rambi rambi zetu kwa familia yake," ilisema taarifa yao".

Saa kadhaa kabla ya mkasa huo modo huyo, aliweka picha zake kwenye akaunti yake ya Instagram ana kuzunzummzia tamasha hilo.

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe

Presentational white space