Mpasuaji wa saratani ya matiti aliyepata saratani ya matiti

Liz O'Riordan

Chanzo cha picha, Alex Kilbee

Maelezo ya picha, Liz O'Riordan alipatikana na saratani ya matiti kwa mara ya kwanza 2015

"Kama wanawake wengine, sikufanyiwa uchunguzi wa matiti yangu. Nilifikiri, haiwezi kutokea kwangu -Mimi ni daktari wa upasuaji wa saratani ya matiti'."

Liz O'Riordan aliishia kuacha kazi aliyoisomea kwa miaka 20, baada ya yeye mwenyewe binafsi kupatikana na saratani ya matiti.

Mwaka 2015, akiwa na umri wa miaka 40, alifanyiwa upasuaji wa kuondolewa matiti yake (mastectomy kwa lugha ya kitaalamu) na mwezi Mei maradhi hayo yakarejea tena.

Dkt O'Riordan alidhani angekuwa mpasuaji wa saratani ya matiti kwa walau miaka 20, lakini matokeo yake ni kwamba alifanya kazi kwa miaka miwili tu.

Baada ya kufanyiwa matibabu ya kuchoma seli za saratani (radiotherapy kwa mara ya pili saratani ilimfanya ashindwe kutumia mabega yake , jambo lililomfanya achukue uamusi ''mgumu kisaikolojia'' wa kuacha kufanya upasuaji wa wagonjwa.

Liz O'Riordan

Chanzo cha picha, John Godwin

Maelezo ya picha, Dr O'Riordan kwa sasa anajitolea katika kampuni ya kijamii inayojishughulisha na saratani

Kabla hajabainika na saratani Dr O'Riordan alipata uvimbe ambao baadaye ulibainika kuwa ni wa kawaida, huku vipimo vya saratani miezi sita ya awali vilibaini kuwa matiti yake yalikuwa yenye afya.

Lakini uvimbe mwingine ulijitokeza na kukuwa na mama yake akamshauri kufanyiwa kipimo cha skani. Mpasuaji anayeishi karibu na na eneo la St Edmunds - Suffolk, alifahamu matokeo ya uchunguzi wake mara moja.

"Wagonjwa wengi hupewa taarifa chache sana. Niliona skani ile na nikajua nitahitaji kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa matiti ,niloifahamu kuwa huenda nikahitaji matibabu ya chemotherapy kwasababu nilikuwa nina umri mdogo, na nilikuwa sahihi kuwa muda wangu wa kuishi ni miaka 10 hilo lilinijia akilini mara moja."

Dr O'Riordan, mwenye umri wa miaka 43, anasema sio madaktari wengi wanaopata maradhi waliyoyasomea ; hakuna daktari katika idara yake kwenye hospitali ya Ipswich aliye na ugonjwa huo aliousomea.

Dermot na mumewe Liz O'Riordan

Chanzo cha picha, Liz O'Riordan

Maelezo ya picha, Liz O'Riordan na mumewe Dermot wakishindana katika mbio za baiskeli za RideLondon 100 mwaka 2017

Mara ya kwanza "aliogopa sana", na maswali mengi yakamjia akilini mwake.

"Ni kwa kiwango gani naweza kumshirikisha mume wangu na wazazi taarifa hii ? Ni kwa kiwango gani naweza kuacha kuwa mpasuaji wa saratani na kuwa mgonjwa tu?''

Ingawa alifahamu fika kilichokuwa kinatokea kwa mwili wake, hakufahamu angekuwa na uzoefu gani wa maradhi yenyewe.

"Nafahamu vile inavyokuwa kumuambia mtu kuwa ana saratani ya matiti.

"Sikufahamu inakuwaje mtu anapoishi na kovu lililokakamaa kifuani nikajiambia ...futa machozi yako, ondoka kliniki, nenda chumba cha kumsubiri daktari, nenda kwenye veranda ya hospitali uingie kwenye eneo la kuegesha magari na uanze kuomboleza ."

Kwapa baada ya upasuaji

Chanzo cha picha, Liz O'Riordan

Maelezo ya picha, Kofu, uvimbe na kujazwa kwa nyama za mwili kwenye tundu vilimsababishia Daktari O'Riordan kushindwa kugeuza mabega

Baada ya kuzungumzia suala hilo na mumewe Dermot, hata hivyo aliamua kutangaza ugonjwa wake katika twitter yake wenye wafuasi 1,500 , ambao walimfahamu zaidi kwa kupenda kwake kuoka who mostly knew her through her love of baking, kufanya mazowezi ya mwili na taaluma yake ya udaktari.

