London Marathon 2019: Eliud Kipchoge ashinda London Marathon mara ya nne mfulululizo

Chanzo cha picha, PA
Mkenya Eliud Kipchoge ameshinda London Marathon kwa mara ya nne mfululizo.
Kipchoge, 34, ambaye alivunja rekodi ya dunia ya mbio hizo mjini Berlin mwaka jana, alikamilisha mbio za leo kwa muda wa saa mbili dakika mbili na sekunde thalathini na nane (2: 02: 38.)
Waethiopia Mosinet Geremew na Mule Wasihun walimaliza katika nafasi ya pili na ya tatu nyuma ya Kipchoge, ambaye alikosa kuvunja rekodi yake mwenyewe ya Dunia kwa sekunde 59 ambayo ilikua 2:01:39.
Muingereza Mo Farah alichukua nafasi ya tano baada ya kumaliza dakika 3 na sekunde moja nyuma ya Kipchoge, huku Muingereza Callum Hawkins akimaliza katika nafasi ya 10.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mkenya mwingine Brigid Kosgei, 25, alishinda mbio hizo upande wa kinadada na kuwa mwanamke wa kwanza wa umri mdogo kushinda London marathon upande wa wanawake.
Kosgei alimshinda bingwa mtetezi Vivian Cheruiyot kwa kutumia mda wa saa 2:18:20 kushinda mbio hizo kwa mara ya kwanza.
Mkenya Vivian Cheruiyot alichukua nafasi ya pili huku Roza Dereje wa Ethiopia akimaliza wa tatu.
Muingereza Charlotte Purdue alimaliza nafasi ya 10.

Chanzo cha picha, Reuters
Maelfu ya watu waMEshiriki makala ya 39 ya mbio za London Marathon 2019.
Mbio hizo zimechangisha £1bn tangu zilipoanzishwa mwaka 1981, kwa mujibu wa wadhamini Virgin Money.
Mshirikishi wa mbio hizo Hugh Brasher amesema : "Hakuna mbio zingine zinazokaribia London Marathon kwa uchangishaji wa fedha.''

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, AFP

Chanzo cha picha, PA
Kipchoge, Hajawahi kushindwa katika umbali wa zaidi ya maili 26.2 tangu mwaka 2013 katika mashindano ya Berlin Marathon.
Mshindi mara nane David Weir ameshiriki mbio hizo katika kitengo cha kutumia kiti cha magurudumu kwa mwaka wa 20 mfulululizo.

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters
Ukweli kuhusu mbio za London Marathon
- Watu 444,168 wamejiandikisha kuchangia mbio za mwaka huu idadi ambayo ni zaidi 7.3% ikilinganishwa na mwaka jana.
- 44% ya watu waliyotoa maombi ya kishiriki mbio hizo ni wanawake na nusu ya wakimbiaji hawajawahi kushiriki mbio za marathon.
- Waandaaji wa mbio hizo mwaka huu wanalenga kukusanya jumla ya pauni milioni 3.5
- Kundi la wanaume linalojiita ''Ever Presents'' limekua likishiriki mbio hizo tangu mwaka 1981














