Uingereza: Daktari wa upasuaji matiti afungwa jela miaka 15 kwa upasuaji usiofaa
Daktari wa upasuajia wa matiti Ian Paterson amefungwa jela miaka 15 kwa kufanya upasuaji usio muhimu.

Chanzo cha picha, SWNS
Paterson, mwenye umri wa miaka 59, aliwafanyia upasuaji wanawake tisa na mwanamume mmoja baada ya kuwadanganya kuwa walikuwa na saratani ya matiti.
Amepatikana na hatia ya mashtaka 17 ya kujeruhi kwa makusudi, baada ya kesi iliyodumu kwa mwezi mmoja uliopita.

Chanzo cha picha, Thinkstock
Jopo la mahakama ya Nottingham liliambiwa kuwa Paterson alizidisha ama kubuni hatari ya saratani.
Mahakama iliambiwa kuwa alifanya upasuaji wa matiti kwa "sababu zisizojulikana" ambazo ni pamoja na shauku ya "kupata pesa za ziada".








