Kimbunga Irma chaendelea na uharibifu mkubwa huko Caribbean

This satellite image obtained from the National Oceanic and Atmospheric Administration (NOAA) shows Hurricane Irma at 11:30 GMT on 6 September

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Irma kikionekana kutoka angani

Kimbunga Irma kimeelekea visiwa vya Turks na Caicos baada ya kusababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean na kuwaua takriban watu 14.

Visiwa vilivyo nyanda za chini vinaripotiwa kuwa kwenye hatari kubwa kukiwa na uwezekano wa kupigwa na mawimbi ya hadi urefu wa mita 6 kuliko viwango vya kawaida.

Flooding in Saint Martin, 6 September

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mitaa iliyofurika huko St Martin

Kumeripotiwa uharibifu na mafuriko nchini Haiti ambapo miundo mbinu bado ni mibaya tangu litokee tetemeo la ardhi mwaka 2010.

Irma ni kimbunga cha kiwango cha tano.

Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi cha kimbunga na upepo wake una kasi ya kilomita 280 kwa saa.

A photo taken on September 6, 2017 shows the Hotel Mercure in Marigot, near the Bay of Nettle, on the French Collectivity of Saint Martin,

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Mafuriko huko St Martin

Takiban watu milioni 1.2 wameathiriwa na kimbunga Irma na idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa haraka hadi watu milioni 26.

Kuna wasi wasi kuwa ugonjwa unaweza kusambaa kwa haraka maeneo ambapo maji ya kunywa na huduma za usafi zimeathirika, na maafisa wameonya kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.

Flood damage on Saint Martin, 6 September

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mafuriko zaidi Saint Martin

Irma sasa kiko karibu na visiwa vya Turks na Caicos na huenda pia kikaelekea huko Bahamas.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kufika Cuba baadaye kabla ya kupinga jimbo la Florida huko Marekani mwishoni mwa wiki huku mkuu wa shirika la huduma za dharura la Mareknia akitabiri uharibifu mkubwa.

Damage done to Sint Maarten from Hurricane Irma, 7 Sept 2017

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Uharibifu huko Sint Maarten

Maandalizi ya kuwasili kimbunga Irma yalifanywa katika visiwa vya Turks na Caicos ambayo ni himaya ya Uingereza yenye vyenye watu 35,000.

Irma pia kilisababisha uharibifu kwa paa za nyumba na kawi katik sehemu za kaskazini mwa Jamhuri ya Dominica.

Nchini Cuba maelfu ya watalii kutoka maeneo ya kistarehe ya pwani wamehamishwa.

People put up shutters as they prepare the Actors' Playhouse at the Miracle Theatre for Hurricane Irma in Miami, Florida, 6 September

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Biashara zafungwa Miami kabla ya kimbunga
line