Aliyetetea ukoloni afukuzwa chamani Afrika Kusini

Helen Zille ni mwanasiasa maarufu Afrika Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Helen Zille ni mwanasiasa maarufu Afrika Kusini

Chama kikuu cha upinzani cha Afrika Kusini, Democratic Alliance, kimesimamisha uanachama wa kiongozi wake wa zamani, Helen Zille, kwa sababu ya tweet aliyoandika, ambapo alisema, siyo ukoloni wote mbaya.

Kiongozi wa sasa wa chama, Mmusi Maimane, alisema hata hivyo, Bibi Zille atabaki na wadhifa wake, kuwa waziri kiongozi wa Jimbo la Cape Magharibi.

Chama cha Democratic Alliance kimeshinikizwa Bibi Zille achukuliwe hatua tangu tweet zake kuzusha utatanishi awali mwaka huu.

Mwandishi wa BBC anasema, chama cha Democratic Allience, kinajaribu sana kuondosha wazi, kwamba kwa jumla, kinawakilisha masilahi ya wazungu wa Afrika Kusini.

Tweet from Helen Zille reads: "For those claiming legacy of colonialism was ONLY negative, thing of our independent judiciary, transport infrastructure, piped water etc."

Chanzo cha picha, Twitter - @helenzille

Tweet from Helen Zille reads: "Would we have had a transition into specialised health care and medication without colonial influence? Just be honest, please"

Chanzo cha picha, Twitter - @helenzhille