Ndege isiyokuwa na rubani ya Hezbollah iliyotumwa Palestina yazua mjadala Israel

,m

Ijumaa iliyopita, kundi la kiislamu la Hezbollah lilituma ndege ndogo isiyo na rubani kwenye maeneo yaliyo ndani ya mpaka wa Palestina.

Taarifa kutoka Hezbollah zilizua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kati ya wale wanaoliunga mkono kundi hilo na wale wanalolipinga.

'Ndege hizo zilirandaranda kwenye maeneo ya Palestina kwa dakika 40 na ilikuwa katika operesheni maalumu," alisema taarifa kutoka Hezbollah.

Taarifa hiyo ilisema kuwa "operesheni ilifanmyika kilometa 70 ndani mipaka ya Palestina.

Taarifa hiyo iliendelea kusema, "licha ya majaribio ya mara kadhaa ya mashambulizi ya mara kwa mara ya adui kuzidondosha ndege hizo, ndege hiyo ilirudi salama ilipotoka.

Akizungumzia taarifa hiyo kutoka Hezbolaah, msemaji wa jeshi wa Israel Avichai Adraee alituma ujumbe wa twitter akisema: "Uchunguzi wa awali uliofanywa leo, unaonyesha ndege ndogo isiyokuwa na rubani imeonekana Lebanon." Tunafuatilia hali hiyo".

m

Aliongeza, "Kombora limerushwa kutoka kwa mfumo wa ulinzi wa makombora ambao haukuweza kuingiliwa na ndege hiyo, na kifaa kikingine cha onyo kilitumwa hewani. Dakika chache baadaye ndege hiyo alirudi Lebanon na hali ilikuwa shwari," alisema.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, siku ya Ijumaa jeshi la Israel lilidungua ndege isiyo na abiria ya Hezbollah.

Wafuasi wa Hezbollah

Wafuasi wa kundi la Hezbollah wamekuwa wakipaza sauti kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ndege hiyo isiyokuwa na rubani inayoitwa "hassan", wakiisifu wakati ilipokuwa inarejea salama Lebanon.

Ghassan Jawad, mchambuzi wa masuala ya kisiasa aliye karibu na Hezbollah, alizungumzia suala hilo na kusema: "makomnbora ya Lebanon na silaha zingine ni mfano. Serikali hii inaweza kufanya nini kufanikiwa? Hezbollah wamekuwa wakipewa sifa na wengi kwa kuzipa majina ndege zake hizo ndogo zisizo na rubani.

Hassan Al la Qeys ni nani?

Hassan al-Qays, mmoja wa makamanda mbele aya nyumba yake huko Beirut mwaka 2013.

Al Laqeys alijulikana kama mmoja wa watu muhimu wa operesheni za Hezbollah, akiwa na jukumu la kusimamia ndege hizo zisizo na rubani.

Wasioiunga mkono Hezbollah

Wakati huo huo, wengi wanakosoa hatua hiyo ya Hezbollah ya kutuma ndege zake zisizo na rubani Israel, wakiliona kundi hili ni kama "linacheza na moto na tishio linalotokana na ndege za kivita za Israel mjini Beirut'.

Ndege zisizo na rubani za Hezbollah

m

Katibu mkuu wa kundi la Hezbollah nchini Lebanon, Hassan Nasrallah, alitangaza siku ya Jumatano kwamba kundi hilo "limeanza kutengeneza ndege zisizo na rubani kwa muda sasa."

Nasrallah alisema: "Tuna uwezo wa kubadilisha maelfu ya makombora yetu kuwa makombora halisi na yenye nguvu. Tulianza miaka iliyopita na kubadilisha idadi kubwa yao kuwa yenye nguvu. Hatuna haja ya kuyahamisha." kwa upande wa Iran".

Unaweza kusoma zaidi: