Je, ni matatizo gani ya kiafya yanayowakabili wanaume wakati wake zao wanapojifungua

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu wengi hufikiri kwamba huzuni baada ya kujifungua au wasiwasi ni hali ambayo huathiri wanawake pekee. Lakini kwa kweli, hali hii pia huwaathiri wanaume na tafiti zingine zinakadiria kuwa hutokea miongoni mwa 10% ya akina baba.
Kuna sababu nyingi za huzuni baada ya kujifungua kwa wanaume kinyume na mabadiliko ya homoni pekee.
Hata kwa wanawake, homoni huchangia kwa kiasi kidogo katika huzuni unayoipata baada ya kijifungua.
Kawaida hali hii hutokana na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa usingizi baada ya kuzaliwa kwa mtoto, ukosefu wa msaada, au matatizo ya kifedha.
Na hii inaweza kutokea kwa mtu katika umri wowote. Dalili za huzuni baada ya kujifungua ni sawa na huzuni ya kawaida.
Dalili zinaweza kuwa kwamba mtu huhisi kukosa motisha, kukosa usingizi, na kujihisi hana thamani, kukosa umakini, mabadiliko ya hamu ya kula au kupungua uzito au kuongezeka, na pia kufikiria kujiua.
Tofauti kuu kati ya unyonge wa kawaida na unyonge wa baada ya kujifungua ni kwamba ungonge wa kawaida unaweza kutokea wakati wowote baada ya kujifungua hutokea baada ya mtoto kuzaliwa. Ni kawaida kuhangaika na afya ya akili kidogo baada ya mtoto kuzaliwa.
Ni vyema kutambua kwamba hali hii inayojitokeza baada ya kujifungua inaweza kutokea wakati wowote baada ya mtoto kufika mwaka wa kwanza au miwili baada ya kujifungua, si tu katika miezi michache ya kwanza.
Kwa hiyo, ikiwa unahisi kuwa unakabiliwa na hali hii baada ya kujifungua, ni muhimu kutafuta msaada, si tu kwa afya yako, lakini pia inaweza kuathiri uhusiano wako na mtoto wako.
Unahitaji kutafuta msaada kutoka kwa marafiki, familia au daktari wako.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Miongoni mwa mabadiliko ambayo yanaweza kukujia ni hasira nyingi. Wanaume wanaopambana na afya zao za akili wana hasira sana.
Ili kukabiliana na hasira hiyo, kuwa mtulivu na mvumilivu. Jaribu kuachilia; Hii inaweza kukusaidia kujisikia vizuri zaidi kuzungumza juu ya hisia zako.
Pia angalia unapozungumza kuhusu matatizo yako na unashiriki na nani.
Kwa mfano, baadhi ya watu wanaweza kuona ni rahisi kuzungumza kwenye mitandao ya kijamii au katika vikundi kwenye vifaa vya intaneti jambo ambalo linaweza kukufanya ujisikie vibaya zaidi na kuwa na matatizo. Ni rahisi na bora kupata programu ya afya ya akili.
Baadhi ya watu wanaona ni rahisi kutumia hii kuuliza maswali, kutafuta suluhu, na kuzungumza kuhusu hisia zao.
Kuna baadhi ya nyenzo ambazo ambazo zinaweza kukusaidia kukabiliana na uzazi.
Huzuni wa baada ya kujifungua kwa wazazi ni kweli, na ni muhimu.
Kwa bahati nzuri, ikilinganishwa na miaka michache iliyopita, kuna ufahamu zaidi na msaada wa kukabiliana nao kuliko hapo awali.















