Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Man United yamlenga kiungo wa Atalanta na Brazil Ederson

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United inamchunguza Ederson wa Atalanta, 25, na kiungo huyo wa kati wa Brazil ni mmoja wa wachezaji wachache ambao klabu hiyo inazingatia sana kusaini kwa nafasi hiyo. (Florian Plettenberg)
West Ham, Leicester City na Southampton wanaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20 kutoka Brighton. (Givemesport)
Southampton wanaweza kumuuza mchezaji wao chipukizi Tyler Dibling, 18, ikiwa watashuka daraja kutoka Ligi ya Premia, huku Manchester United na Newcastle zikiwa na nia ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Uingereza. (Football Insider)
Uvumi kwamba kiungo wa zamani wa Manchester United na Juventus Paul Pogba, 31, alikuwa ameonekana kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester City haukuwa wa kweli. (Fabrizio Romano),
West Ham, Fulham, na Crystal Palace wote wanamfuatilia kiungo wa Juventus Nicolo Fagioli, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 23 ameivutia Tottenham hapo awali na huenda akapendelea kujiunga na klabu hiyo. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wanafikiria uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21. (TeamTalks)
Hapo awali Arsenal walifanya mazungumzo kuhusu kutaka kumnunua Sesko na kubaki na nia ya kumnunua mchezaji huyo ambaye ameanzisha uhusiano mzuri na wawakilishi wake. (Mail Plus - Subscription Required)
Bosi wa West Brom Carlos Corberan na meneja wa zamani wa Denmark Kasper Hjulmand ni miongoni mwa wagombea kuchukua nafasi ya Russell Martin huko Southampton, lakini bosi wa muda Simon Rusk atasalia kuinoa kwa safari ya Jumapili ya Fulham. (Sky Sports),
Klabu ya Saudi Pro League, Al-Shabab inavutiwa na dili la bei iliyopunguzwa kwa mlinda lango wa Newcastle Slovakia Martin Dubravka, 35. (I),
Wolves wanaweza kulenga uhamisho wa Januari kwa mlinzi wa kati wa Austria Kevin Danso, 26, ambaye Lens inaweza kutaka kumuuza. (L'Equipe - in French)
Kiungo mshambuliaji wa Monaco Mfaransa Maghnes Akliouche, 22, alisema angependa kuichezea Barcelona katika maisha yake ya soka. (Sport - In Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa Arsenal Reiss Nelson - ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Fulham - ataruhusiwa kuondoka The Gunners msimu ujao kwa kuwa kuna uwezekano mchezaji huyo wa miaka 25 hatokuwa sehemu kubwa ya mipango ya Mikel Arteta katika siku zijazo. (Mail Plus - Subscription Required)
Bosi wa zamani wa Coventry Mark Robins amekataa fursa ya kuzungumza na klabu nyingine ya Championship Millwall kuhusu nafasi yao ya umeneja. (South London Press)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












