Thierry Henry asema anamuiga Pep Guardiola katika kazi yake mpya ya ukufunzi klabu ya Monaco

Chanzo cha picha, Thierry Henry asema anamuiga Pep Guardiola katika
Mkufunzi mpya wa klabu ya Monaco Thierry Henry anasema kuwa mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola atakuwa na ushawishi muhimu wakati anapoanza kazi ya ukufunzi.
Henry ambaye alianza kazi ya kusakata soka ya kulipwa katika klabu ya Monaco amerudi baada ya klabu hiyo kumfuta aliyekuwa mkufunzi wake Leonardo Jardim.
Anasema kuwa alijifunza kucheza soka chini ya Guardiola wakati akiichezea Barcelona muongo mmoja uliopita.
''Pep ndio mshawishi wangu mkubwa'' , Henri mwenye umri wa miaka 41 alisema .Uvumbuzi aliokuwa nao katika mchezo yuko mbele ya kandanda.
Raia huyo wa Ufaransa ametia saini mkataba hadi Juni 2021 na amewacha kazi yake kama naibu wa mkufunzi katika timu ya taifa ya Ubelgiji.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal aliisaidia Monaco kushinda taji la daraja la kwanza 1997 na anachukua timu hiyo ikiwa ya tatu kutoka chini katika ligi kuuu ya Ufaransa msimu huu.
Mechi ya kwanza ya Henry akisimamia timu hiyo itakuwa dhidi ya Strasbourg katika ligi tarehe 20 Oktoba , kabla ya mechi ya vilabu bingwa dhidi ya Club Brugge siku nne baadaye.
''Hakuna la sawa ama makosa, kwangu mimi'', alisema kuhusu lengo lake la kumuiga Guardiola na vile anavyochukulia kandanda.
''Nilijifunza upya jinsi ya kucheza soka wakati nilipokwenda Barcelona chini yake. Ukiwa na Pep unaweza kuzungumza kuhusu soka, hatakwenda kulala utajikuta ukilala na yeye anazungumza kuhusu kandanda. Unajifuza kutoka kwa watu wanaokupatia msukumo. lakini pia wewe unahitaji kutia bidii yako''.

Chanzo cha picha, Getty Images
Alipoulizwa kuhusu aliyekuwa kocha wa Arsenal Arsene wenger, ambapo anadaiwa kucheza kipindi kirefu cha soka yake akiwa Arsenal kutoka 1999 hadi 2007.
Henry alisema: Arsene alizindua vitu vingi akilini mwangu , na kunifanya nielewe ni nini kuwa mchezaji wa kulipwa na jinsi ya kucheza vyema. Sitasahau hilo. Munajua uhusiano niliokuwa nao naye hivyobasi nitatumia baadhi ya mambo ambayo alikuwa akifanya.
Henry ambaye aliichezea Juventus na klabu ya New York Red Bulls , anachukua hatua yake ya kwanza katika usimamizi baada ya kipindi kirefu cha uchezaji soka ambapo kilishirikisha ushindi wa kombe la dunia na Ufaransa 1998 na kombe la bara Ulaya miaka miwili baadaye.
Mshambuliaji huyo wa zamani alifunga magoli 51 katika mechi 123 akiichezea Les Blues kabla ya kustaafu akiwa mchezaji mnamo mwezi Disemba 2014 ili kufanya kazi kama mchanganuzi wa soka katika runiunga kabla ya kujiunga na ukufunzi wa timu ya Ubelgiji 2016.













