Utajihisi vipi kufuatiliwa uwapo kazini kila wakati?

Chanzo cha picha, Getty Images
Je udukuzi wa maeneo ya kazi unasaidia kuboresha uzalishaji au ni njia ya kuwadhibiti wafanyakazi na kuvuna matokeo mabaya ya kazi?
Courtney Hagen Ford, mwenye umri wa miaka 34, aliacha kazi yake kama muhudumu wa benki kwasababu alibaini kuwa uchunguzwa aliokuwa akifanyiwa ''ulidunisha utu wake''.
Muajiri wake alikuwa akiingia kwenye kompyuta yake kwa kutumia programu ya software kuangalia ni wateja wangapi aliowahudumia walioweza kufikia hatua ya kuomba mkopona akaunti zisizo na malipo.
"Msukumo wa mauzo ulikuwa mkubwa," akakumbuka . "Ulikuwa ni wa kutisha kabisa."
Aliamua kuwa kuuza chakula cha haraka ingekuwa bora zaidi, lakini sababu ya kuacha kazi ya benki ilikuwa ni kutaka kusomea teknolojia ya uchunguzi wa kimtandao na kupata shahada ya udaktari wa taaluma hiyo.
Courtney si yeye pekee asiyependa aina hii ya kuchunguzwa, lakini inaendelea kukua kote duniani huku makampuni yakitaka kupata faida zaidi kutoka kwa wafanyakazi wao kwa kutumia raslimali chache iwezekanavyo.

Chanzo cha picha, Courtney Hagen Ford
Zaidi ya nusu ya makampuni yenye mapato ya zaidi ya $750m (£574m) kwa mwaka zilitumia njia "ambazo si za kawaida " kuwachunguza waajiriwa mwaka jana, anasema Brian Kropp, maka rais wa wa kampuni ya utafiti ya Gartner.
Hii ni pamoja na kutumia mbinu kama vile tathmini ya barua pep, matumizi ya kpmpyuta, na namna wafanyakazi wanavyotembea kutoka sehemu moja hadi nyingine ndani ya ofisi zao . Baadhi ya makampuni pia huchunguza viwango vya mapigo ya moyo na saa zao za kulala kuangalia namna inavyathiri kazi zao.
Mwaka 2015, 30% yalitumia mbinu hizo. Mwaka ujao, Bwana Kropp anatarajia 80% ya makampuni yatafanya hivyo.
Na tathmini ya nguvu kazi itakuwa itakuwa ni sekta yenye thamani ya $1.87bn ifikapo mwaka 2025, inasema taasisi ya tathmnini ya utafiti ya San Francisco.
Je ni makampuni yanakuwa makini kiasi hiki?
Ben Waber, Mkurugenzi mkuu wa Humanyze, kampuni ya Boston ya tathmini ya nguvu kazi , anasema udukuzi huu unayapa makampuni uwezo wa kutathmini namna wafanyakazi wao wanavyofanya kazi na kmahusiano yao , jambo ambalo linaweza kuw zuri kwa kampuni lakini si kwa waajiriwa wenyewe.

