Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

DF

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

Siku chache tu baada ya shambulio la Hamas tarehe 7 Oktoba, Rais wa Marekani Joe Biden alifika Tel Aviv na kueleza mshikamano wa Marekani na Israel.

Aliwaita Hamas ni 'mashetani' na kusema Marekani iko pamoja na Israel katika kila hali na itapata kila msaada.

Mwanzoni mwa mwezi Novemba, Bunge la Marekani liliidhinisha pendekezo la msaada wa kijeshi wa dola bilioni 14.5 kwa Israel.

Marekani pia inaonekana kuunga mkono msimamo wa Israel kuhusu kutositisha mapigano Gaza.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema siku ya Jumapili - usitishaji vita utainufaisha Hamas pekee.

Urafiki wao una umri gani?

ED

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Mfereji wa Suez ambapo Israel ilipigana

Rais wa Marekani Henry Truman alikuwa mwanasiasa wa kwanza duniani kuitambua Israel. Tarehe 2 Novemba 1917, Azimio la Balfour la Uingereza liliunga mkono kuanzishwa nchi ya Wayahudi huko Palestina.

Miaka miwili baadaye, Machi 3, 1919, aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo Woodrow Wilson aliunga mkono wazo la kuwa na nchi ya Wayahudi.

Baadaye mwaka 1922 na tena mwaka 1944, Bunge la Marekani lilipitisha maazimio ya kuunga mkono Azimio la Balfour. 1948 Marekani ikawa nchi ya kwanza kuitambua.

Ndani ya dakika 11 tangu Israel kujitangaza kuwa nchi, Marekani iliitambua Israel kama nchi. Rais wa wakati huo Harry Truman alikuwa kiongozi wa kwanza duniani kuitambua Israel.

Kwa nini Marekani iliitambua Israel haraka?

DC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani D. Eisenhower (kushoto) akiwa na Waziri Mkuu wa India Jawaharlal Nehru

Kilikuwa ni kipindi cha baada ya Vita vya Pili vya Dunia - wakati Vita Baridi kati ya Marekani na Muungano wa Sovieti vilipokuwa vinaanza.

Marekani ilivutiwa na nchi za Kiarabu kutokana na hifadhi zao za mafuta. Vilevile njia ya baharini ya Mfereji wa Suez - ilikuwa njia ya biashara ya kimataifa. Ulikuwa ni uwanja wa kupimana nguvu kati ya Marekani na Sovieti.

Marekani ilivutiwa na hifadhi ya mafuta katika ulimwengu wa Kiarabu. Kwa hiyo ilihitaji Israel ili kudhibiti nchi za Kiarabu. Hii ndiyo sababu kwa nini Marekani haikuchelewa kuitambua Israel na kuijengea uwezo wa kijeshi.

Nyakati za mivutano

EDFC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Benjamin Netanyahu akiwa na Barack Obama
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Licha ya uhusiano imara wa Marekani na Israel – lakini huko nyuma kumekuwa na mivutano katika uhusiano wao. Wakati Israel ilipoanzisha vita na Ufaransa na Uingereza juu ya Mfereji wa Suez, utawala wa Eisenhower wa Marekani uliikasirikia sana.

Rais wa Marekani alitishia ikiwa Israel haitaondoka katika maeneo iliyoyateka wakati wa vita, misaada itasitishwa.

Umoja wa Kisovieti pia ulitishia ikiwa Israel haitarudi nyuma, ingeishambulia kwa makombora. Chini ya shinikizo hilo, Israel ilibidi kurudi nyuma kutoka maeneo hayo.

Vile vile, katika miaka ya 1960, kulikuwa na mvutano katika uhusiano wa Marekani na Israel. Wakati huo, utawala wa Kennedy wa Marekani ulikuwa na wasiwasi kuhusu mipango ya siri ya Israel ya nyuklia.

Lakini 1967 baada ya Israel kuzishinda Jordan, Syria na Misri katika vita vya sita na kuteka eneo kubwa la ulimwengu wa Kiarabu, mtazamo wa Marekani kwa nchi hii ya Kiyahudi ulibadilika kabisa.

Wakati huo Marekani ilikuwa imejiingiza katika Vita vya Vietnam na Israel ilizishinda nchi za Kiarabu bila msaada wowote mkubwa kutoka Marekani.

Jambo jingine muhimu ni kwamba - nchi mbili ambazo zilishindwa na Israel, Misri na Syria, zilikuwa marafiki wa Umoja wa Kisovieti.

Baada ya ushindi huu wa Israel, Marekani ilianza kuiona Israel kama mshirika wa kudumu dhidi ya Umoja wa Kisovieti katika ulimwengu wa Kiarabu.

Obama, Netanyahu na Biden

EW

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Uhusiano kati ya Marekani na Israel ulionekana kuyumba kwa muda mfupi kutokana na tofauti kati ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa sasa wa Israel.

