Becky: Nitakuwa na mahusiano mapya bila maambukizi

Chanzo cha picha, BBC Three
Nilikuwa nimeketi nikiwa mbele ya mshauri wa afya nikiwa na binti yangu niliyempakata, wakati maneno ambayo yangeweza kubadilisha maisha yangu yalipotamkwa:
''Majibu yako yanaonyesha una virusi vya UKIMWI.''
Kivipi? Nilikuwa wa baridi kwa mshtuko.Mwili wangu sikuusikia tena, wakati machozi yalipoanza kunitiririka kwa kasi mashavuni mwangu.
maswali mengi yalizungka kichwani kwangu:Nilikuwa nakaribia miaka 30, nitaweza kuishi zaidi ya umri wa miaka 40? Nitaweza kuwa na watoto zaidi? nitaweza kuwa kwenye mahusiano tena? lakini mwisho nilijiambia ''hapana siwezi''.
Ninakumbuka nilikuwa nikitazama kupitia dirishani wakati mshauri alipokuwa akinihakikishia kuwa haina maana kuwa hali hii ni adhabu ya kifo, na kuwa ni taishi maisha marefu a yenye afya.Nilichokuwa nafikiria ni yale matangazi ya miaka ya 80 yaliyokuwa yakisema ''UKIMWI unaua''.Kila mtu anakumbuka matangazo hayo, au sivyo? .
Kabla sijaathirika nilikua nimeolewa na mwanaume mmoja ambaye tulipokutana nilikuwa na miaka 18.Tulikutana chuoni,na alipohitimu, niliamua kuacha kozi yangu mapema ili tuanze maisha ya kufanya kazi.Tulikuwa na furaha mwanzoni lakini tulikutana tukiwa wadogo sana, na miaka 10 baadae tulikuwa watu tofauti.
Tulipata mtoto wa kike, jambo ambalo lilikuwa jema sana lakini niliona nilikua tegemezi kwake , niliogopa kuwa peke yangu

Chanzo cha picha, BBC Three
Niliamua kumuacha na kusitisha mahusiano yetu yaliyodumu kwa muongo mmoja, aliondoka na nikajihisi niko huru; ulikuwa ni uamuzi wa kwanza kuwahi kufanya na ikajisikia kama ninaweza kuishi maisha yangu kwa matakwa yangu.
Baada ya muda kidogo nilianza kutafuta mwenza mtandaoni na nikakutana na mwanaume mmoja ambaye aliishia kuniambukiza virusi vya ukimwi.Tangu nilipomuona nilijisikia vizuri sana.Sikuwahi kuvutiwa na mtu kiasi hicho.Lakini mwanzoni tu mwa mahusiano hayo mapya, nikaambukizwa virusi.Tayari alikuwa na maambukizi lakini hakuwa akifahamu kwa wakati huo;Ni kitu ambacho tungekibaini pamoja.
Nilikuwa mdogo, mama ambaye ana mtoto anayelea mwenyewe hayo pekee yalikuwa mwengi sana kuyakabili, ukiongezea na hali yangu, ilikuwa hali mbaya sana.
Kwa mara ya kwanza tulipojamiiana tulitumia kinga.Na mara ya pili pia, lakini hatimaye tulikuwa wenye tamaa hatukutumia mpira,na kwa kuwa tulishafanya hivyo mara ya kwanza, ilikuwa rahisi kufanya tena.Sikuwa na shinikizo kufanya hivyo isipokuwa tulipitiwa kwa wakati huo.
Nafikiri ningemuuliza kama alipima, lakini nilifungwa kwa ile hali ya kuwa mtu mpya alikuwa akivutiwa na mimi na sikuwahi kuwaza jabo jingine lolote.Sijui kama ningefanya kwa namna nyingine tofauti, kutokana na niliyoyapitia hapo nyuma nafikiri vilinifanya nishindwe kuwa mdadisi wake kuhusu afya yake.

