Hali ya usalama mdogo na ukuaji wa kiuchumi unaelezwa kuwa wa kasi isiyoridhisha ni vikwazo kwa Nigeria

nigeria

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Buhari aliahidi kushugulikia matatizo ya wanageria kama watamchagua tena
Muda wa kusoma: Dakika 2

Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari amechaguliwa kwa muhula mwingine wa miaka minne baada ya masaa kadhaa ya kuhesabiwa kwa kura.

Ameshinda kwa kura millioni 15 akiwa zaid kwa kura millioni 4 zaidi ya mpinzani wake Atiku aboubakar .

Upinzani wamekataa matokeo hayo.

Buhari mwenye umri wa miaka 76 amemshida mpinzani wake mkuu na aliyekua makamu wa rais bwana Atiku Aboubakar.

Changamoto anazokabiliana nazo.

Rushwa: Rushwa kwa kiasi kikubwa, imeshamiri nchini Nigeria, inaathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya jamii kiasi cha kwamba ni lazima suala hili litazamwe kwa jicho la tatu, nguvu ambayo wakosoaji wanasema ilikosekana katika utawala wa Rais Buhari katika awamu ya kwanza ya utawala wake.

Changamoto nyingine anazokabiliwa nazo katika kupambana na rushwa ni kuwa na uungwaji mkono kisiasa.Bila shaka anaungwa mkono na watu lakini Chama cha Buhari kina viongozi wakubwa ambao wanashukiwa kujinufaisha wenyewe kwa kujilimbikizia mali zilizopatikana kwa njia ya rushwa. Hofu ni kwamba kundi hilo la watu litaendelea na unyang'anyi huu kama kawaida.

Kiuchumi:suala la kuondoa utegemezi kutoka kwenye mapato yatokanayo na mafuta linapaswa kufanyika kwa haraka sana.Benki ya dunia ilikisia uchumi ukipanda kwa asilimia ndogo ya 2.2% kwa mwaka ujao huku kukiwa na ukosefu wa ajira kwa zaidi ya 20% .Vijana wengi wenye umri wa kufanya kazi hawana ajira na karibu nusu ya watu nchini humo wanaishi katika hali ya umasikini mkubwa.

Usalama mdogo:Rais Muhammadu Buhari anakabiliwa na vitisho vya kiusalama kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji,usalama mdogo katika katika eneo linalozalishwa mafuta la Niger Delta lakini kubwa zaidi ni vitisho kutoka makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali katika maeneo ya Kaskazini mwa Nigeria.

Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika inachangamoto pia za ukosefu wa umeme pia.

Chama cha Buhari kimeshinda majimbo 19 kati ya 36 , wakati chama cha upinzani cha PDP wakishinda majimbo 17.

Asilimia 35 tuu ya wapiga kura walijitokeza , baadhi wafuasi wa Buhari tayari wameingia mtaani kushangilia.

nigeria

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, wafuasi wa Buhari wakishangilia huko Kano

''Kama kijana wa Nigeria naamini kuwa huu ni mwanzo mpya kwa nchi yetu, ndo mana tumeamua kumrudisha kwa muhula mwingine'' anasema mfuasi wa Buhari

''Nafurahi sana , ni kitu ambacho tuliona kinatokea kuhusu Rais, na ukizungumzia suala la kupambana na rushwa kumesaidia sana, tunajivunia.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekuwa kiongozi wa kwanza barani Afrika kumpa hongera rais Buhari kwa ushindi wake:

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Buhari alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 akiwa ni kiongozi wa kwanza wa upinzani kukalia kiti cha urais,

Wakosoaji wake wanasema kuwa amekua akijitetea kusimamia vita ya rushwa na suala la Boko Haram, lakini kwa upande wa uchumi bado kumedorora.

Tume ya uchaguzi imesema kuwa itaangalia malalamiko yote kabla ya kutangaza Rasmi matokeo ya uchaguzi.