Tetesi za Soka Ulaya Jamamosi 23.11.2024

Muda wa kusoma: Dakika 3

Chelsea wanataka kumsajili Liam Delap wa Ipswich, Liverpool na Arsenal mbioni kumsaka Martin Zubimendi wa Real Sociedad, na hatma ya Joshua Zirkzee Manchester United ipo shakani.

Mshambuliaji wa Ipswich Muingereza Liam Delap, 21, anasakwa na Chelsea baada ya klabu hiyo kusitisha mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Newcastle na Uswidi Alexander Isak, 25. (I - usajili unahitajika)

Arsenal, huenda wakajaribu kumshawishi Isak kuhamia Uwanja wa Emirates mwezi Januari kwa ofa ya kucheza Ligi ya Mabingwa. (Give Me Sport)

Mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku hana furaha kutokana na kukosa muda wa kuchezea Chelsea lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hana mpango wa kuondoka Stamford Bridge kwa sasa. (Athletic-Usajili unahitajika)

Liverpool wanatarajiwa kufanya jaribio la pili la kumnunua kiungo wa Real Sociedad Martin Zubimendi, 25, mwezi Januari lakini watakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania. (Team Talk)

Newcastle wanawafuatilia mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Rayan Cherki, 21, na mchezaji wa kimataifa wa Canada Jonathan David David wa Lille, 24 wakati wakitathmini uwezekano wa kumnunua kiungo mshambuliaji mwezi Januari. (The I -usajili unahitajika)

Wakuu wa Manchester United wana mashaka na mchezo wa mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 23, tangu alipomnunua kwa £36.5m kutoka Bologna msimu wa joto. (Manchester Evening News)

Tottenham wana matumaini ya kuwashinda Manchester United na Newcastle mbio za kumsaini ya kiungo wa kati wa Lille na Uingereza Angel Gomes, 24. (GiveMeSport)

Winga wa Uhispania Lamine Yamal, 17, amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka sita katika klabu ya Barcelona atakapofikisha umri wa miaka 18. (El Chiringuito TV, via Football Espana)

Kocha mkuu wa Sunderland Regis Le Bris anataka viungo wa kati wa Uingereza Jobe Bellingham, 19, na Chris Rigg, 17, kusalia katika Stadium Of Light ili kuendeleza fani yao ya soka huku klabu kadhaa za Ligi ya Premia zikiwanyatia. (Sunderland Echo)

Galatasaray wanamfuatilia mlinda lango wa Liverpool na Brazil Alisson Becker, 32, huku wakimtafuta atakayechukua nafasi ya Fernando Muslera, 38, wa Uruguay, mwishoni mwa msimu huu. (Sabah - kwa Kituruki)

Manchester City wameelekeza darubini yao kwa winga wa Sporting na Uruguay Maximiliano Araujo, 24. (Football Insider)

Newcastle wako katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Algeria Ibrahim Maza, 18, baada ya Hertha Berlin kupunguza bei yake hadi euro milioni 20. (Caught Offside)

Tottenham wanatazamiwa kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Atletico Madrid kumnunua kiungo wa Real Betis na Marekani Johnny Cardoso, 23. (Estadio Deportivo - kwa Kihispania)

Mlinzi wa Slovakia Milan Skriniar, 29, anataka kuondoka Paris St-Germain mwezi Januari baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, huku klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England zikifuatilia hali yake. Juventus na Napoli pia wanamtaka. (Le Parisien - kwa Kifaransa)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi