Hakuna kuongea, ua': Je shirika la kijasusi la Mossad linafanya nini Iran?

Februari 2, 2017, kundi la watu wasiojulikana walivunja milango ya ghala moja lililotelekezwa kwenye maeneo ya viwanda huko Tehran na kuvunja makufuli ya makasini 27 kwa muda wa chini ya saa 7 ili kuchukua maelfu ya ramani, hati na CD zilizo na taarifa za siri kuhusu mpango wa nyuklia wa Irani.
Miezi mitatu baada ya operesheni ya siri, nyaraka zilizoibiwa zilipatikana huko Tel Aviv, kilomita 2,000 kutoka Shurabad.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akionyesha vifuniko na masalia ya nyaraka na CD hizo na alisema ziliibiwa na mawakala wa Shirika la kijasusi la Mossad kutoka Tehran na kupelekwa Israeli.
Hata hivyo maafisa wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu iliyotuhumiwa waliita madai hayo kuwa uwongo na walighushi nyaraka, hata wakati wa uchaguzi wa urais, maafisa wa ngazi za juuu wa Irani akiwemo rais wa wakati huo Hassan Rouhani, alithibitisha wizi huo.
Kwa namna gani Mossad, waligundua sehemu hiyo ya kutunza nyaraka za siri kuhusu mpango wa nyuklia wa Irani na iliwezaje kuiba nyaraka hizi? Je! Jukumu la Shirika hili ni nini hasa kwenye mauaji ya watu na hujuma katika maeneo nyeti ya Irani.
Kupata majibu ya maswali haya na kuichunguza moja ya taasisi kubwa duniani Mossad , BBC ilisafiri mpaka Tel Aviv, mji mkuu wa Israel, yalipo makao ya jeshi la Israel na masuala yote ya kijasusi na ulinzi yanaratibiwa pale.
'Hakuna kuongea, ua'
Shughuli za Mossad ni za siri sana kiasi kwamba hata makao makuu yake yanayoendesha shughuli zake hayajulikani. Hadhi ya Mossad ni ya kimya kimya na za siri hata zile shughuli zake zenye mafanikio ni operesheni ya kumuondoa Mohsen Fakhrizadeh, mtu aliyekuwa nyuma ya mpango wa nyuklia wa Irani, ambaye aliuawa karibu na Tehran, na hakuna ofisa yeyote wa juu aliyethibitisha kwamba Israel imehusika.
Kwenye mahojiano na BBC, waziri wa ulinzi wa Israeli Benny Gantz alikataa kuzungumzia kuhusu mauaji hayo, alisema: "Israeli ina moja ya mifumo mizuri zaidi ya ujasusi na ulinzi ulimwenguni na inafanya kila iwezalo kujilinda na "Inatumia njia tofauti."

Chanzo cha picha, Getty Images
Norman Roll, Afisa wa zamani wa CIA katika mashariki ya kati, aliiambia BBC kwamba Israel kufikia nyaraka za siri za mpango wa nyuklia wa Iran ilikuwa moja ya "shughuli za ujasusi zilizofanikiwa zaidi katika historia ya kisasa. "Kulingana na yeye, hati hizi zilithibitisha kwamba Iran ilikusudia kutengeneza silaha za nyuklia na ina uwezo huo.
Nchini Israel, BBC ilipata hati kadhaa zilizoibiwa. BBC haikuweza kuthibitisha ukweli wa hati hizi, lakini hati hizi zilikuwa na taratibu za kiutawala za Irani na ziliainishwa. Katika hati hizi, inashauriwa vituo vya nyuklia kuanzishwa.
Mwishoni mwa mwaka 2017, mawakala wa Mossad nchini Iran waliripoti kwa Tel Aviv kwamba nyaraka za mpango wa nyuklia wa Iran zimehamishiwa kwenye ghala lingine nje kidogo ya Tehran.
Kwa mujibu wa mwandishi mwandamizi anayefuatilia masuala ya Mossad, Ronen Bergman, makasiki yenye urefu wa mita mbili na nusu yametengenezwa na kampuni moja huko Tehran. Walichukua mfano wa makasiki mawili na kupeleka Uingereza. Mwandishi huyo anasema kwamba maafisa wa Mossad waligundua kwamba kukiwa na joto la nyuzi joto 3,500, linaweza kufungua kasiki kwa dakika saba.
Makamanda waliogeuka majasusi wapelelezi

Chanzo cha picha, IRAN MEDIA
Maafisa wengi wa zamani wa Irani wanaamini kwamba wakala wa kijasusi wa Israeli wana ushawishi mkubwa kwenye masuala ya usalama na ulinzi. Mahmoud Ahmadinejad, Rais wa Iran miezi kadhaa iliyopita, alisema kwamba mashtaka makubwa zaidi dhidi ya Israeli katika Wizara ya Habari, ni kwamba yeye ni mpelelezi wa Israeli.
Ali Younesi, waziri wa zamani wa ujasusi wa Irani, hivi karibuni alionya ushawishi wa Mossad katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kwamba "maafisa wote wa Jamhuri ya Kiislamu wanapaswa kujali maisha yao wenyewe."
BBC imekuwa ikiwasiliana na baadhi ya maafisa kwenye upande wa usalama kwenye gereza la Evin, ambaye anasema, kuna makamanda wa usalama na jeshi wa Irani wakiwemo wa Revolutionary Guards na Quds Force, wako jela. Wanatuhumiwa kwa kutumwa na nchi za kigeni hasa Israel kuipeleleza Irani.
Kivuli cha vita
Katika miaka ya hivi karibuni, huduma za kiintelijensia za Iran zimekuwa zikivutia watu nchini humo. Katikati ya miaka ya 1990's Gonen Segev waziri wa nishati na miundo mbinu aliwekwa jela kwa miaka 11, akituhumiwa kusafiri kwenda Tehran mara kadhaa kwa ajili ya kuipepeleza, akidaiwa kutumwa na Israel.
Ronen Bergman anasema vita katika karne ya 21 "sio tena mapambano kwa kutumia vifaru na makambi ya majeshi. Hiyo ndio vita. Iran na Israel wanahusika katika vita vikali vya kutawala na ushawishi katika eneo hilo la mashariki ya Kati."
Afisa wa zamani wa CIA Norman Roll pia anaamini kwamba vita vya Iran-Israel sio tena ya kificho au vita ya kivuli, vita ya nyuma ya pazia. Waisrael wanasema watatumia njia yoyote wanayoona inafaa kuzuia nchi hiyo ya Kiislamu kuwa na mabomu ya nyuklia. Kwa Iran, kukabiliana na Israeli ni mapambano ya kiitikadi na vita kuu katika Mashariki ya Kati .














