Israel yadai kusambaratisha mtandao wa kijasusi wa Iran uliowasajili wanawake kuipeleleza

Picha ya profile ya "Rambod Namdar",ambaye ametambuliwa kama mfanyakazi wa kijasusi wa Iran na maafisa wa usalama wa Shin Bet wa Israel

Chanzo cha picha, Facebook

Maelezo ya picha, Mshikaji huyo wa Iran, aliyejiita Rambod Namdar, anadaiwa kuwafuata wanawake hao kwenye Facebook

Shirika la Israel la usalama wa ndani limewakamata Waisrael watano wanaotuhumiwa kufanyia ujasusi hasimu wao mkuu Iran.

Tukio hilo linajumuisha wanawake wanne wa Kiyahudi wenye asili ya Iran, ambao Shin Bet inasema walisajiliwa na mhudumu anayedai kuwa mwanaume wa Kiyahudi anayeishi nchini Iran.

Wanawake hao wanadaiwa kulipwa maelfu ya dola kupiga picha maeneo nyeti na kufuatilia mipangilio wa usalama,na kujenga uhusiano na wanasiasa.

Mawakili wa wanawake hao wanasema hawakujua mtu huyo alikuwa jasusu wa Iran.

Pia walisisitiza kuwa wanawake hao hawakua na nia ya kudhuru usalama wa Israel.

Lakini Shin Bet ilisema kuna "njama kubwa" ambapo kulikuwa na mpango wakuunda mtandao wa ujasusi wa Iran ndani ya Israel, na kwamba wanawake hao wanakabiliwa "mashtaka makali".

Mhudumu wa Iran,aliyejiita Rambod Namdar, alidaiwa kuwaendea wanawake hao kwenye Facebook na kisha kuendelea kuwasiliana nao kwa miaka kadhaa kupitia huduma ya utumaji ujumbe uliofichwa ya WhatsApp.

"Licha ya kwamba wanawake hao walishuku kuwa mwanamume anayehusika alikuwa mfanyakazi wa ujasusi wa Iran, baadhi yao waliendelea kuwasiliana naye, walikubali kufanya kazi mbalimbali alizowaomba wamfanyie na kupokea pesa kutoka kwake," Shin Bet alisema.

Kwa mujibu wa shirika hilo, mwanamke mwenye umri wa miaka 40 kutoka kitongoji cha el Aviv huko Holon alikubali kupiga picha za ubalozi wa Marekani amao bado ulikuwa mjini humo, pamoja na mambo ya ndani ya majengo ya wizara ya mambo ya ndani na masuala ya kijamii ya Israel pamoja na kituo cha kibiashara.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 57 kutoka mji wa Beit Shemesh anadaiwa kumhimiza mwanawe kuhudumu katika ujasusi wa kijeshi pia na kupitisha hati za kijeshi zake.

Mhudumu huyo pia alimuomba mmoja wa wanawake hao kuwashawishi mwanawe wa kiume kujiunga na jeshi la intelijensia la Israel wakati wa utumishi wake wa lazima wa kijeshi, ilisema.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 57 kutoka mji wa Beit Shemesh anadaiwa kumhimiza mwanawe kuhudumu katika ujasusi wa kijeshi pia na kupeana hati zake za kijeshi.

Mwanamke huyo aliagizwa kuanzisha klabu kwa ajili ya Waisraeli wenye asili ya Iran kukusanya taarifa zao za kibinafsi, na kujaribu kuwa marafiki wa karibu na mbunge wa kike wa bunge la Israel, kulingana na Shin Bet.

Pia inasemekana aliweka kamera iliyofichwa kwenye chumba cha kukanda watu nyumbani kwake, ili kukusanya picha zinazoweza kuwaaibisha wateja wake.

"Taifa la Israel liko katika oaresheni inayoendelea na Iran. Ni wazi: tunaona juhudi zisizoisha na majaribio ya Jeshi la Ulinzi wa Iran kuwaajiri raia wa Israel," Waziri Mkuu Naftali Bennett alisema.

"Majaribio haya yanaenda zaidi ya usalama na kijasusi; yanapanuka kwa juhudi za kushawishi raia wa Israeli na jamii ya Israeli, kuzua mifarakano na ubaguzi, kudhoofisha utulivu wa kisiasa nchini Israeli na kuharibu imani ya umma kwa serikali," aliongeza.