Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 22.10.2018: Milenkovic, Mourinho, Benitez, Lopetegui, Foden, Martial

Mourinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mourinho

Fiorentina wamewaambia Manchester United kuwa mlinzi raia wa Serbia Nikola Milenkovic, 21, atagharimu pauni milioni 40 ikiwa ni milioni 10 zaidi na wana moyo wa kutumia pesa kwa mchezaji huyo wa miaka 21. (Sun)

Meneja Jose Mourinho anajaribu kuwashawishi maafisa wa Manchester United kufadhili mpango wa kumpata mlinzi bora zaidi ifikapo Januari. (Sunday Times)

Mourinho atafanya uchunguzi wa ndani kuhusu ni vipi orodha ya kikosi cha Manchester United ilifichuliwa kabla ya mechi ya Jumamosi iliyotoka sare na Chelsea. (Daily Mail)

Anaweza kupigwa marufuku ya kuvuka laini na makabiliano na kocha wa pili wa Chelsea Marco Ianni huko Stamford Bridge. (Daily Express)

Anthony Martial

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Anthony Martial

Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 22, amekana kuwa na uhusiano mbaya na meneja Jose Mourinho. (London Evening Standard)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez, ambaye kikosi chake kiko chini katika jedwali la Premier League, anakiri kuwa anaishiwa na muda huko St James' Park. (Daily Mirror)

Meneja wa Real Madrid Julen Lopetegui anaripotiwa kukaribia kutimuliwa huku meneja wa kikosi cha B Santiago Solari akiwa katika nafasi ya kuchukua mahala pake. (Talksport)

Julen Lopetegui

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Julen Lopetegui

Borussia Dortmund, waliomchukua mchezaji wa miaka 18 Jadon Sancho kwenda Bundesliga wanamtazama lkiungo wa kati wa Manchester City Phil Foden, 18, mshambuliajia wa Chelsea Hudson-Odoi, 17, na mshambuliaji wa miaka 17 wa Liverpool Bobby Duncan. (Daily Mirror)

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, ambaye amehusishwa na Liverpool na pia Juventus, anaripotiwa kukaribia kuongeza mkataba wake na klabu hiyo wa Ufaransa. (Calciomercato)

Meneja wa Leicester Claude Puel anasema hafikirii kumuita kiungo wa kati Harvey Barnes, 20, ambaye yuko kwenye mkopo huko West Brom. (Birmingham Mail)

Wayne Roone

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wayne Roone

Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney, 32, anasema alijua atafanikiwa huko Old Trafford. (NBC via Goal.com)

Tottenham huanda wakafungua duka lao jipya ambalo linatarajiwa kuwa duka kubwa la klabu barani Ulaya kwenye uwanja wao mpya siku ya Jumanne. (Football London)

Meneja wa zamani wa Newcastle Alan Pardew anasema meneja Rafael Benitez anakabiliwa na changamoto sawa na zilizomkumba alipokuwa meneja hiko Magpies. (Newcastle Chronicle)

Bora zaidi Kutoka Jumapili

Chelsea wanataka kumfanya Eden Hazard kuwa mchezaji anayelipwa kitita cha juu zaidi katika Ligi ya Premier kwa kumpa ofa ya mshahara wa dola 350.000 kwa wiki. (Express)

Eden Hazard

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Eden Hazard

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Prince Mohammed bin Salman anatarajiwa kukutana na wamiliki wa Manchester United familia ya Glazer wiki chache zinazokuja, kuwasilisha ofa ya dola bilioni 4 kuinunua klabu hiyo. (Mirror)

Manchester City wanakataa kubadilisha msimamo wao kuhusu masharti ya mkataba wake na Raheen Sterling, na kuongeza hofu kuwa mchezaji huyo wa miaka 23 wa England anaweza kuondoka msimu ujao. (Mirror)

Real Madrid wako tayari kumpa ofa Sterling mwezi Januari. (Express)

Raheen Sterling

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raheen Sterling

Manchester City wanatathmini ofa ya pauni milioni 40 kwa mchezaji wa Bournemouth Nathan Ake mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 wa Uholanzi pia amehusishwa na Manchester United na Tottenham. (Sun)

Tottenham wanapanga kumuendea kiungo wa kati wa Blackburn Bradley Dack, 24, kutokana na ripoti nzuri za majenti. (Express)

Meneja Manchester United Jose Mourinho anataka kumleta mlinzi wa Fiorentina Nikola Milenkovic. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Serbia anawekewa thamani ya dola milioni 40 na klabu ya Italia kwa kuwa wanajua anawindwa na United, Tottenham, Chelsea, Arsenal na Juventus. (Star)