Ballon d'Or: Je ni yupi mchezaji wa tatu bora zaidi duniani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Tuzo ya Ballon d'Or - ambayo ni muhimu zaidi katika soka ya wanaume duniani itatolewa mjini Paris mwanzoni mwa mwezi Disemba.
Hatahivyo mwaka huu kuna fursa ya kwanza tangu 2007 ambapo atakayepokea tuzo hiyo hatokuwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi wala mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo.
Mchezaji mwenza wa zamani wa Ronaldo katika klabu ya Real Madrid Luka Modric alitangazwa kuwa mchezaji bora wa tuzo za Fifa mnamo mwezi Septemba na mwaniaji wa tuzo hiyo huku mshambuliaji wa Real raia wa taifa la Wales Gareth Bale na mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane wakiwa miongoni mwa wagombea 30 wa tuzo ya mwaka huu.
Hivyobasi iwapo tunachukulia kwamba Messi na Ronaldo ndio wababe basi ni mchezaji gani wa tatu aliyebora zaidi duniani?
Tuliwauliza baadhi ya wachanganuzi wa soka wa BBC kuhusu mawazo yao na tukaangalia takwimu ili kujaribu kuelewa.
'Wameonyesha kiwango cha mchezo mzuri msimu wote.
Aliyekuwa nahodha wa Uholanzi Ruud Gullit amemchagua mshambuliaji wa Paris St-Germain na mshambuliaji wa Brazil Neymar

"Huu ni uamuzi mgumu kwa kuwa wagombea wanakaribiana. Kevin de Bruyne alionyesha mchezo mzuri akiichezea Manchester City msimu uliopita , lakini kiwango cha muda wa mwaka mmoja ni kifupi kumpima mchezaji, uwezo wake ndio unaohitajika.
Eden Hazard amekuwa katika kiwango hicho kwa misimu michache na hivyobasi sasa yupo juu-lakini Neymar amekuwa mzuri sana katika misimu kadhaa kufikia sasa akifunga mabao mengi.
Neymar hakuwa na kipindi kizuri cha kombe la dunia lakini alikuwa amejeruhiwa na kujaribu kucheza hivyohivyo swala ambalo sio rahisi.
Sasa kiwango chake kimeimarika tena akiwa na PSG na huwezi kusahau vitu vizuri alivyofanya akiichezea Barcelona.
Je wajua kwamba Neymar amekosa mechi nyingi akiichezea PSG mwaka 2018 akicheza mechi 21 pekee.
Klabu hiyo imeshinda mechi 19 kati ya 21 alizoshiriki lakini kati ya mechi 14 amekosa kushiriki.
'Alionyesha mchezo mzuri mwezi Agosti na Septemba, huku akiimarika zaidi mwezi Oktoba'
Nahodha wa zamani wa Uingereza Alan Shearer amemchagua mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard

"Kylian Mbappe alikuwa na kipindi kizuri katika kombe la dunia akiichezea Ufaransa nchini Urusi na atakuwa katika orodha ya tano bora, lakini ni Eden wakati huu kutokana na alivyoanza msimu wake na kuendeleza kiwango chake kizuri cha mchezo kutoka Urusi.
"Hazard alikuwa akicheza vizuri katika klabu ya Chelsea mnamo mwezi Agosti na Septemba na wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba alizidi kuimarika. Matumaini ya Chelsea kuweza kushinda taji la ligi yanamtegemea yeye''
'Anaweza kuendesha mchezo'
Beki wa zamani wa Liverpool Mark Lawrenson amemchagua kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Luka Modric

"Eden Hazard yupo miongoni mwa wachezaji bora zaidi pamoja na mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, lakini ninamchagua Luka Modric.
"Amekuwa na msimu mzuri akiichezea Real Madrid baada ya misimu mingine mizuri iliopita na alimalizia vizuri kwa kuiongoza Croatia hadi katika fainali za kombe la dunia.
Modric anaweza kusukuma mechi kutoka safu ya kati dhidi ya upinzani, lakini sio mchezaji anayeendesha mchezo pekee kwa kuwa pia anaweza kukupokonya mpira .
Je kumekuwa na kiungo wa kati bora zaidi barani Ulaya ama kokote kule katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita? kwa kweli hakuna ninamchagua yeye."
'Tayari amefanya mengi'
Mchezaji wa zamani wa Uingereza na Tottenham Jermaine Jenas anamchagua Neymar