Chanzo cha picha, BBC Three
Mimi ndiye niliyebaini kwanza. Wote tulikwenda kwa ajili ya uchunguzi, na nilipangiwa kuchunguzwa mapema.Nilikuwa nikijisikia mchovu , kabla ya kwenda kupimwa niliangalia kwenye mtandao wa google niliandika UKIMWI kisha nikaona hali niliyonayo ni moja ya dalili.Kidogo niliingiwa na hofu na kufikiria ''Vipi kama nimeathirika'' lakini niliyaondoa hayo mawazo. Kisha waliniita ili kunipa majibu , lakini bado nilifikiri kuwa itakuwa jambo dogo tu.
Walimfanyia vipimo na majibu yake yalionyesha kuwa ameathirika pia.Alianza kulia na kuanza kuniomba msamaha.
Hali ya kuwa tumeathirika tulikuwa tukishirikiana ,tulikuwa pamoja.Sikuwa na hasira kwa wakati huo,kwa sasa hasira zinakuja na kupotea lakini zamani nilikuwa na jukumu la kuukabili ukweli kwa kile kinachonisumbua

Chanzo cha picha, BBC Three
Katika hatua za mwanzo, virusi vilikua na athari kubwa mwilini kwangu, nilipungua uzito ndani ya kipindi kifupi , nilikuwa nimekonda na nilikuwa dhaifu.Lakini mara niliimarika nikawa mwenye nguvu na nilielewa safari niliyonayo kuhusu afya yangu katika maisha yangu.
Nilikuwa nataka kuzungumza na watu ambao wanaelewa nilichokuwa nakipitia na ndio moja ya sababu ya kusimulia hadithi yangu, kuwaambia wanawake kama mimi walio na virusi vya ukimwi kuwa yanaweza kukupata kama yangu, na kuwa unaweza kuwa na wakati mgumu sana lakini utakuwa sawa.
Kulikuwa na hatua mbalimbali nilizozipitia kutokana na virusi hivi.Lakini sasa kuwa katika hali hii kumenipa hali ya kujiamini na kuwa mwenye nguvu katika maisha yangu .
Nilipokuwa mdogo, niliuchukia mwili wangu.Nilikuwa mnene na nilikuwa najaribu kulificha tumbo langu, nilikuwa sijiamini kuhusu hilo.Nilikuwa nikibadilishia nguo bafuni na kuhakikisha kuwa mgongo nimeuelekeza aliko mume wangu wa zamani kwa kuwa nilikuwa naona aibu kwa namna nilivyokuwa nikionekana.
Kuathirika kwangu kulibadili namna nilivyouona mwili wangu.Nilidhoofu miezi michache ya kwanza lakini hali hiyo ilipoisha, niligundua ni kwa namna gani mwili wangu ulikuwa mzuri, nilirudisha uzito wangu niliokuwa nao na nilikuwa sijifichi tena.
Niligundua kuwa uhusiano wangu na aliyekuwa mume wangu haukua wa manufaa na tukaachana kwa sababu ambazo hazina uhusiano wowote na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Chanzo cha picha, BBC Three
Baada ya hayo, kuanzisha mahusiano mengine ilikuwa tofauti, Nilikutana na mwanaume mmoja mtandaoni ambaye ningeweza kufikiri kuwa naye.Alikuwa mdogo wa umri kuliko mimi jambo ambalo si tatizo, tulikuwa tunazungumza usiku mzima, tulikuwa tunaendana sana.Nilipofikiria kuwa tunaelekea kuanzisha uhusiano nilimweleza hali yangu, lakini mambo yalikuwa mabaya.alishtushwa sana,ilionekana usoni kwake.Nafikiri aliona kuwa ni mapema sana na nilimwambia kuwa anaweza kuwa hatarini kuambukizwa.
Pamoja na kutaka kumuelewesha kuhusu hali yangu alitaka kuondoka nyumbani kwangu haraka.Alikuwa kwenye mshtuko.
Hali hii ilinifanya nijihisi mwenye hatia kwa kutosema chochote mapema.Hata hivyo nina amani nilimweleza, ingawa tuliachana.Lakini sasa ninajua kuwa yeyote nitakayekuwa naye anatakiwa kuwa muwazi na muelewa,kwa kuwa kuna wakati nitahitaji msaada wao.Lilikuwa somo zuri kuhusu ninachokihitaji kutoka kwa mwenza.
Ninahitaji kuwa na mtu na kutengeneza naye familia, jambo linalowezekana ikiwa nitataka kuwa mja mzito tena. Sasa kwa kuwa ninajisikia vyema na hali niliyonayo, ninajua hakuna kinachonizuia kuwa na maisha ya baadae ninayoyataka.













