Unaitumia Google mara ngapi kwa siku? haya ni mambo ambayo huenda huyajui kuhusu kampuni hiyo

A bicycle rider on a Google bike zooms outside of one of the main buildings of search engine giant Google's sprawling campus in Mountain View, California

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vitu kumi ambavyo huenda hauvijui kuhusu Google

Unakumbuka maisha kabala ya Google? ulifanya nini wakati ulihitaji kutafuta taarifa fulani kwa haraka?

Chochote unachokitafuta liwe jina la kitu fulani au jinsi ya kuandika jina fulani au jina la eneo fulani bila shaka ni lazima utafute kwenye Google.

Kwa kukadiria Google hushughulikia karibu mambo 40,000 kwa sekunde moja, hiyo ni sawa na mambo bilioni 3.5 kwa siku.

Google sasa imegeuka kuwa sio eneo tu la kutafuta majina lakini pia sehemu muhimu kwa matangazo na mkusanyaji wa taarifa za watu.

Kila wakati unapofanya kitu fulani, Google inajua kuhusu tabia zetu. Lakini wewe unafahamu mambo yapi kuhusu Google?

Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kukushangaza.

1. Jina

Close up to Google website through a magnifying glass on the laptop.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuliandika vibaya jina kati ya marafiki

Google ni nini? kwa kweli neno Google halimaanisha chochote.

Lilitokana na kuandikwa vibaya kwa jina la 'googol'

Kuna madai kadhaa kuhusu labda vile mhandisi au mwanafunzi aliweza kuibuka na jina hilo.

Makosa hayo ya uandishi yalichangia kupatikana nene hilo, na mengine ni historia.

2. 'Backrub'

Massage mat on the background of rainforest in Bali

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Awali waalipa Google jina jina 'Backrub'.

Waanzilishi wa Google Larry Page na Sergey Brin awali waliipa Google jina jina 'Backrub'.

Haikumaanisha kisugua mgongo lakini ilimaanisha mfumo wa kuorodhesha vitu.

3. Mchezo

Google front page appears askew when you google the word "askew"
Maelezo ya picha, Usishangae hamna tatizo lolote na macho yako

Google haihusu tu biashara. Kuna mchezo pia.

Andika jina "askew" kwa Google na ujionee...

4. Mbuzi

Two goats agains a bright blue sky

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna lishe kwa mbuzi huko Google

Google inasema inaunga mkono mazingira kwa hivyo moja ya njia ni kubadilisha mashine za kufyeka na mbuzi.

Bustani kubwa za makao makuu ya Googleplex huko Mountain View, California, zinahitaji watu wa kuzitunza kila wakati, kwa hivyo kile unachokiona ni karibu mbuzi 200 wanaozunguka huku wakitafuta lishe.

5. Biashara inayokua

Social media logos printed onto handmade cubes. photographed in a studio.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Google imekuwa ikinunua kampuni kila wiki tangu mwaka 2010.

Baada ya kuunda kampuni za GMail, Google Maps, Google Drive, Google Chrome...Google imekuwa ikinunua kampuni kila wiki tangu mwaka 2010.

Hautajua lakini kampuni kama Android, Youtube, Waze na AdSense zinamilikiwa na Google na kuna zingine 70.

6. Nembo

A space drawing by Ryan Shea, a 7th grader at Creighton Middle School in Lakewood, is the Colorado winner in the Doodle 4 Google contest, April 29, 2014.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nembo ya kwanza ya Googe au Doodle ilikuwa na nia ya ujumbe wa tarehe 30 Agosti mwaka 1998.

Nembo ya kwanza ya Google au Doodle ilikuwa na nia ya ujumbe wa tarehe 30 Agosti mwaka 1998.

Hilo liliamuliwa wakati Larry na Sergey walikwenda huko Nevada kwa warsha moja iliyofahamika kama (Burning Man Festival) ndipo wakataka watu wafahamu kuwa hawakuwa karibu kuwahudumia.

Tangu wakati huo imekuwa kawaida kwa Google kufanya hivyo kila mara kuashiria siku fulani au watu fulani.

7. Fursa iliyopotezwa lakini si kwa Google

Mgao katika soko
Maelezo ya picha, Mgao katika soko

Mwaka 1999 Larry na Sergey walijaribu kuiuza Google kwa dola milioni moja lakini hakuna mtu aliyetaka kuinunua hata licha ya bei kushushwa.

Google kwa sasa ina thamani ya dola bilioni 300. Kuna mtu anajutia sana.

8. Kauli mbiu

Close-up of "evil" and "angel" eggs, against blue background.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, 'Usiwe muovu' ilikuwa moja ya kauli mbiu ya kwaza ya kampuni hiyo.

'Usiwe muovu' ilikuwa moja ya kauli mbiu ya kwanza ya kampuni hiyo.

Iwapoa kampuni imedumisha hilo au la ni wewe uamue.

9. Chakula ni muhimu sana

Sculptures of an Android and a cherry pie at at the entrance of Googleplex, Google's HQ in the south San Francisco bay area

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna chakula kila wakati huko Google

Kulingana na jarida la Forbes, mwanzilishi wa Google Sergey Brin aliamua mapema kuwa hakuna ofisi ya Google inaweza kuwa umbali wa mita 60 kutoka mahala kuna chakula.

Kuna uvumi kuwa siku za mwanzo chakula bora kwenye kampuni hiyo kilikuwa ni kitu kilikuwa kinaitwa "Swedish Fish", lakini siku hizi wafanyakazi wa Google, (ambao ni mimi na wewe) wanaweza kupata vyakula vizuri kama kahawa ya kiwango cha juu.

10. Rafiki mkubwa wa Google.

An Alaskan Malamute dog, sitting on an office floor and looking for people

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbwa na rafiki mkubwa wa Google

Wafanyakazi wa Google au wasio wafanyakazi huruhusiwa kupeleka mbwa wao kazini lakini wawe wamefunzwa vizuri wasije wakachafue ofisi.