Irma, kimbunga kikali zaidi kuipiga Carribean

Maafisa wa serikali katika visiwa vya Caribbean wamewataka watu wanaoishi katika maeneo hayo kuondoka kwa sababu upepo mkali zaidi ambao haujawahi kutokea katika bahari ya Atlantic unakaribia.
Kimbunga Irma kimeorodheshwa kama kimbunga kibaya zaidi kuwahi kutokea huku kikiambatana na upepo wenye kasi ya takriban kilomita mia tatu kwa saa moja.
Viwanja vya ndege vimefungwa katika visiwa mbalimbali huku watu wakiambiwa wajikinga katika maeneo ya umma.

Katika kisiwa cha Antigua, ambapo upepo huo ndio unapita, ndege ya Marekani ambao ina vifaa vya matibabu imewekwa karibu na Puerto Rico.
Gavana wa jimbo la Florida amewaambia wakazi wa eneo hilo kuchukua tahadhari wakati kimbunga kinatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi.
Jeshi la Uholanzi limewasili katika kisiwa cha Saint Martin katika meli mbili na helikopta wakiwa tayari kutoa msaada.












