Kwa nini vita vya sasa vya Gaza ni tofauti na vita vilivyopita?

t4rgfv

Chanzo cha picha, REUTERS

    • Author, Jeremy Bowen
    • Nafasi, Mhariri wa BBC

Iwapo vita vya sasa huko Ukanda wa Gaza vingekuwa kama vita vilivyopita, pengine usitishaji wa mapigano ungekuwa umeshafikiwa kwa sasa.

Waliokufa wangezikwa na Israel ingekuwa katika Umoja wa Mataifa ikijadili kuhusu kiasi gani cha saruji kiruhusiwe kutumwa katika Ukanda wa Gaza kwa ajili ya kujengwa upya.

Lakini vita vya sasa si kama vita vya zamani. Kwa sababu nyingi tu. Kwanza, Hamas iliingia Israeli Oktoba 7 na kisha, kwa maneno ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, 'watalipiza kisasi.'

Watu wengi waliouawa na Israel ni raia wa kawaida wa Palestina.

Mtandao wa Iran

dsxz

Chanzo cha picha, WAEL HAMZEH/EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK

Mtandao wa Iran, ama pia huitwa 'mhimili wa upinzani,' unajumuisha Hezbollah ya Lebanon, utawala wa Bashar al-Assad wa Syria, waasi wa Houthi wa Yemen na wanamgambo wa Iraq.

Wanamgambo wa Iraq wamepokea mafunzo na silaha kutoka Iran. Iran pia inaunga mkono Hamas na Islamic Jihad ya Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Kwa upande mwingine, Iran pia inaongeza ukaribu wake na Urusi na China. Iran imekuwa mshirika muhimu katika vita vya Urusi vinavyoendelea nchini Ukraine. China inanunua kiasi kikubwa cha mafuta kutoka Iran.

Maadamu vita vya Gaza vinaendelea, na Israel ikiendelea kuwaua Wapalestina na kuharibu makazi yao, kutakuwa na hatari ya wanachama wa mtandao wa Iran kujiunga na mzozo huu.

Mvutano unaongezeka polepole kwenye mpaka kati ya Israel na Lebanon. Pande zote mbili Israel na Hezbollah zinaonekana hazitaki vita kamili kwa sasa.

Biden hana raha

dc

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Joe Biden

Waasi wa Houthi kutoka Yemen wanaishambulia Israel kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora, hadi sasa yamedunguliwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel na meli za kivita za Jeshi la Wanamaji la Marekani zilizopo kwenye Bahari Nyekundu kabla ya kutua ardhini.

Wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran wameshambulia kambi za jeshi la Marekani nchini Iraq. Katika kulipiza kisasi, Marekani imelenga baadhi ya vituo vyao nchini Syria. Ingawa pande zote mbili zinaepuka kuzidisha makali ya mzozo.

Marekani inaunga mkono kikamilifu hatua inayoendelea ya Israel dhidi ya Hamas. Hata hivyo, ni wazi pia Rais wa Marekani Joe Biden hana raha na idadi kubwa ya vifo vya raia kutokana na mashambulizi ya Israel.

Wito wa kusitisha mapigano

ED

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema hadharani - idadi kubwa ya raia wa kawaida wa Palestina wanauawa. Washirika wote wa kiarabu wa Marekani wameilaani Israel na kuomba kusitishwa kwa mapigano.

Picha za maelfu ya Wapalestina wakikimbia makaazi yao na kuelekea kusini kutoka kaskazini mwa Gaza zimerudisha kumbukumbu za ushindi wa Israel dhidi ya ulimwengu wa Kiarabu mwaka 1948. Ni katika vita hivi Israel ndipo ilitangaza uhuru wake.

Mwaka huo zaidi ya Wapalestina laki saba walikimbia makaazi yao. Wengi wao walifukuzwa katika nyumba zao kwa mtutu wa bunduki na Waisraeli.

