kujifungua mtoto kwa niaba ya mtu mwingine kunahatarisha watoto wachanga?

Watoto mapacha watatu

Chanzo cha picha, Getty Images

Kujifungua mtoto au watoto kwa niaba ya mwanamke mwingine soi jambo geni. Kwa miaka maelfu kadhaa wanawake wamekuwa wakiwachagua wengine kujifungua watoto wa niaba yao.

Hata hivyo, teknolojia ya uzazi wa kusaidiwa kwa upandikizaji wa mbegu za kiume katika yai la uzazi la mwanamuke na maarufu IVF, umelainisha mtizamo wa kitamaduni na hivyo kuwachochea wanawake wengi kupata watoto wakiwa na umri mkubwa jambo lililofanya uzazi wa njia ya kumbebea mimba mwanamke mwingine kuongezeka.

Katika miongo miwili iliyopita, limekuwa ni jambo la kawaida duniani. Hakuna idadi kamili inayofahamika kuhusu idadi ya watot wanaozaliwa kwa njia hiyo lakini mwaka 2012 sekta ya uzazi wa kubeba mimba kwa niaba ya mwanamke mwingine ilikuwa na thamani ya dola takriban Bilioni 6 kwa mwaka.

Nchini Uingereza pekee, idadi ya wazazi walioagiza wanawake kuwabebea mimba za watoto wao wana watoto mapacha watatu kuanzia 121 hadi 368 kufikia mwaka 2018 lakini idadi kamili ya matukio ya uzazi huu inaweza kuwa ni ya juu zaidi, kwani sio lazima kwa mtu kutuma maombi ya kufanya hivyo

Kim Kardashian

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kim Kardashiananatarajia kupata mtoto wa nne, wapili alipatikana kwa kubebewa mimba na mwanamke mwingine

Aina za kupata mtoto kwa kusaidiwa na mwanamke unayemchagua

Watoto wanaopatikana kwa njia ya mwanamke kujifungua kwa niaba ya mwanamke mwenzake huja kwa aina mbili - aina ya kwanza ni ile inayofahamika kama gestational, ambapo mama wa kujitolea hupandikizwa yai na mbegu ya uzazi ya mwanamume na ya pili iliyoanza kutumika tangu zamani ambapo yai la mwanamke anayejitolea kumzalia mwenzake hutumika.

Mchakato huu unaweza kuleta faida kubwa, hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kupata watoto kwa njia ya kawaida, kwa kuwaruhusu watu binafsi na wanandoa kuwa na watoto wao ''wenyewe'' bila kupitia mchakato mrefu wa kuasili.

Katika matukio mengi, mchakato huu hufanyika bila matatizo, Lakini uzazi huu ambao umekuwa maarufu umekuja kwa gharama za uanadamu na hadithi za uwezekano mateso wanayofanyiwa watoto wanaozaliwa kwa njia hii zimekuwa zikigonga vichwa vya habari katika miaka ya hivi karibuni.

Mtoto mchanga Gammy na mama aliyesaidia kumpata Pattaramon Chanbua, ambaye amemlea na kumkuza

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtoto mchanga Gammy na mama aliyesaidia kumpata Pattaramon Chanbua, ambaye amemlea na kumkuza

Kwa mfano, kisa cha baby Gammy kilichotisha ulimwengu, wakati ilipodaiwa kuwa wazazi waliogiza azaliwe kupitia mama mwingine walimuacha makusudi Gammy, ambaye alikuwa na matatizo ya afya ya ubongo -Down's syndrome, nchini Thailand, huku wakimchukua pacha wake msichana Pipah nyumbani kwao Australia.

Maelezo ya video, Kizungumkuti cha kujaliwa watoto wenye jinsia mbili

Mahakama baadae iliamuru kuwa hakuwa ametelekezwa, ingawa ilibainika kuwa baba aliyemuagiza awali alikuwa amepatikana na hatia ya makosa ya ubakaji wa watoto , jambo lililowafanya wengi wahofie maisha ya watoto hao wa uzazi wa kusaidiwa.

Baby Manji alizaliwa kupitia mama wa India baada ya wazazi kutoka Japan kuagiza apandikizwe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baby Manji alizaliwa kupitia mama wa India baada ya wazazi kutoka Japan kuagiza apandikizwe

Hofu ya kwanza juu ya maslahiya watoto, kuna pia mifano ya wanawake wanaosaidia uzazi wa kuwabebea mimba wenzao wanaotumiwa vibaya na wakala na kutunzwa katika hali mbaya kinyume na ubinadamu.

Wanawake wenye matatizo ya kifedha na kijamii wanaweza kulengwa kwa kazi ya kuwakutumiwa kuzaa watoto kwa ajili ya wanawake wenzao, na vile vile baadhi huvutiwa na pesa nyingi kufanya hivyo.

Maelezo ya sauti, Wazazi waliyo na watoto walemavu Zanzibar washauriwa kutowaficha majumbani

Hata hivyo kumekuwa na taarifa za mateso yanayofanywa na akina mama wanaosaidiwa kupata watoto kwa watoto wanaowapata kwa njia hiyo ,huku baadhi wakikataa kuwalipa wakina mama waliowasaidia kuwazalia watoto pale wanaposhindwa kupata masharti yao au hata mimba zinapotoka kwa bahati mbaya.

Hofu hizi zimesababisha nchi nyingi kufunga huduma yao ya awali ya kuwasaidia akina mama kupata watoto kwa kusaidiwa na wanawake wenzao huku mwaka jana Umoja wa mataifa ukionya kuwa uzazi wa kusaidiwa na mwanamke mwingine wa malipo kawaida ni sawa na kumuuza mtoto.

Wazazi wanaotarajiwa kusaidiwa kupata mtoto na mwanamke mwingine wakiwa wameketi katika chumba cha hospitali
Maelezo ya picha, Ukrainekimekuwa ni maarufu kwa uzazi wa ksaidiwa kupitia mwanamke anayelipwa

Kuhusu taarifa hii

Hii ni tathmini iliyoagizw ana BBC kutoka kwa wataalamu wanaofanya kazi nje ya shirika.

Maelezo ya sauti, Watoto wenye ulemavu wa ngozi walia ukiwa

Daktari Claire Fenton-Glynn ni mwalimu katika Chuo kikuu cha Cambridge kitivo cha sheria ambako amebobea katika maswala ya hali za watoto, sheria ya familia na sheria ya kimataifa ta haki za binadamu