Chanzo cha picha, Robin Lubbock
Kampuni yake hukusanya "data" zilizoachwa na waajiriwakwenye barua pepe, na programu ya kutuma ujumbe wa hapo kwa hapo na kutumia kifaa cha majina chenye mitambo yenye uwezo wa kutambua utambulisho na sauti za vipaza sauti.
Vifaa hivi vinaweza kutambua ni kwa muda gani umeutumia katika mazungumzo, kiwango cha sauti yako, na kauli yako ilikuwa na ujumbe gani , hata kama utatawala mazungumzo. Wakati hii inawez kuonekana kama kuingilia nafsi ya mtu -si wote wanadhani hivyo- wanaounga mkono matumizi ya njia hizi wanadai mbinu hizi zinaweza kumlinda muajiriwa unyanyasaji wa kingono na vitisho
Baadhi ya tathmini ya data hizi inaweza kutoa matokeo ambayo hayakutarajiwa, anasema Bwana Waber. Kwa mfano, mteja mkubwa wa teknolojia hii aligundua kuwa watu 12 waliokuwa wanakaa katika meza za chakula walikuwa wakifanya kazi zaidi ya wale waliokuwa wakikaa kwenye meza za watu wanne.
Kadri watu wetu wengi walivyokuwa wakikaa kwenye meza iliongeza mazungungumzo na wafanyakazi kutoka kampuni nyingine, anasema na hii iliongeza wazo la ushirikishi.
Meza kubwa ziliweza "kufanya kazi kwa kiwango cha zaidi ya 10% ya utendaji". Jambo ambalo huenda lisingebainika bila tathmini ya data za aina hiyo.
Kwa miaka michache iliyopita mtandao wa kazi shirikishi wa Stockholm unaofahamika kama Epicenter ulifikia kiwango cha juu cha udukuzi huo na kufanya kinachoitwa "chipping parties", ambapo watu wanaweza kuwa na vifaa vyenye ukubwa wa mchele vinavyopandikizwa kwenye mikono yao, ili kutambua zaidi data zao .
Wanaweza kutumia vifaa hivyo vilivyopandikizwa na kuweza kufungua na kufunga milango inayodhibitiwa kielekroniki, kupata anwani za makazi au kuchunguza namna kasi ya kupiga chapa inavyoshabiahiana na viwango vya mapigo ya moyo ,anasema mmiliki wa Epicenter Hannes Sjöblad, ambaye binafsi anaishi na kifaa hicho kilichopandikizwa mikononi mwake.
Kifaa kinachopandikizwa "hakiwezi kuhamisha data mpaka uweke kipimo cha entimetre kinachosoma data , kwa hiyo mtu mwenye kifaa kilichopandikizwa ana uwezo wa kudhibiti ni lini kinaweza kutoa data/ taarifa zilizonaswa ", anasema.
Vifaa vinavyowekwa kwenye mwili huenda vikaonekana kuwa ni jambo lisilo la kawaida, lakini ni hatua moja ya teknolojia ya vitambulisho vya kielekroniki, anasema profesa Prof Jeffrey Stanton, mtafiti wa Chuo kikuu wa masuala ya msongo wa mawazo unaotokana na kazi.
Kama mpango huo ni wa kujitolea, "kuna uwezekano wa kuongezeka kwa kiwango cha matumizi yake kiasi kwamba idadi kubwa ya wafanyakazi wangependelea kuchagua kupandikiza kifaa hicho ", anaamini.
Lakini kama vifaa hivyo vinatumiwa kupunguza muda mapumziko ya wafanyakazi , "huenda tuko mahala pabaya'', anasema . Na kama vifaa vya uchunguzi wa data "vinachukua nafasi ya mazungumzo ya mfanyakazi kujiongoza ", hapo ndipo havipendwi.

Chanzo cha picha, Gartner
Mengi yanategemea ni kwa namna gani uchunguzi huu ulivyoelezwa kwa wafanyakazi , Gartner's Mr Kropp anadai.
Mwaka 2016, gazeti la Uingereza la Telegraph liliweka kifaa kinachochunguza joto na matembezi ya wafanyakazi wake chini ya madawati yao . Huku utawala ulisema kifaa hicho kililenga kuchunguza kwa ajili ya maswala ya utawala , wafanyakazi walifikiri kuwa walikuwa wanapelelezwa na wakapinga.
Kifaa hicho kiliondolewa katika kipindi cha saa 24.
Kama mabosi hawatawasiliana ipasavyo, wafanyakazi wanafikiria mabaya zaidi anasema kropp says. lakini wakiwa wazi na taarifa wanazozikusanya - na ni nini wanachokwenda kufanyia taarifa hizo - 46% ya waajiriwa "kwa ujumla wanakubali kuwekea kifaa kama hicho".
Ingawa mingi kati ya mifumo ya uchunguzi hutumia data ambazo hazina utambulisho na wanaoshirikishwa huwa hawalazimishwi ,wafanyakazi wengi huwa hawana imani na huwa na hofu na mifumo hii kwamba inaweza kuwanyima uhuru wao kamili . katika nchi ambazohakuna uhuru wa kutosha , wafanyakazi hawana usemi wowote,
lakini kwa baadhi faida ni dhahiri unapotumia vifaa vya kuwachunguza wafanyakazi

Chanzo cha picha, Jessica Johnson
"Nina tatizo la kiafya inaloitwa narcolepsy," la kulala kila ninapokuwa katika mazingira tulivu, anaeleza Jessica Johnson, mwenye umri wa miaka 34, kutoka Canberra, nchini Australia.
Hulala kwa vipindi vifupiwakati wa mchana, halafu anakosa mwelekeo anapoamka.
Hii "inaathiri kumbukumbu yangu, uwezo wangu wa kumakinika na kuwa na malengo ," anasema.
Anafanya kazi katika kampuni ya ambako wafanyakazi hutumia programu inayochunguza saa za kazi . Anasema ilimsaidia kubaini haraka kile alichokuwa akikifanya kabla ya kulala na kuendelea na kazi pale alipoachia.
"Unaiweka programu hiyo kwenye simu yako, halafu kwenye kompyuta na hivyo ndivyo unavyopata data zote ," anasema Mathias Mikkelsen, Mkurugenzi mkuu mtendaji wa programu ya Timely nchini Norway
Kwa hiyo uchunguzi wa maeneo ya kazi unaweza kuwa ni wa kuongezea uwezo wafanyakazi na muhimu kwa kampuni inayotaka kuzalisha faida zaidi na kutekeleza majukumu yake zaidi.
Lakini ukitekelezwa kwa njia isiyo sahihi, unaweza kuwa ni nyenzo ya kuchukiwa na kusababisha wafanyakazi kutofanya kazi kama ilivyotarajiwa.