Wapalestina wanalikumbuka tukio hili kama 'Al Nakba' (yaani Siku ya Janga). Wakazi wengi wa Gaza ni vizazi vya Wapalestina waliokimbia makaazi yao 1948.

Baadhi ya makundi ya Wayahudi yanayounga mkono serikali ya Benjamin Netanyahu yanasema mambo ya hatari kama vile kuleta 'Al Nakba' nyingine kwa Wapalestina. Nchi za Kiarabu za Jordan na Misri zina wasiwasi.

Hofu ya Waarabu

CX

Chanzo cha picha, REUTERS

Maelezo ya picha, Njiwa akiruka juu ya vifusi vya nyumba huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza

Waziri katika serikali ya Netanyahu alipendekeza kurushwa mabomu ya nyuklia kwenye Ukanda wa Gaza ili kukabiliana na Hamas. Alikaripiwa lakini hakuondolewa kwenye wadhifa huo.

Matamshi kama haya yanaweza kutupiliwa mbali kama matamanio yasiyo na mantiki ya wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia, lakini huko Jordan na Misri yanachukuliwa kwa uzito mkubwa.

Israel ina akiba kubwa ya silaha za nyuklia ambazo hazijatangazwa.

Labda sio hofu ya matumizi ya silaha za nyuklia, lakini uwezekano wa kulazimishwa mamilioni ya Wapalestina kuvuka mpaka - ndilo jambo linalotazamwa kwa uzito na wasiwasi.

Wanadiplomasia katika baadhi ya nchi washirika wa Israel huko Magharibi - waliiambia BBC - ni jambo gumu kumaliza vita hivyo na kukabiliana na athari zake.

Suluhu ya mataifa mawili

K,

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Mwanadiplomasia mmoja alisema 'njia pekee ya suluhu itakuwa ni kujenga upya mazingira ya kisiasa kwa Wapalestina.' Akimaanisha kuundwa kwa taifa huru la Palestina pamoja na Israel. Wazo hili halijafanikiwa na sasa linasalia kama kauli mbiu tu.

Lakini wazo zuri zaidi ni kufufua aina fulani ya maelewano kati ya Israel na ulimwengu wa Kiarabu, jambo ambalo halitakuwa rahisi katika mazingira ya sasa yaliyojaa maumivu, chuki na vitisho. Mataifa mawili hayawezekani chini ya uongozi wa sasa wa Israel na Palestina.

Waziri Mkuu wa Israel, Netanyahu bado hajasema lolote kuhusu anachopanga kufanya baada ya vita vya Gaza kumalizika, lakini amekataa pendekezo la Marekani la kuacha udhibiti wa Gaza kwa Mamlaka ya Palestina.

Sehemu ya pili ya mpango wa Marekani ni kujadili 'suluhu ya mataifa mawili,' ambayo Benjamin Netanyahu ameipinga katika maisha yake yote ya kisiasa.

Uhuru wa Palestina

FDC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Netanyahu hapingi tu na uhuru wa Palestina, bali anategemea kuungwa mkono na wafuasi wa itikadi kali ya Kiyahudi wanaoamini eneo lote kati ya Mto Jordan na Bahari ya Mediterania lilitolewa na Mungu kwa Wayahudi na linapaswa kusimamiwa na Israel.

Kuna watu wengi nchini Israel wanaomlaumu Netanyahu kwa kushindwa kwa usalama na ujasusi baada ya mashambulizi ya Oktoba 7 na wanataka kumuondoa.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas sasa ana umri wa miaka 80. Wapiga kura wanamwona hafai. Hajakabiliwa na uchaguzi wowote tangu 2005.

Mamlaka ya Palestina inashirikiana na Israeli kwa ajili ya usalama katika Ukingo wa Magharibi, lakini haiwezi kuwalinda watu wake na mashambulizi ya Wayahudi wenye silaha.

Ikiwa vita hivi vya kutisha vya Gaza havitawatayarisha Waisraeli, Wapalestina na marafiki zao kuanzisha amani, basi vita vitaendelea katika siku zijazo.