'Maisha yangu yalitatizika baada ya kaka yangu kumuua baba yetu'

za

Chanzo cha picha, STEVE HUNTLEY/BBC

Maelezo ya picha, Karen Cooper dada wa Gary
    • Author, Phil Shepka
    • Nafasi, BBC

Maisha ya Karen Cooper "yalitatizika siku kaka yake Gary alipomuua baba yao na kumshambulia mama yao. Miaka mitano sasa imepita.

Machi 2019, Karen alioka keki ili kusherehekea siku ya kuzaliwa ya baba yake Hedley Robinson. Watu wa familia walikuwa wanakusanyika kusherehekea kutimiza miaka 86.

Siku iliyofuata, Margarete mama wa Karen alipiga simu polisi - kwa sababu mwanawe Gary alikuwa "akifanya vurugu ndani ya nyumba."

Alikamatwa, akapelekwa hospitali na baadaye kurudishwa kituo cha polisi. Gary alionekana hafai kuzuiliwa chini ya kifungu cha 136 cha Sheria ya Afya ya Akili, sheria inayowataka polisi kuwapeleka watu wa aina hiyo mahali salama.

Baada ya wakili kubaini kuwa hafai kwa mahojiano. Polisi hawakuwa na chaguo ila kumwachilia huku wakiendelea na uchunguzi.

Siku ya Tukio

sd

Chanzo cha picha, KAREN COOPER

Maelezo ya picha, Gary Robinson, Margarete Robinson, Karen Cooper na mume wake na Hedley Robinson siku ya harusi ya Karen

Dakika kumi tu baada ya polisi kuondoka tangu walipomfikisha nyumbani kwao, Gary aliwashambulia wazazi wake kwa kisu.

Baba wa Karen alifanyiwa upasuaji na mama yake alilazwa katika kitanda cha dharura, akiwa amedungwa kisu kwenye koo.

Margarete alinusurika - lakini madaktari hawakuweza kumwokoa Hedley, alifariki wiki tatu baadaye.

Agosti mwaka huo Gary alilazwa hospitali baada ya kukubali mauaji na na jaribio la kuua. Madaktari wa magonjwa ya akili walikubali kwamba alikuwa akiugua ugonjwa huo.

Karen anaamini kwamba mengi zaidi yangefanywa kuzuia shambulio hilo. "Wangemtenga kaka yangu siku hiyo na kumweka kwenye kituo au hata kumweka kizuizini kwa saa nyingine 24," anasema.

Maisha yamebadilika

sr4e

Chanzo cha picha, STEVE HUNTLEY/BBC

Maelezo ya picha, Karen Cooper akitolewa na baba yake siku ya harusi yake

Karen anasema imekuwa kama kifungo cha maisha kwa familia yake, ambayo maisha yao "yametatizika mara moja," na mustakabali wao "umebadilika.’’

“Ndugu yangu anapata msaada, amelazwa katika hospitali ya matatizo ya akili. Hivyo mahitaji yake yote yanatimizwa na anahudumiwa.

"Mimi na familia yangu? Hakuna mtu anayeshughulika nasi."

Karen, ambaye aliuza biashara yake ya zaidi ya miaka 20 baada ya kuhisi hawezi kufanya kazi baada ya shambulio hilo, anaamini familia kama yake zinapaswa kupatiwa wataalamu, washauri na usaidizi wa kisheria.

Maboresho

qwas

Chanzo cha picha, KAREN COOPER

Maelezo ya picha, Hedley Robinson alishiriki vita vya Korea
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika uchunguzi wa kesi ya babake, polisi ilisema kwa sababu tukio hilo - imebadilisha jinsi inavyoshughulikia watu wenye matatizo ya afya ya akili na imeboresha mafunzo.

Afisa Mkuu wa polisi Konstebo Katy Barrow-Grint anadokeza kwamba wakati Gary Robinson alipoachiliwa kutoka kizuizini hapakuwa na sababu ya kushuku angejidhuru yeye au wazazi wake.

“Pia iligundulika kuwa maombi kadhaa yasiyo rasmi ya kutathminiwa upya afya ya akili ya Gary Robinson yalitolewa kwa wataalamu wa afya ya akili, lakini yalikataliwa."

Maboresho yalifanywa katika upashanaji habari ili maafisa "waweze kuhakikisha kwamba wana taarifa zote muhimu kuhusu historia ya mgonjwa kabla ya kulazwa".

"Milango yetu iko wazi kutoa msaada baada ya matukio ya kusikitisha kama haya na tungehimiza mtu yeyote aliyeathiriwa na matukio haya na anahisi kuhitaji msaada kuwasiliana nasi."

Kujibu mwito wa Karen wa msaada ziada kwa familia, Wizara ya Sheria ilisema serikali "inaongeza ufadhili mara nne kwa huduma za wagonjwa wa aina hii na mswada wa waathiriwa unapanuliwa ili kujumuisha familia zilizofiwa kama yake ili wapate msaada kamili wanaostahili."

“Changamoto ni kuwa yeye ni kaka yangu na ninampenda,’’ Karen anasema.

"Yeye ni kaka yangu mdogo, na wakati huo huo alifanya shambulio la kutisha na baya kwa wazazi wangu na kumuua baba yangu."