Kimbunga Kenneth: Hofu ya mafuriko yatangazwa huku mvua kubwa ikinyesha Msumbiji

Kimbunga hicho kimesababisha mvua kubwa na mafuriko
Muda wa kusoma: Dakika 2

Kimbunga kikali kilipiga ndani ya taifa la Msumbiji siku ya Alhamisi , yapata mwezi mmoja baada ya kimbunga chengine kusababisha maafa ya mamia ya raia wa taifa hilo huku kikifanya uharibifu mkubwa katika eneo kubwa.

Kimbunga Kenneth kiliwasili nchini Msumbiji kikiwa na upepo wenye kasi ya kilomita 220 kwa saa yapata mwezi mmoja tu baada ya kimbunga chengine kuwawua mamia na kuwawacha wengi bila makao.

Kimbunga hicho hatahivyo kiliisha nguvu baada ya upepo kupungua lakini mvua kubwa ilifuatia na inatarajiwa kunyesha kwa muda.

Msumbiji ilikuwa bado inaendelea kukabiliana na athari za kimbunga Idai, ambacho kiliwaua zaidi ya watu 900 katika mataifa matatu mnamo mwezi Machi.

Mtu mmoja aliripotiwa kufariki nchini Msumbiji baadya ya kuripotiwa baada ya kuangukiwa na mti. Kimbunga hicho tayari kilikuwa kimewaua watu watatu katika kisiwa cha Comoros.

Lipi jipya?

Upepo ulipungua nguvu siku ya Ijumaa, lakini idara ya hali ya hewa nchini Ufaransa ilisema kuwa mvua yenye ya kati ya milimita 600-800 inatarajiwa kuwasili nchini Msumbiji katika siku kadhaa zijazo.

Mashirika ya misaa yamewasilisha malalamishi kuhusu athari za mvua hiyo katika jamii ambayo huenda ikasababisha mafuriko na mporomoko.

Kiwango cha mvua inayotarajiwa ni mara mbili ya kiwango cha mvua ilionyesha na kusababisha mafuriko.

Ramani ya ya njia mbayo kimbunga kingepitia
Presentational white space

Je maeneo yalioathirika yakoje?

Mkoa wa Cabo Delgado hauna watu wengi kama ulivyokuwa kabla ya kimbunga Idai, na kuna maeneo mengi ya juu katika eneo hilo.

Mbali na onyo lililotolewa na mamlaka kabla ya, kimbunga hicho kinaweza kusababisha maafa makubwa zaidi ya Idai.

Lakini ripoti zimesema kuwa maelfu ya makaazi yameharibiwa na upepo huo huku eneo hilo likishuhudia ghasia za wapiganaji katika miezi ya hivi karibuni.

Maelfu ya wakaazi wametoroka makaazi yao ili kutafuta hifadhi kutoka katika kambi za ghasia za watu walioachwa bila makao.

Na je mataifa mengine katika eneo hilo

Taifa la Comoro bado linajikwamua kutoka katika uhairibifu uliosababishwa na kimbunga hicho ,ambacho kilipigwa na upepo mkali na mvua kubwa.

Upepo umesababisha ukosefu wa umeme na uharibifu katika nyumba.

Katika maeneo mengine ya kusini yanayopakana na taifa jirani la Tanzania , mamlaka zimeagiza shule na biashara kufungwa.

Wakaazi wamesimama katika makaazi yalioharibiwa na mvua

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cyclone Kenneth imefanya uharibifu mkubwa katika kiswa cha Comoro.

Wakaazi wa mji wa kusini mwa Tanzania Mtwara waliagizwa mapema kuelekea katika maeneo ya juu , lakini onyo hilo lilitupiliwa mbali.

Shirika la msalaba mwekundu limesambaza picha katika mitandao ya kijamii .

Katika mtandao wa Twitter kundi hilo limejitolea kuzisaidia jamii zilizoathirika.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Licha ya Zimbabwe kuwa ndani , ya nchi kavu , maafisa wanasema kuwa wanaweka maafisa wao waliopo katika idara ya dharura katika hali ya tahadhari.

''Kutokana na Kimbunga Idai hatuwezi tena kuruhusu hali kuendelea bila kutoa tahadhari yoyote'', alisema mkurugenzi wa idara ya ulinzi wa raia Nathan Nkomo.