Mamilioni ya Wanigeria wapiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali zaidi kuwahi kushuhudiwa

Chanzo cha picha, Reuters
Mamilioni ya Wanigeria wanapiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali zaidi wa urais tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi.
Tangu mwaka 1999, nchi hiyo maarufu zaidi barani Afrika imekuwa ikitawaliwa na vyama viwili – chama tawala cha APC na cha PDP.
Lakini wakati huu, kuna pia mgombea wa tatu kutoka chama cha Labour Peter Obi, ambaye anaungwa mkono na vijana wengi.
Rais wa sasa wa Nigeria Muhammadu Buhari hagombei kiti hicho tena baada ya kuhudumu kwa mihula miwil.i
Chama chake -All Progressives Congress (APC) kinawakilishwa na gavana wa zamani wa Lagos Bola Tinubu, huku makamu wa rais wa zameni Atiku Abubakar akigombe kwa tiketi ya upinzani kupitia chama kikuu cha upinzani ha Peoples Democratic Party (PDP). Kuna jumla ya wagombea 18 wa kiti cha urais.
Kura za maoni kabla ya uchaguzi zilitawaliwa na uhaba wa fedha uliosababishwa na jaribio la kubadilisha sarafu ya nchi, na hivyo kusababisha kuendea kwa vurugu katika benki na machine za kutoa na kuweka pesa - ATM 2, huku watu waking’ang’ana kutoa pesa zao.
Noti mpya zilitolewa ili kukabiliana na mfumuko wa bei, na pia kununua kura. Siku moja kabla ya uchaguzi mbunge wa Bunge la wawakilishi alikamatwa na akiwa na $500,000(sawa na £419,000) pesa taslimu na orodha ya watu aliopaswa kuwapatia, ilisema polisi.
Yeyote atakayeshinda itabidi ashughulikie uundwaji mpya wa sarafu, kuyumba kwa uchumi, ukosefu wa hali ya juu wa ajira kwa vijana, na ukosefu wa usalama wa hali ya juu ambao ulisababisha vifo vya watu 10,000 mwaka jana.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Baada ya mauaji ya mgombea wa kiti cha seneti Jumatano wiki hii yanayoshukiwa kutekelezwa na watu wneye silaha kutoka katika kikundi kinachotaka kujitenga, Ipob, uchaguzi wa wabunge uliahirishwa katika jimbo la kusini -mashariki la Enugu East.
Uchaguzi huu umewavutia wapiga kura wengi wanaopiga kura kwa mara ya kwanza pamoja na vijana- theluthi ya watu milioni 87 wenye uwezo wa kupiga kura wana chini ya umri wa miaka 35 – jambo linaloweza kupelekea kkuongezeka kwa idadi ya wapiga kura kuliko 35% iliyorekodiwa mwaka 2019.
"Ni wajibu wang una nimeona jinsi kura yangu ilivyo muhimu," Blessing Ememumodak mwenye umri wa miaka 19, anayepiga kura kwa mara ya kwanza aliiambia BBC mjini Lagos.
Bw Obi, 61,anatumai kuvunja mfumo wa vyama viwili baada ya -kujiunga na chama cha Leba Labour Party mwezi Mei mwaka jana.
Ingawa alikuwa katika chama cha PDP kabla yah apo, anaonekana kama sura mpya na ana uungaji mkono miongoni mwa baadhi ya vijana wa Nigeria, hususan kutoka katika maeneo ya kusini mwa nchi.
Mfanyabiashara huyu Tajiri alihusumu kama gavana wa jimbo la kusini-magharibi la Anambra State kuanzia mwaka 2006 hadi 2014. Wafuasi wake wanamfahamu kama mgombea mwenye maadili akifahamika kama "OBIdients" wanasema ndiye mgombea pekee mwenye maadili, lakini wakosoaji wake wanasema kwamba kumpigia kura Obi ni kuipoteza kwasababu huenda asishinde.
Badala yake, PDP, ambacho kiliongoza hadi mwaka 2015, kinataka Wanaigeria wampigie kura Atiku Abubakar, 76 – mgombea pekee mkuu kutoka eneo la kaskazini lenye idadi kubwa ya waislamu.
Amegombea urais mara tano kabla – na mara hizo zote amekuwa akishindwa.
Amekumbwa na shutuma za ufisadi na upendeleo, ambazo anazikana.
Katika muda wake mwingi wa kazi yake amekuwa mamlakani, ambapo alikuwa mkuu wa wafanyakazi wa umma, makamu wa rais na mfanyabiashara maarufu.
Watu wengi wanachukulia uchaguzi kama kura ya maamuzi kwa chama cha APC, ambacho kimehudumu katika kipindi cha hali ngumu ya uchumi na kuzoroteka zaidi kwa usalama wa nchi.
Mgombea wake, Bola Ahmed Tinubu, 70, alisifiwa kwa kujenga mji wa kibiashara wa Nigeria Lagos, wakati wa mihula yake miwili kama gavana hadi mwaka 2007.
Anafahamika kama baba wa siasa katika kanda ya kusini- magharibi, ambako amejivunia ushawishi mkubwa, lakini saw ana Bw Abubakar, amekuwa akikabiliwa na madai ya ufisadi kwa miaka mingi na afya mbovu, madai ambayo amekuwa akiyakana.
Uchaguzi unaanza kuwanza saa mbili unusu asubuhi kwa saa za Nigeria (07:30 GMT), ingawa yeyote ambaye ataweza kuwepo kwenye mstari wa kupiga kura hadi saa `nane unusu mchana ataweza kupiga kura yake.
Uchaguzi pia unafanyika wa maseneta wa shirikisho 109 na wabunge 360 wa bunge la wawakilishi , huku ule wa magavana ukitarajiwa kufanyika mwezi Machi.

Chanzo cha picha, Reuters
Tume huru ya taifa ya uchaguzi (Inec)imeahidi kuendesha uchaguzi wa haki na huru, na imepuuzilia mbali mazungumzo ya kuahirisha uchaguzi huku kukiwa na hofu ya usalama katika baadhi ya maeneo ya nchi na uhaba wa pesa taslimu ambao wengi wanahofia kuwa unaweza kuathiri maandalizi yake.
Ni mara ya kwanza kwa Inec kuendesha uchaguzi wa taifa kwa kutumia mfumo wa teknolojia ya utambuzi wa wapiga kura - Bimodal Voter Accreditation System (BVAS), unaotambua sura na vidole , hilo linadhaniwa kuwa linaweza kuboresha uwazi kwa kufanya hali kuwa ngumu kwa wanasiasa kuiba katika mchakato wa kuiba kura.
Matokeo ya mwisho yamekuwa yakitangazwa katika siku ya tatu baada ya kura katika chaguzi mbili zilizopita, lakini huenda yakatangazwa mapema wakati huu kwasababu ya mfumo wa BVAS, ambao pia una uwezo wa kupakua matokeo ya kura moja kwa moja kwenye wavuti wa tume ya uchaguzi Inec kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.
Mgombea anahitaji kuwa na kura zaidi na 25% ya masanduku yaliyopigwa katika theluthi mbili ya majimbo yote 36 ya Nigeria ili kutangazwa kuwa mshindi.
Kama hakuna atakayefanikiwa hilo, kutakuwa na awamu ya pili ya uchaguzi ndani ya siku 21 - na hii itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Nigeria.
Katika chati zifuatazo, ni baadhi ya changamoto zinazowazonga wapiga kura.
















