Tuzo ya Nobel iliotunukiwa mwanaharakati yaibwa India

Bw Satyarthi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Bw Satyarthi

Tuzo ya medali ya Nobel aliyopewa mwanaharakati wa haki za watoto Kailash Satyarthi imeibiwa nyumbani kwake katika mji mkuu wa Delhi.

Bw Satyarthi aliambia BBC kwamba cheti cha tuzo hilo la Nobel pia kimetoweka kufuatia wizi huo siku ya Jumanne alfajiri.

Anasema kuwa hakukuwepo na mtu wakati wizi huo ulipofanyika.

Bw Satyarthi alitunukiwa tuzo hiyo mwaka 2014 kwa kazi yake ya kukabiliana na ajira za watoto mbali na ulanguzi wa watoto nchini India.

Aligawana tuzo hiyo na mwanaharakati Malala Yousafzai kwa kazi yake ya elimu ya wanawake.

Tuzo ya Nobel iliopewa Bw Satyarthi

Chanzo cha picha, BHASKER SOLANKI

Maelezo ya picha, Tuzo ya Nobel iliopewa Bw Satyarthi

Bi Satyarthi alisema kuwa maafisa wa polisi mjini Delhi walichunguza wizi huo.

''Kufuli ya nyumba yangu ilivunjwa na cheti na medali kuibwa mbali na vitu vyengine vichache. Bado tunaendelea kuangalia ni nini kilichoibwa'',alisema