Uzalishaji wa zao la coca waongezeka maradufu nchini Colombia

Serikali ya Marekani imesema uzalishaji wa zao la coca inayotengeneza cocaine umevuka mipaka nchini Colombia.
Ripoti zinasema kuwa maeneo ya uzalishaji yameongezeka mara mbili ya ilivyokuwa miaka mitano iliyopita ikiwa ni takriban hekta laki moja na elfu tisini.
Hii inaweza kutengeneza mpaka kilo mia saba za cocaine kwa mwaka.

Serikali ya Marekani inaamini kuwa kuachwa kupuliziwa kwa dawa maalumu ya kukausha zao hilo kwa njia ya helikopta imekuwa sababu ya kuongezeka kwake.
Serikali ya Colombia imesema hekta elfu hamsini zitateketezwa mwaka huu na zilizobaki zitateketezwa taratibu.








