Wataalamu wavumbua teknolojia mpya ya kudhibiti mlipuko wa magonjwa

Vimelea

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu masikini wanaoishi katika mazingira ya uchafu wanakabiliwa na hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza ambayo yanaimarika katika mazingira hayo.

Magonjwa kama vile ukambi na kifua kikuu ambayo yalikaribia kutokomwezwa mwongo mmoja uliyopita yameanza kuongezeka tena.

Maradhi ambayo yanaweza kutibiwa kama mafua na kuharisha yamesababisha vifo vya maelfu ya watu kila mwaka.

Kubuniwa kwa teknolojia mpya ya matibabu ambayo inauwezo wa kudhibiti mlipuko wa magonjwa hasa maeneo ya vijijini huenda ndio suluhisho la kukabiliana na magonjwa hayo.

Kuanzia jinsi chanjo zinavyopeanwa hadi mfumo unaotumiwa kuhakikishi inawafikia wahusika ni sehemu ya hatua zilizopigwa katika sekta ya matibabu.

Kushuka kwa viwango vya maambukizi miongoni mwa wagonjwa kumesaidiwa na juhudi zilizofikiwa katika harakati za kudhibiti magonjwa duniani.

Kuongezeka kwa matumizi ya antibiotiki inamaana kwamba baadhi ya bakteria imekuwa sugu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuongezeka kwa matumizi ya antibiotiki inamaana kwamba baadhi ya bakteria imekuwa sugu

Insulin ya tembe

Kuna aina nyingine za dawa ambazo sharti zipeanwe kupitia sindano.

Kudungwa sindano kila wakati kunanamuacha mgonjwa na maumivu makali.

Ikizingatiwa kuwa maeneo mengine yanakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kuhifadi sindano hizo kuna hofu ya hali hiyo huenda ikasababisha maambukizi ya magonjwa.

Watafiti kutoka chuo cha MIT Koch kinachohusika na uchunguzi wa saratani na hospitali ya wanawake Brigham inayomilikiwa na Harvard wamevumbua dawa ya tembea ya kisukari ambayo wanadai inaweza kutumika badala ya sindano.

Wagonjwa waliyo na aina ya kwanza ya kisukari huenda wakanufaika na dawa hiyo ambayo imetajwa kuwa imara katika udhibiti wa viwango vya sukari mwilini.

Dawa ya kuua viini hatari vya magonjwa vinavyofahamika kama 'superbugs'

Karibu 10% ya wagonjwa hupatwa na magonjwa mapya wakiwa wamelazwa hospitali - hasa baada ya kutumia vyombo vichafu au kuwa katika mazingira machafu.

Mtu akijidunga sindano

Chanzo cha picha, Getty Images

Hali hiyo husababisha vifo vya karibu watu 100,000 kila mwaka nchini Mraekani pekee.

Duniani watu 700,000 hufariki kila mwaka kutokana na maambukizi ambayo yamekuwa suugu kwa dawa, ikiwa ni pamoja na kifua kikuu, HIV na malaria.

Shirika la afya duniana hivi karibuni ilitaja usugu wa dawa aina ya antibiotiki kuwa "janga la kumatibabu" linalostahili kushughulikiwa kwa haraka.

BRCK: Huduma ya bure ya Wifi kwa umma

Mara nyingi watu hupuuza umuhimu wa kuwa na intaneti, lakini huduma hiyo imeibuka kuwa suluhisho kwa kwa masuala ya afya.

Ukosefu wa mawasiliano ya kidijitali wakati kunapotokea mlipuko wa ugonjwa huenda ukawa na madhara mabaya kwa wahudumu wa afya.

Wanaweza kukosea kiwango cha dawa ambacho mgonjwa anastahili kutumia , kupoteza rekodi zao, kushindwa kufanya maamuzi , makosa ya kitaalamu na kukosa kabisa maelezo kuhusu mlipuko wa ugonjwa.

Barani Afrika ambako zaidi ya watu bilioni 1.1 billion wanategemea simu zao za mkononi kupata huduma za interneti kuna tatizo la kuunganishwa na huduma hiyo muhimu.

Ukosefu wa interneti huenda ukaathiri sekta ya afya kwa umma katika mataifa yanayoendelea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ukosefu wa interneti huenda ukaathiri sekta ya afya kwa umma katika mataifa yanayoendelea

Tatizo hilo linachangiwa na baadhi ya watumiaji wa mtandao ambao wanajaribu kufikia taarifa zilizo mbali nao kwa mfano nchini Marekani na Ulaya.

Enter Moja, huduma ya bure ya Wifi iliyobuniwa na kundi la BRCK inatumika katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba wa interneti.

Mtandao wa Moja hawaunganisha watumiaji wake na Facebook, Netflix na Youtube, katika hatua ambayo inaweza kusaidia kusambaa kwa magonjwa.

Watumiaji wa mtandao huo wanewaza kupeana taarifa kuhusiana na magonjwa kwa muda unaofaa.

Waimamizi wa huduma hiyo wanasema kuna haja ya kuimarisha mawasiliano kati ya madaktari, wagonjwa, hospitali na wahudumu wa afya.