Mitandao ya habari ya kijamii, alisema ilikuwa sehemu ya maisha yake na huko alipata "uungaji mkono mkubwa".

"Ni mgonjwa ambaye aliniambia jinsi ya kuishi na saratani.

" Kilawakati kuna mtu ambaye huamka saa tisa usiku kuzungumza nae wakati unapokea matibabu ya saratani -steroid ."

Mitandao ya kijamii pia ilimkutanisha na wataalamu wengine wa tiba ya saratani wenye saratani ,na tangu wakati huo ameanzisha kikundi cha WhatsApp cha madaktari wenye magonjwa.

Liz O'Riordan

Chanzo cha picha, John Godwin

Maelezo ya picha, The former consultant found she was "reliving" her own cancer when she returned to her department

Baada ya matibabu ya saratani , Dkt. O'Riordan alirejea katika hospitali ya Ipswich kama daktari wa upasuaji. lakini anasema hakufahamu jinsi itakavyokuwa "changamoto ya kihisia" kwake.

Alisema kuwa na saratani mwenyewe, angeweza kuwasaidia watu kwa namna tofauti.

"Lakini kilikuwa ni kitu kigumu sana nilichowahi kukifanya ''.

"Wakati unapotoa taarifa mbaya kwa mara ya kwanza na kuwaambia wanawake kuwa wana saratani, ni jambo linalokuwa gumu sana , lakini nilikuwa ninatoa taarifa na niliweza kujiona mimi na mume wangu namna tulivyokuwa nilipopokea taarifa kwamba nina saratani.

"Pia unakuwa na shauku kubwa ya kuungana na mtu mwingine mwenye tatizo kama lako, lakini huwezi - walikuwa ni wagonjwa wangu."

Aliongeza kuwa : "Niliachwa na maumivu yangu baada ya kuondolewa matiti na mara ghafla nikaanza upasuaji- nilifahamu fikakwamba ningeweza kuwapa maumivu niliyonayo , na sikutaka kufanya hivyo na ilikuwa vigumu sana , vigumu sana."

Liz O'Riordan

Chanzo cha picha, Liz O'Riordan

Maelezo ya picha, Akisugua mikono kabla ya upasuaji

Alisema pia alihangaika kuketi katika mikutano ya madaktari inayojadili matokeo ya uchunguzi ya mgonjwa.

"Katika mkutano wangu wa kwazna siku za nyuma, mgonjwa wangu alisikia kuhusu saratani yangu. Alikuwa na umri sawa na wangu- alikuwa na saratani sawa na yangu, alikuwa na matibabu kama yangu - alikuwa ni sawa na kuniweka mimi kwenye karatasi.

"Nilisikia madaktari wenzangu wakisema 'ile ni mbaya sana'."

manamo mwaka 2018, saratani ya Dkt O'Riordan ilirejea kwenye kwapa lile lile. Ilipatikana alipokuwa akufanyiwa kipimo cha skani kabla ya kuondolewa kwa titi lake lililokarabatiwa ambalo lilikuwa limemsababishia maumivu makubwa.

Ilibidi apewe dose ya pili ya tiba ya radiotherapy kwenye eneo eneo lile lile , "jambo ambalo ni nadra sana kufanyika".

Alionywa kuwa huenda asiweze kunyenyua mkono kama kawaida baada ya upasuaji wa pili , lakini baada ya kufanyiwa upasuaji huo kulikuwa na shimo.

Matokeo yalikuwa ni kuwa na makovu zaidi, uvimbe na ukusanyaji wa nyama laini , kuziba shimo hilo yaliyomsababishia kupungua kw auwezo wa kugeuza mabega kama ilivyotarajiwa , hii ikimaanisha kuwa nguvu za mikono zilipungua.

Dkt Liz O'Riordan

Chanzo cha picha, Dermot O'Riordan

Maelezo ya picha, Dkt O'Riordan akifichua sanamu yake katika bustani ya Bury St Edmunds Abbey Gardens mwaka jana

Anasema wafanyakazi wake walifanya kila liwezekanalo kumsaidia kurejea kazini tena kwa mara ya pili.

"Nilikuwa na usaidizi mkubwa wa matibabu ya kisaikolojia, niloimuona Daktari wa upasuaji wa mifupa - kwasababu kilikuwa ni kitu kikubwa kusema , 'kitu ambacho nimekuwa nikikifanya kwa miaka 20 ya maisha yangu, na shahada na stashahada tofauti, mitihani na mafunzo kuwa mtaalamu katika kitu ninachokipenda , ambacho sitakifanya tena'.

"Ninaweza kuendelea na maisha yangu, lakini kuweza kufanya kazi kwa utulivu ,hicho ni kitu ambacho hakitokea tena ," alisema.

