Mamba apatikana akitangatanga ndani ya mji wa Melbourne Australia

Chanzo cha picha, VICTORIA POLICE
Polisi nchini Australia wanamtafuta mmiliki wa mamba mdogo ambaye alipatikana akitangatanga kwenye mitaa ya mji wa Melbourne siku ya Krismasi.
Wenyeji waliokuwa wakitembea saa za jioni wallikumbana na mamba huyo nje ya maduka ya biashara.
Polisi huko Victria wanasema kuwa wakati waliitwa walidhani alikuwa ni mamba mkubwa.
Badala yake waligungua kuwa alikuwa mamba mdogo wa urefu wa mita moja ambaye alikuwa ametulia kwenye njia ya watembea miguu
Mtu anayeshika nyoka Mark Pelley aliitwa kumshika mamba huyo.
Mamba huyo alijaribu kutorokea vichakani lakini akashikwa kwenye mkia na sasa yuko mikononi mwa mamlaka za wanyapori
Watu huko Victoria huruhusiwa kuwafuga mamba wa hadi urefu wea mita 2.5








