Kimbunga Irma kupiga Cuba,Caicos na Haiti

Muelekeo wa kimbunga Irma
Maelezo ya picha, Muelekeo wa kimbunga Irma

Haiti, Cuba na visiwa vya Turks na Caicos vinajiandaa kwa kuwasili kwa kimbunga Irma, ambacho tayari kimefanya uharibu mkubwa katika visiwa vyengine vya Caribbean.

Mawimbi makubwa, mafuriko na upepo mkali vinatarajiwa huku maafisa wa serikali ya Haiti wakizunguka kila nyumba kushawishi watu waondoke.

Nako nchini Cuba, mamia na maelfu ya wananchi wameambiwa waondoke majumbani mwao.

Cuba ni kisiwa kikubwa katika eneo la Caribbean ,ambacho kipo katika mkondo wa kimbunga.

Kimbunga Irma tayari kimetandika Barbuda, St Martin na visiwa vya Marekani vya Virgin, ambapo msemaji wa serikali amethibitisha watu wanne kuuawa.

Kimbunga Irma kimeleta madhara makubwa maeneo ya Carribean
Maelezo ya picha, Kimbunga Irma kimeleta madhara makubwa maeneo ya Carribean

Wakati huo huo, zaidi ya watu nusu milioni wameamriwa waondoke majumbani mwao katika jimbo la Florida kabla kimbunga Irma hakijapiga jimbo hilo la Marekani siku ya Jumapili.

Kumekuwa na hali ya vurumai takriban kwa siku nzima katika uwanja wa ndege wa Miami huku watu wakikimbilia kupanda ndege kuondoka.

Watalii wingi nao wamekwama baada ya ndege zote kujaa.

Kumekuwa pia na upungufu wa nishati ya mafuta kaskazini kutoka jimbo la Florida.

Baadhi ya madhara ya kimbunga Irma
Maelezo ya picha, Baadhi ya madhara ya kimbunga Irma

Gavana wa Florida, Rick Scott, amesema kumekuwa na maandalizi makubwa ya tahadhari ya kimbunga Irma:

Wakati huo huo, gavana wa jimbo la Georgia ambalo liko jirani na Florida ametaka watu waondoke katika maeneo ya pwani.