Liverpool na Chelsea zapanda kileleni mwa jedwali la ligi ya Uingereza

Sadio Mane akicheka na wavu dhidi ya Leicester

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa makosa ya Alisson yalikuwa yatafanyika siku moja baada ya kikosi chake kujitahidi na kuimarisha uongozi wake kwa asilimia 100 baada ya kuilaza Leiecester.

Kikosi cha Klopp kilionyesha umahiri wake baada ya Mo Salah kukosa bao la wazi kabla ya Sadio Mane kuingia katika eneo hatari na kufunga bao baada ya dakika 10.

Nafasi ya Liverpool ilizidi kuimarika baada ya Roberto Firmino kufunga kona iliopigwa na james Milner na kufanya mambo kua mbili nunge kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Lakini walifanya mambo kuwa magumu baada ya Allison kufanya masikhra na kuwapatia lwicester bapo la kwanza.

Chelsea imeshinda memchi yake ya nne ya ligi ya Uingereza msimu huu

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huohuo Chelsea imepanda katika nbafasi ya pili ya jedwali la ligi baada ya kuilaza Bournemouth kupitia mabao yaliofungwa na Pedro na Eden hazard.

The Cherris walikuwa wameimarisha lango lao kabla ya Pedro kufunga dakika saba baada ya kuingia mahala pake Willian.

Raia huyo wa Uhispania aligusiana na Olivier Giroud kabla ya shambulizi lake kumfunga kipa Asmir Begovic.

Hazard aliongeza bao la pili kupitia shambulizi zuri huku beki wa Bournemouth na mchezaji wa zamani wa Chelsea Nathan Ake kukosa bao la wazi.