Pasipoti zilianza kutumika baada ya vita vikuu vya kwanza vya dunia

Paspoti ni stakabadhi muhimu inayomuwezesha mtu kuzuru sehemu tofauti duniani

Chanzo cha picha, Getty Images

Pasipoti ni stakabadhi muhimu ambayo humfungulia mtu milango ya kusafiri sehemu tofauti duniani, lakini kwa wengine inadhibiti utangamano wa watu kimataifa.

Lakini ni mara ngapi ushawahi kujipata ukiangalia uhalisia wa paspiti yako kusafiri?

Kuna historia ya kipekee iliyochangia kubuniwa kwa stakabdhi hii muhimu ya usafiri ambayo itakufanya ubadili mtazamo wako kuhusiana na masharti unayotakiwa kutimiza kabla ya kuomba pasipoti .

1. Pasipoti ya Scandinavia inatoa mwangaza maalum ikipitishwa chini ya miale jua

Mwanga kwenye pasipoti ya Scandnavia

Chanzo cha picha, Getty Images

Ukiweka pasipoti ya Scandinavia chini ya mwanga wa jua itatoa laini iliyo na mwangaza kwenye karatasi zake.

2. Pasipoti ya kwanza imetajwa kwenye Biblia

Kurasa za kitabu zilizochanika

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika kitabu cha Nehemia, Mfalme Artaxerxes wa kwanza wa Uajemi alimpatia afisa mmoja ruhusa ya kusafiri kupitia Judea.

3. Paspoti zilianza kutumika baada ya vita vikuu vya kwanza vya dunia

Picha ya paspoti

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha ya paspoti

Picha zilianza kuwatumika kama sehemu ya masharti ya kuomba passporti mwanzoni mwa vita vikuu vya kwanza vya Dunia - baada ya majasusi wa Ujerumani kuingia Uingereza kwa kutumia pasipoti gushi ya Marekani.

4. Umepunguza uzani? Chukua pasipoti mpya

Jihifadhie picha zako mwenye haziwezi kutumika kwa pasipoti

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jihifadhie picha zako mwenye haziwezi kutumika kwa pasipoti

Nchini Marekani unahitajika kubadilisha picha yako ya pasipoti ukinenepa au kupunguza uzani ama kama umefanyiwa upasuaji kwenye uso au kuchora tattoo.

5. Picha za familia zilikuwa zinatumika katika pasipoti

Ulihitaji kuchagua picha yako nzuri

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ulihitaji kuchagua picha yako nzuri

Zamani watu waliruhusiwa kutuma picha ambazo wangelipenda iwekwe kwenye paspoti zao.

Hata picha za familia zilikubalika

6. Toa maombi ya pasipoti nyingine miezi sita kabla muda wake kuisha

Ukurasa wa paspoti

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ukurasa wa paspoti uliyopigwa muhuri

Usifanye mzaha na tarehe ya mwisho ya pasipoti yako kabla ya kupanga safari.

Nchi zingine zina masharti ya kutaka pasipoti yako kuwa sahihi kwa siku 90 baada ya kuingia - ikiwa ni pamoja na nchi nyingi za Ulaya.

Ni vyema kuwasilisha maombi ya pasipoti mpya miezi sita kabla ya tarehe ya mwisho, huo ndio muda inaotakikana nchini China, Indonesia, Urusi, Saudi Arabia na mataifa mengine.

Hatua hiyo itakuepushia madhila ya kukwama katika nchi ya kigeni kwa kukosa namna ya kurudi nyumbani.

7. Hauhitaji kuwa na pasipoti kuingia Australia kupitia Queensland…

Huu ni uhusiano maalumu?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Huu ni uhusiano maalumu?

Ikiwa wewe ni mkaazi wa moja ya vijiji 9 katika pwani ya Papua New Guinea, huhitaji kuwa na passpoti ya kuingia Australia kupitia Queensland.

Papua New Guinea ilipopata madaraka ilitia saini na makubaliano maalumu inayowawezesha watu wa Queensland kutembelea visiwa hivyo bila kuwa na paspoti

8. Vatican hana udhibiti wa uhamiaji

Unadhani ni nani wa kwanza kuwa na pasipoti katika mji wa Vatican...

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Unadhani ni nani wa kwanza kuwa na pasipoti katika mji wa Vatican...

Vatican haina udhibiti wowote wa uhamiaji - lakini Papa hubeba Pasipoti ya Vatican No. 1

9. Wamarekani wengi hawana pasipoti

Pasipoti ya Marekani na tiketi ya ndege

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pasipoti ya Marekani na tiketi ya ndege

Kwa mujibu wa idara ya mambo ya ndani ya Marekani, kuna karibu pasipoti 121,512,341 na pasipoti 321,362,789 ni za raia wa Marekani.

10. Tonga walikua wakiuza pasipoti zao

Pasipoti ya Tonga

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pasipoti ya Tonga

Tonga ilikua ikiuza pasipoti yake kwa dola 20,000 kila moja.

Marehemu Mfalme Taufa'ahau Tupou wa IV wa jimbo huru la Polynesia aliripotiwa kuuza pasipoti ya Tonga ili kukusanya mapato ya nchi.

11. Pasipoti za Finland na Slovenia zilikuwa zikitumia vitabu kama flicker vilivyo na picha aina tofauti

Pasipoti zilizokua zikitumia vitabu kama flicker

Chanzo cha picha, Getty Images

Wamiliki wa pasi hizo walikua wakiangalia picha hizo ili kupitisha muda katika uwanja wa ndege wakati wakisubi kuanza safari zao.

Ukisongeza mbele kurasa za pasipoti, picha za chini ya ukurasa inaanza kutengeneza picha inayopita moja baada ya nchingine.

12. Pasipoti ya Nicaragua ndio ngumu zaidi kuighushi

Pasipoti mbili za Nicaragua juu ya meza

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pasipoti mbili za Nicaragua juu ya meza

Pasipoti ya Nicaragua ina vipengele 89 tofauti vya usalama tofauti

Kutokana na hilo inatajwa kuwa passipoti hiyo inatajwa kuwa ngumu sana kuighushi.

13. Malkia wa Uingereza hana pasipoti

Malikia Elizabeth II akiwa ndani ya boti Malta

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malikia Elizabeth II akiwa ndani ya boti Malta

Malkia Elizabeth II huwa hana haja ya kuwa na pasipoti kwa sababu ndiye huwa anatoa idhini kwa watu wake wote kuwa na stakabadhi hiyo muhimu ya usafiri duniani

Hata hivyo ana pasipoti ya stakabadhi zake nyingine za siri.

Watumishi wa Malkia ndio wanaosimamia stakabadhi hizo za siri na kila moja ina pasipoti yake.

Inadaiwa kuwa kuna pasipoti 15 pekee za aina hiyo ambazo zinatumika.