Kwa Picha: Uharibifu wa Kimbunga Irma Caribbean

Kimbunga hivi cha ngazi ya juu zaidi kimesababisha uharibifu mkubwa sana visiwa vya Caribbean, na jimbo la Florida limewekwa kwenye hali ya tahadhari Marekani.

Gustavia Saint-Barthélemy

Chanzo cha picha, Facebook/ Kevin Barrallon

Maelezo ya picha, Kimbunga hicho kimeharibu nyumba na biashara, na kukatiza umeme maeneo mengi. Watu 10 wamethibitishwa kufariki kufikia sasa. Hapa ni ufukweni katika mji wa Gustavia kisiwa cha Saint-Barts
British Virgin Islands

Chanzo cha picha, Ron Gurney/Handout via REUTERS

Maelezo ya picha, Katika visiwa vya Virgin Islands vya Uingereza, upepo mkubwa na mawimbi vinaonekana vikisukuma meli na boti hadi ufukweni
Kimbunga

Chanzo cha picha, Handout/ RCI Guadeloupe

Maelezo ya picha, "Ni janga kubwa, kisiwa kimeharibiwa 95%. Nimesikitishwa sana," afisa wa kisiwa cha Saint-Martin Daniel Gibbs amesema kwenye mahojiano.
Kimbunga

Chanzo cha picha, Handout

Maelezo ya picha, Jeshi la Uholanzi limetoa picha za kutoka angani zikionesha uharibifu Sint Maarten, eneo la kisiwa cha St Martin linalomilikiwa na Uholanzi. Kisiwa hicho kimegawanywa mara mbili - eneo la Uholanzi na la Ufaransa.
Fajardo, Puerto Rico.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika jimbo la Puerto Rico. Nusu ya nyumba na biashara hazina umeme na maeneo mengi ya kisiwa hicho yamefurika maji.
Puerto Rico

Chanzo cha picha, AFP/ Getty Images

Maelezo ya picha, Ingawa Puerto Rico haijapigwa moja kwa moja, maafisa wa uokoaji wamelazimika kuondoa miti iliyoanguka pamoja na vifusi barabarani.
Puerto Rico

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kina cha maji kinatarajiwa kupanda kwa hadi 20ft (6m) maeneo mengi ya pwani Caribbean
Haiti

Chanzo cha picha, AFP/ Getty Images

Maelezo ya picha, Kaskazini mwa Haiti, watu waliondoa vitu vyao vya thamani kutoka kwenye paa za nyumba wakijiandaa kwa Irma.
Kimbunga

Chanzo cha picha, AFP/ Getty Images

Maelezo ya picha, Kituo cha Taifa cha Vimbunga cha Marekani kimetahadharisha kwamba juhudi za kulinda maisha na mali zinafaa kuharakishwa kabla ya kimbunga hicho kupitia maeneo yanayotarajiwa kupigwa na kimbunga hicho.
Dominican Republic

Chanzo cha picha, AFP/ Getty Images

Maelezo ya picha, Wakazi maskini wa Santo Domingo katika Jamhuri ya Dominika wana wasiwasi kuhusu athari za upepo na maji kwenye nyumba zao.
Richard Branson

Chanzo cha picha, Virgin.com

Maelezo ya picha, Richard Branson amekuwa katika kisiwa chake cha kibinafsi cha Necker, katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza wakati wa kimbunga hicho.
Kimbunga

Chanzo cha picha, AFP/ Getty Images

Maelezo ya picha, Vimbunga vimekuwa vikipiga pwani ya Florida mara kwa mara lakini Irma ndicho kimbunga chenye nguvu zaidi kuwahi kutokea Atlantiki katika kipindi cha mwongo mmoja.
Kimbunga

Chanzo cha picha, AFP/ Getty Images

Maelezo ya picha, Wakazi wa Key West, Florida, wamekuwa wakijiandaa na wengine kuondoka maeneo yaliyo hatarini.
Kimbunga

Chanzo cha picha, AFP/ Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya maduka Florida yameishiwa na maji ya chupa. Katika baadhi ya maeneo, kumeripotiwa makabiliano kati ya wateja wakipiganuia maji na chakula.
Kimbunga

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Baada ya Irma, vimbunga Jose na Katia. Vinatarajiwa kufuata. Kimbunga Katia kinatishia pwani ya Mexico.