Kwa sasa Dkt O'Riordan alihisi haja ya kisaikolojia ya "kuwa huru na saratani ", hususani kwamba alirejea kazini kabla ya kufadhaishwa na kuteje tena kwa saratani.

Zaidi ya hayo, hatari ya kurejea kwa saratani ilikuwa ni ya juu kuliko kabla , na kulikuwa na hatari kuwa inaweza kuja mahali pengine.

Baada ya takribani miezi minne alichukua uamuzi kuwa taaluma yake ya upasuaji imekwisha.

"Lilikuwa ni jambo la uchungu na gumu gumu sana kusema kwaheri."

Liz O'Riordan

Chanzo cha picha, Liz O'Riordan

Maelezo ya picha, Dr O'Riordan akishiriki sehemu ya mashindano ya mtu jasiri katika eneo la Staffordshirebaada ya matibabu mwaka 2017

Kwa ujasiri alionao , sasa anawashauri watu juu ya haki zao za kurejea kazini baada ya matibabu ya saratani.

Dkt O'Riordan, ambaye mumewe ni Daktari wa upasuaji, anasema alikuwa na ''bahati'' kuweza kulazimika kufanya kazi ya kulipwa.

Hivi karibuni alianza kujitolea kama balozi wa kampuni ya kijamii inayofanya kazi za saratani , ambayo ilimshauri juu ya hki zake za ajirabaada ya kuamua kurejea kazini mwaka 2017,kufuatia matibabu yake ya kwanza ya saratani.

Mkurugenzi wa muda wa hospitali alikuwa amemuambia wakati huo kuwa anatarajiwa kuwa amerejea kazini baada ya wiki nne.

"Nilikuwa bado nina uchovu na kujaribu kurejesha ubongo wangu kufanya kazi tena ," alisema Dkt O'Riordan.

"Sikuelewa kuwa kama una saratani , unawekwa kwenye kundi la watu wasiojiweza chini ya sheria ya usawa na waajiri wanatakiwa kufanya mabadiliko ya kikazi kukuruhusu kurejea kazini.

" Kwa hiyo watu wengi huhangaika kuhakikisha maisha yao yanarejea kuwa ya kawaida wakati wana saratani, lakini ni vigumu sana kurejea kazini na waajiri wengi hawajui namna ya kuwasaidia wagonjwa wa saratani - au kufahamu ikiwa wanapaswa kuwasaidia."

Liz O'Riordan

Chanzo cha picha, Liz O'Riordan

Maelezo ya picha, Dkt O'Riordan, alipigwa picha alipokuwa akizungumza Stuttgart juu ya huduma ya wagonjwa, pia ni mzungumzaji wa umma mwenye taaluma hiyo

Dkt. O'Riordanalisema kuwa wengi miongoni mwa watu wanaotoa mafunzo ya saratani katika kituo cha Working with Cancer wameishawahi kuwa na ugonjwa huo binafsi na " wanaupata".

pamoja na kutoa taarifa juu ya haki zao, huwaandaa wafanyakazi kwa ajili ya kuwasaidia kisaikolojia.

Kutokana na tiba ya Kimotherapy, Dkt O'Riordan ananywele fupi.

Msaidizi wake wa kisaikolojia alimuuliza: "Utafany anini watu wakishindwa kukutambua?"

Alipuuza jambo hilo, hadi siku moja alipobaini kuwa mfanyakazi mwenzake alikuwa anazungumzia namna alivyoshindwa kumtambua ni nani.

Maandalizi aliyoyafanywa na taasisi ya Working with Cancer kwa kiasi kikubwa yalikuwa ni kumsaidia kuepuka hali yoyote ya kumuaibisha au kumsikitisha.

Kabla ya kurejea kazini alimuandikia meneja wake na kuelezea kuwa angefurahia kuzungumzia ugonjwa wake na wafanyakazi wenzake , lakini sio wakati wa saa za kazi.

"Unayo haki ya kuuliza mambo kuwa rahisi kwako . Hawawezi kukufukuza kazi kwasababu hupo utakuwa ni ubaguzi."

Daktari huyo wa zamani wa upasuaji amesema kazi yake kama balozi imemsaidia katika kurudisha tena ari ya kuishi maisha yenye sababu .

"Kama Dkt wa upasuaji nilikuwa nikiwasaidia wanawake 70 au labda 100 kwa mwaka wenye saratani ya matiti.

"lakini sasa kupitia kitabu changu, blogi mazungumzo na kuwa balozi wa Working with Cancer,ninaweza kuwasaidia mamia, maelfu ya wanawake r."