Unaweza kuuelewa ujumbe wa kwanza CIA wa Instagram

Ujumbe wa kwanza wa CIAuliotumwa kwenye Instagram

Chanzo cha picha, CIA

Maelezo ya picha, CIA imeushirikisha umma ujumbe wake wa kwanza uliotuma kwenye Instagram

Shirika la ujasusi la Marekani (CIA) limetuma ujumbe wake kwenye ukurasa wake wa Instagram, utakaoliwezesha shirika hilo kutekeleza majukumu yake.

Likijulikana kwa mbinu zake za usiri, busara na kutotabirika linapofanya ujasusi, Shirika la Marekani la huduma ujasusi katika mataifa ya kigeni limeonyesha ujasiri wake kwa kujiunga na mtandao wa habari wa kijamii.

" Sisi tuko mstari wa mbele katika ulinzi wa taifa ," Utambulisho wa akaunti hiyo ya Istagram umeandikwa , kuonyesha umakini unaozingatiwa na shirika lenyewe.

Ni ujumbe wa kwanza , lakini umetolewa katika lugha ambayo ina machenga. Ujumbe huu unajumuisha picha ya dawati lililojaa vitu vilivyosambazwa juu yake vitakavyokufanya uwe mdadisi , kuanzia wigi hadi sarafu za noti za benki za mataifa mbali mbali ya kigeni.

Picha gii iliyochukuliwa katika makao makuu ya CIA mjini Langley, Virginia, ina kiungohabari katika picha kinachosema : "nitakupeleleza kwa macho yangu madogo …"

Changamoto inaweza kuwa ni kutambua vitu vilivyomo kwenye picha. Na kuelewa ni nini maana yake , msemaji wa CIA alikiambia kituo cha habari cha CBS News kuwa vingi kati ya vitu vilivyomo kwenye picha hiyo ni vya wafanyakazi wa CIA

Unaweza kutambua vingapi ?

Akaunti hii ilifunguliwa kama sehemu ya mkakati wa CIA wa kuwaajiri maafisa vijana wa kizazi hiki, linasema shirika hili na wachambuzi.

Wengi miongoni mwa watumiaji wa Instagram wako chini ya umri wa miaka 30.

"Kujiunga na Instagramni njia nyimngine ya kushirikisha umma hadithi za CIA na kuwaajiri Wamarekani vijana wenye vipaji kufanya kazi hapa ," amesema msemaji wa CIA.

" Kupitia akaunti ya Instagram, tutatoa mwangaza kuhusu maisha ya shirika , lakini hatuwezi kutoa ahadi ya kuona picha zozote za selfie kutoka maeneo ya siri ."

Mkurugenzi wa CIA Gina Haspel alitangaza mipango ya kuanzisha akaunti wiki iliyopita wakati alipohudhuria kipindi cha maswali na majibu katika Chuo kikuu cha Auburn cha Alabama.

Je ni vifaa gani vilivyomo kwenye picha hii?

Ujumbe wa kwanza uliotumwa na CIA kwenye Instagram

Chanzo cha picha, CIA

Maelezo ya picha, Vitu , baadhi yake vikiwa ni mali ya wafanyakazi wa CIA vinaonekana kwenye picha

Hii ni orodha ndefu ya vitu vilivyomo kwenye picha hii ya CIA:

1) Mmea, uliojumuishwa kama ishara ya kuelezea ujasusi wa CIA katika mataifa ya kigeni " mimea".

2) Saa ambayo imewekwa kwenye muda wa 8:46, muda ambao ndege ilishambulia mnara wa Korea Kaskazini wakati wa shambulio la kigaidi la World Trade Center tarere 9/11/ 2001.

3) Bendera ya Uchina , moja ya mahasimu wakuu wa Marekani katika bara Asia.

4) Bundi mwenye rangi ya dhahabu anasemekana kuwakilisha Athena, mungu wa busara wa Kigiriki . Bundi huyo alitolewa na Mkuu wa shughuli za CIA Andy Makridis.

5) Kile kinachoonekana kuwa hirizi inayofanana kama jicho la shetani -huenda inamaanisha hatari za uso wa maafisa wa CIA ?

6) Sanaa yenye picha ya Tony Mendez, afisa wa CIA ambaye alijifanya kuwa mtengenezaji wa filamu kuwaokoa wamarekani sita waliokuwa wametekwa nyara nchini Iran mwka 1980.

7) Vipande viwili vya karatasi vilivyokatwa , vinavyoripotiwa kutumiwa na wakala wa CIA kujitambulisha kwa wenzao.

8) Wigi lenye mvi ambalo huenda liliwahi kuvaliwa na wakala wa siri wa CIA.

9) kitambulisho chenye picha ya Bi Haspel

10) mfuko wa siri kubwa, unaotumiwa na wakala wa CIA kuharibu ushahidi.

Mkurugenzi wa CIA Gina Haspel - akiwa ameketi chini

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa CIA Gina Haspel amezungumzia juu ya kazi zao katika Instagram

Akaunti hiyo ya Instagram kulingana na Bi Haspel ni mfano juu ya namna huduma ya ujasusi inataka kuendana na wakati huu wa digitali.

Hata hivyo CIA si shirika geni katika mitandao ya kijamii. Ina akaunti za Twitter na Facebook, ambapo ilijiunga na mipandao hiyo mwaka 2014.