India: Mahakama imesema sheria hiyo imekuwa ikiwakandamiza wanawake

Wapenzi Mumbai

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Chini ya sheria hiyo wanawake hawana makosa lakini mwanaume anaadhibiwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Mahakama ya juu zaidi nchini India, imeamua kuwa uzinzi sio kosa la uhalifu tena nchini humo katika hatua ambayo imefutilia mbali sheria ya kikoloni iliyodumu miaka 158.

Katika uamuzi wake mahakama hiyo imesema sheria hiyo imekuwa ikiwakandamiza wanawake na kuwafanya kana kwamba wao ni mali ya wanaume.

Kabla ya uamuzi huo mwanamume yeyote aliyeshiriki tendo la ndoa na mwanamke aliyeolewa bila idhini ya mume wake alikuwa ametenda kosa la uhalifu.

Mlalamishi aliyewasilisha kesi mahakamani, kupinga sheria hiyo alisema kuwa ni sheria ya kiholela na ambayo inawabagua wanaume na wanawake.

Haijabainika ni wanaume wangapi wameshitakiwa chini ya sheria hiyo kwa sababu hakuna taarifa zozote kuhusiana na suala hilo.

Hii ni sheria ya pili ya kikoloni kufutiliwa mbali na mahakama ya juu zaidi nchini India mwezi huu.

Akitoa hukumu hiyo, jaji mkuu, Dipak Misra,amesema japo sheria hiyo inaweza kutumiwa kutatua masuala ya kijamii kama vile kuachana kwa mume na mke lakini, "haiwezi kuwa kosa la uhalifu".

Ni nani aliyepinga sheria hiyo?

Mwezi Agosti, mfanyibiashara Joseph Shine, 41, anayeishi nchini Italia aliwasilisha kesi katika mahakama ya juu zaidi kuomba sheria hiyo ifutiliwe mbali.

Bwana Shine alihoji kuwa shiria hiyo ni ya kibaguzi dhidi ya wanaume na kwamba inawafanya wanawake waliyoolewa kuonekana kama chombo cha waume zao.

"Wanawake waliyoolewa hawafai kulengwa kisheria kwa sababu ya kufanya uzinzi,".

Ili kuongezea uzito kesi hiyo Shine, aidha amewanukuu mshairi wa Ralph Waldo Emerson, mzaliwa wa Marekani, mwanaharakati wa haki za wanawake Mary Wollstonecraft, aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan kuhusu suala la usawa wa kijinsia na haki za wanawake.

ndoa India

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Kesi zilizopita zilitupiliwa mbali na mahakama kwa maslahi ya ndoa

Chama tawala cha BJP nchini India, kilikiwa kimepinga kesi hiyo kikisisitiza kuwa suala la uzinzi linafaa kusalia kuwa kosa la kihalifu.

Baraza kuu la chama hico lilisema kuwa "Kupunguza makali ya sheria hiyo kutaathiri taasisi ya ndoa''.

Sheria ya Uzinzi India inasema nini?

Kwa mujibu wa sheria hiyo mwanamke anayefanya kosa la uzinzi hafai kuchukuliwa hatua kisheria lakini mwanamume anastahili kuadhibiwa kwa kumtongoza mwanamke.

Sheria hiyo pia haiwaruhusu wanawake kuwasilisha kesi dhidi ya waume zao wenye tabia ya uzinzi.

Mwanamume atakaepatikana na kosa la uzinzi huenda akafungwa jela hadi miaka mitano na kutozwa faini au vyote viwili.

Japo hakuna taarifa zozote kuhusiana na watu waliyohukumiwa chini ya sheria hiyo, wakili wa mlalamishi Kaleeswaram Raj, amesema sheria hiyo hutumiwa vibaya na wanaume dhidi ya wake zao.

Majaji wamesema nini?

Majaji wote watano waliyokua wakisikiliza kesi hiyo wamesema sheria hiyo ni ya kidhalimu na kwamba inakiuka katiba

Jaji mkuu Dipak Misra, amesema ''Wanawake na wanaume wanastahili kuwa na haki sawa na wanaume''.

Jaji Rohinton Nariman amesema ''Dhana potofu za zamani kwamba mwanamume ndiye mwenye makoso huku mwanamke akichukuliwa kama muathiriwa imepitwa na wakati''

Jaji DY Chandrachud amesema sheria hiyo inamdhalilisha mwanamke kutokana kwa kudunisha jinsia yake.

Wakosoaji wa sheria hiyo wanasema ina kiuka haki ya usawa katika jamii, ina wanyanyasa wanawake na kwamba imepitwa na wakati.

Jarida mashuhuri la kila wiki linaloangazia masuala ya kichumi na kisiasa nchini India, linahoji ikiwa ni sahihi kwa serikali kuingilia uhusiano wa kimapenzi wa watu wawili iwe wameoana ua la.

Ni wapi kwingine Uzinzi ni kosa la kihalifu ?

Uamuzi wa sasa umetolewa kwa kuzingatia mabadiliko katika jamii

Chanzo cha picha, Mansi Thapliyal

Maelezo ya picha, Uamuzi wa sasa umetolewa kwa kuzingatia mabadiliko katika jamii

Majimbo 21 nchini Marekani miongini mwao New York yameharamisha uzinzi na yanaichukulia na kosa la kihalifu japo wamarekani wengi wanapinga hatua hiyo.

Uzinzi pia hauruhusiwi katika sheria ya dini ya Kiislamu na nchi kama Iran, Saudi Arabia, Afghanistan Pakistan, Bangladesh na Somalia zina sheria kali dhidi ya suala hiyo.

Taiwan huwafunga jela mwaka mmoja watu wanaopatikana na kosa la uzinzi.

Nchini Indonesia Uzinzi ni kosa la kihalifu na taifa hilo linabuni sheria ambayo inaharamisha tendo la ndoa kati ya watu wawili ambao hawajaoana.

Mwaka 2015, Mahakama ya juu zaidi nchini Korea Kusini ilipinga sheria sawa na hiyo ambapo mtuangeweza kufungwa gerezani kwa miaka miwili au chini ya miaka miwili kwa ajili ya uzinzi.

Mahakama hiyo alisema sheria ilikiuka uamuzi wa kibinafsi na faragha.

Wakili wa mlalamishi, Kaleeswaram Raj pia amesema zaidi ya mataifa 60 duniani yamefutilia mbali sheria inayosema uzinzi ni kosa la uhalifu.

Wakosoaji wanasema sheria hiyo ni ya kibaguzi

Chanzo cha picha, Mansi Thapliyal

Maelezo ya picha, Wakosoaji wanasema sheria hiyo ni ya kibaguzi

Watu wanasema nini kuhusiana a uamuzi huu

Watu wengi nchini India hawakua na habari kuhusu uwepo wa sheria kama hiyo lakini wanaunga mkono uamuzi wa siku ya Alhamisi wa mahakama dhidi ya sheria hiyo .

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2

Mwisho wa X ujumbe, 2

Wengine wamesema mahakama hiyo ya juu inafaa sasa kuamua kwamba ubakaji katika ndoa pia ni kosa la uhalifu.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Lakini wengine walihisi kwamba sheria hiyo ilifaa kuangazia kusawazisha jinsia zote mbili.

Ruka X ujumbe, 4
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 4

Ruka X ujumbe, 5

Mwisho wa X ujumbe, 5