"Luka Modric amekuwa na mwaka mzuri wa kumbukumbu na napenda kumuona Antoine Griezmann, ambaye anaonekana kuimarika zaidi na zaidi.
Kwa kiwango kizuri Eden Hazard amekuwa akionyesha mchezo mzuri zaidi.
"Lakini sitoangazia kiwango cha mchezo bali uwezo wa mchezaji , kile walichofanyia klabu kafikia kiwango cha kimataifa na pale nafikiria wanaelekea. Nitamchagua Neymar .
Katika klabu ya Paris St Germain anaonekana kucheza pekee kwasababu nadhani ligi ya daraja la kwanza ni rahisi sana kwake, lakini katika klabu ya Barcelona alikuwa imara zaidi akishirikiana na Lionel Messi na Luis Suarez.
Ana umri wa miaka 26 pekee lakini tayari ana magoli 30 ya ligi ya mabingwa Ulaya , goli moja nyuma ya Rivaldo ambaye anashikilia rekodi ya ufungaji mabao katika mashindano hayo, na tayari amefanya cha ziada katika ulingo wa kimataifa.
Najua kwamba Neymar hakuwa na kipindi kizuri cha kombe la dunia , lakini hio sio sababu.
'Ameleta tofauti kubwa'
Mshambuliaji wa zamani wa Celtic Chris Sutton alimchagua beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk
"Huenda sio vyema kumtaja beki wakati wa mjadala kama huu, lakini unapotazama tofauti alioleta Virgil van Dijk katika timu ya Liverpool basi ni hapo unapoweza kubaini umahiri wake.
hakuna kile kilicho na beki ambacho hana , ana kasi, ni thabiti, na haonekani kupoteza uwezo wake.
Pia ni mchezaji anayesambaza mipira kwa wingi anapokuwa na mpira na anaweza kusoma mchezo vizuri.
Ana uwezo mwingi sana.
Kutakuwa namitizamo tofauti kuhusu Eden hazard akilinganishwa na washambuliaji wengine- na naelewa hilo-lakini Van Dijk ameonyesha tofauti ambayo beki mzuri anaweza kuleta katika timu yoyote.
'Kwa sasa ni Hazard lakini Mbappe ndio mchezaji anayechipuka kwa kasi'.
Winga wa zamani wa Chelsea Pat Nevin anamchagua Eden Hazard ama mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe

"Je tunazungumzia kuhusu mchezaji bora wa tatu hivi sasa? ama mchezaji anayetarajiwa kumrithi Messi na Ronaldo? kwa sababu kuna jibu tofauti.
"Eden Hazard hakuwepo katika orodha ya wagombea msimu uliopita.
Iwapo ningeulizwa basi ningesema kuwa mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salah alikuwa bora zaidi na pia Kevin De Bryune akiwa katika klabu ya Manchester City alikuwa mzuri kama wagombea wengine.
Lakini iwapo tunazungumza kuhusu sasa , na kiwango cha msimu huu , basi Hazard anakaribia sana hata iwapo sio mchezaji bora wa tatu kwa sasa.
Kumpatia mtu jukumu hilo kwa kuwa alianza misimu vyema ni kwenda mbali sana.
Iwapo utaniuliza ni mchezaji gani bora anayetarajiwa kumrithi Messi na Ronaldo ambalo ni swali tofauti nitasema Kylian Mbappe.
Mbappe ndio mrithi wa Messi na Ronaldo-na ndiye anayepigiwa upatu kuwa mchezaji bora duniani-lakini sitosema kwamba yeye ni wa tatu kwa ubora kwa sasa ikilinganishwa na alivyofanya msimu huu.

"Kwa sasa Hazard anacheza vyema kama mchezaji mwengine yeyote yule lakini hilo ni la muda mfupi.












