Takwimu ligi kuu England: Ryan Sessegnon na chipukizi wanaojikita na kung'aa

Chanzo cha picha, Getty Images
Iwapo una zaidi ya miaka 25 basi huenda ukajihisi mkongwe...
Watoto waliozaliwa milenia hii wanaonekana kujikita na kudhihirisha umuhimu wao katika ligii kuu England.
BBC Sport imetathmini takwimu muhimu kutoka kwa timu kuu wikendi hii.
Watoto wa Milenia wamewasili
Y2K - Manjonjo kama alivyosema msanii wa taarab ya Rusha Roho Khadija Kopa Tanzania - kirusi cha kompyuta kilichotabiriwa kusababisha ghasia ( Hakikufanikiwa) wasanii wa hip hop kama Britney Spears
na kadhalika yote haya yanakumbusha kuingia kwa milenia mpya. Lakini hiyo ni kama wewe u mzee kutosha kuyafahamu au kuyakumbuka haya.
Mchezaji wa Fulham mwenye miaka 18 Ryan Sessegnon hakumbuki. Kwasababu alizaliwa 2000.

Chanzo cha picha, Reuters
Mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka -21 ya England aliteleza na kufunga bao la pili wikendi hii dhidi ya Cardiff . Licha ya kwamba bao hilo halikuwa na uzito vile maana mwisho mechi ilimalizika kwa Fulham kufungwa 4-2, alifanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa mwaka 2000 kuwahi kufunga katika timu kuu ya England.
Sessegnon ni mojawapo ya wachezaji wanane waliozaliwa katika milenia hii kuwahi kucheza katika ligi kuu ya England.
Na mchezaji huyo asiyekosekana katika mechi za Fulham msimu huu ina maanisha hakuna mchezaji mwingine aliyezaliwa 2000 amewahi kucheza zaidi katika ligi kuu ya England kama yeye...

Hatahivyo, Sessegnon na Foden bado wako mbali na mchezaji mwingine chipukizi wa England ambaye ameweka historia ya milenia.
Jadon Sancho amekuwa mchezaji wa kwanza wa kimataifa aliyezaliwa katika miaka ya 2000 alipocheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Croatia wiki iliyopita.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji huyo mwenye miaka 18 alitoka Manchester City kujiunga na Borussia Dortmund mwaka jana na anapata faida kwa kujumuishwa katika kikosi cha kwanza katika ligi ya Ujerumani Bundesliga.
Sancho ameichezea timu hiyo kuu ya Ujerumani mara 20, inayomaanisha ni mchezaji mmoja pekee aliyezaliwa milenia hii - mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Moise Kean, aliyekuwa kwenye mkopo huko Verona msimu uliopita - aliye na uzoefu mkubwa katika ligi tano kubwa za Ulaya.

Sessegnon aliibuka kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi wa Fulham alliyeifungia timu hiyo katika Primia Ligi akiwa na miaka 18 na siku 154 .
Lakini bado hajafuzu kuwa katika orodha ya wafungaji 10 bora walio wadogo katika historia ya mashindano hayo.














