Mwanamgambo wa Hezbollah Salim Ayyash afungwa maisha kwa kumuua Hariri

Salim Jamil Ayyash

Chanzo cha picha, Special Tribunal for Lebanon

Maelezo ya picha, Salim Ayyashmpaka sasa hajulikani aliko

Mwanamgambo wa kundi la Hezbollah amehukumiwa vifungo vitano jela bela kuwepo mahakamani kwa kumuua Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.

Alipatikana na makpsa mapema mwaka huu kwa kuhusika na mauaji hayo.

Majaji katika mahakama maalum ya Lebanon iliyo na makao yake nchini Uholanzi (STL) wamesema Salim Ayyash alikuwa kiungo muhimu katika shambulio la bomu la Beirut mwaka 2005 lililomuua Hariri.

Waliwaondolea mashtaka wastakiwa wengine watatu, ambao kama Ayyash walishtakiwa bila kufika mahakamani.

Hezbollah imepinga kuhusika na kivyovyote na shambulio hilo, na majaji wamesema hakuna ushahidi unaohusisha viongozi wa kundi hilo la wanamgambo wa Kishia.

Mahakama hiyo maalum pia ilimpata Salim Ayyash na kosa la mauaji. Rafiq Hariri aliuawa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga miaka 15 iliyopita.

Kesi hiyo ilihusu nini?

Rafik Hariri, ambaye alikuwa wa dhehebu la Kiislamu la Sunni, alikuwa bilionea na mfanyabiashara aliyehudumu kama Waziri Mkuu wa Lebanon mara tano kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 1975hadi miaka ya 1990.

Muhula wake wa mwisho madarakani ulimalizika mwaka 2004, na baada ya hapo aliungana na upinzani bungeni na kuunga mkono wito wa kutaka Syria kuondoa vikosi vyake, ambavyo vilikuwa nchini Lebanon tangu mwaka 1976.

Rafik Hariri akiwa na mke wake, Nazek (Sept 2000)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hariri, billionea na mfanyabiashara, alitoa wito kwa Syria kuondoa vikosi vyake Lebanon

Asubuhi ya Februari 14 mwaka 2005, Hariri alikuwa katika msafara uliopita Hoteli ya St George katikati ya Beirut wakati bomu lililokuwa limefichwa ndani ya gari kulipuka.

Mauaji hayo yalifanya maelfu ya watu kuandamana dhidi ya serikali iliyokuwa inaunga mkono Syria, kidole cha lawama kikielekezea majirani hao wa Lebanon wenye ushawishi mkubwa.

Serikali ilijiuzulu wiki mbili baadaye na vikosi vya Syria kuondoka nchini humo mwezi AprilI.

Pro-Hariri protest in Beirut (07/03/05)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mauaji ya Hariri yaliibua maandamano makubwa dhidi ya serikali mjini Beirut

Baada ya kupata ushahidi, Umoja wa Mataifa na Lebanon zilibuni mahakama maalum ya STL mwaka 2007 kuchunguza shambulio hilo, hatimaye washukiwa wanne wakashtakiwa bila kuwepo.

Mawendesha mashtaka walijiridhisha na uchanguzi wa mawasiliano ya simu ya mkononi iliyosadikiwa kutumiwa kupanga, kuandaa na kutekeleza shambulio hilo.

Mchunguzi wa Lebanon ambaye alianza mapema kufuatilia data za simu alipata mafanikio ya mapema Wissam Eid, aliuawa mjini Beirut mwaka 2008.