Kulikuwa na mzozo kati ya wawili hao kuhusu makubaliano ya nyuklia na Iran. Netanyahu alikwenda kwenye Bunge la Marekani linalotawaliwa na Chama cha Republican na kumkosoa vikali Barack Obama kuhusiana na sera ya Marekani kwa Iran.

Wakati wa utawala wake wa miaka minane, Obama alipinga maazimio yote dhidi ya Israel isipokuwa azimio moja katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Biden hivi karibuni alikosoa jaribio la Netanyahu la kubadili mfumo wa mahakama nchini Israel, lakini baada ya shambulio la Hamas Oktoba 7, ameonekana kusimama imara na Waziri Mkuu wa Israel.

Uhusiano wao sasa ikoje?

ED

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Kwa sasa, Marekani inafanya kazi kama mshirika wa ajabu wa Israel. Marekani inatoa msaada wa kifedha, kijeshi na kisiasa bila masharti kwa Israel.

Israel ina nguvu ya nyuklia ambayo haijatangazwa. Lakini kwa sababu ya kukingiwa kifua na Marekani haijawahi kukabiliwa na uchunguzi wowote.

Marekani inatoa msaada mkubwa wa kiuchumi kwa Israel. Tangu Vita vya Pili vya Dunia, imepokea msaada wa Marekani wenye thamani ya dola bilioni 158.

Kila mwaka inapokea misaada ya Marekani yenye thamani ya dola bilioni 3.8, ambayo ni takriban asilimia 16 ya bajeti yote ya ulinzi ya Israel. Leo Israel imekuwa msafirishaji wa kumi wa silaha na zana za kijeshi ulimwenguni.

Israel pia ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Marekani. Kuna biashara ya dola bilioni 50 kati ya nchi hizo mbili kila mwaka.

Tangu 1972, Marekani imekataa maazimio 50 yaliyoletwa dhidi ya Israeli katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Makundi ya ushawishi ya Israel

EFD

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken alipohudhuria mkutano wa AIPAC

Israel ina umuhimu wa kimkakati katika siasa za ulimwengu wa Kiarabu. Wakati wa Vita Baridi, Marekani iliitumia Israeli kama ngome muhimu dhidi ya ushawishi wa Umoja wa Kisovieti katika ulimwengu wa Kiarabu.

Baada ya Vita Baridi, Marekani ilizidi kujiweka Asia Magharibi na nchi ya Israel, Saudi Arabia na Misri zikawa washirika wake muhimu.

Maoni ya watu wa Marekani, siasa za wakati wa uchaguzi na makundi ya ushawishi - ni mambo yanyochangia sera ya Marekani inayoiunga mkono Israel.

Katika Bunge la Marekani, wabunge wengi wa vyama vya Republican na Democratic wanaunga mkono Israel. Makundi ya ushawishi kutoka jamii ya Wayahudi na Wakristo wote hufanya kazi kubwa kuhakikisha uungwaji mkono wa Israel katika siasa za Marekani.

Kundi moja la ushawishi lenye nguvu ni Kamati ya Masuala ya Israel na Marekani au AIPAC. Marais, Maseneta na Mawaziri Wakuu wa Israel na Marekani huhudhuria mikutano yake ya kila mwaka kama wageni.

Mashirika yanayounga mkono Israel hutoa usaidizi wa kifedha kwa vyama vya Republican na Democratic. 2020 mashirika hayo yalikusanya dola bilioni 30, asilimia 63 zilitolewa kwa Democratic na nyingine kwa wabunge wa Republican.

Je, kuna makundi ya ushawishi kwa Wapalestina?

EDFC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Katika miaka michache iliyopita, maseneta kama Bernie Sanders na Elizabeth Warren wa Chama cha Democratic wamejitokeza kama wafuasi wa Palestina.

Wote wawili walishiriki katika kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya kugombea urais 2020. Bernie na Warren wanasema misaada ya kiuchumi inayotolewa kwa Israel inapaswa kuwa na masharti ya kulinda haki za binadamu za Wapalestina.

Kizazi cha wanasiasa wachanga kama Alexandria Ocasio-Cortez, Ilhan Omar, Ayanna Presley na Rashida Taleb wameibuka kama sauti za Palestina katika Bunge la Marekani.

Katika miaka ya hivi karibuni, uungaji mkono wa Palestina umeongezeka miongoni mwa wa-Marekani. Kwa mujibu wa utafiti wa Gallup, asilimia 25 ya watu walioshiriki katika utafiti huo mwezi Februari mwaka huu walionesha kuunga mkono harakati za Palestina. Miaka mitano iliyopita ilikuwa asilimia 19.

Lakini sehemu kubwa ya umma wa Marekani bado wanaunga mkono Israel. Asilimia 58 ya Wamarekani waliohojiwa waliunga mkono Israel. Na asilimia 75 ya Wamarekani walitoa maoni mazuri juu ya Israel.