Uingereza, Ufaransa au Ureno...nani atashinda kombe la Euro?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mikwaju ya penalti ndiyo iliyoizuia England kushinda ubingwa wa Uropa mwaka 2021.
Baada ya kuvumilia kichapo kichungu kutoka kwa Itali kwenye fainali zilizochezwa katika uwanja wa Wembley, ilikuwa vigumu kujiuliza ikiwa miamba ya The Three Lions walikuwa wametupilia mbali fursa yao bora zaidi ya mafanikio ya michuano mikubwa.
Lakini labda sivyo.
Kulingana na utabiri wa Opta kabla ya michuano ya Euro 2024, dirisha la ushindi bado liko wazi kwa upande wa Gareth Southgate…
Ni vigumu kwa England kuelekea kwenye michuano mikubwa ya kimataifa wakiwa na uwezo mkubwa wa kuibuka washindi, lakini ndivyo hali ilivyo wakati huu kulingana na utabiri wa Opta.
Kikosi cha Southgate ndicho kinaongoza kundi la washindi watarajiwa, wakiwa na nafasi ya 19.9% ya kutwaa kombe hilo nchini Ujerumani.
Ingawa habari hii bila shaka itakaribishwa kwa uchangamfu na wengi, pengine sasa unashangaa ni kwa jinsi gani tumefikia matokeo hayo… na iwapo ni swali la haki.
Ili kupata picha kamili ya nani atashinda shindano hili, muundo wa ubashiri wa Opta unakadiria uwezekano wa kila matokeo ya mechi - kushinda, sare au kushindwa - kwa kutumia uwezekano wa soko la kamari na orodha ya timu zetu wenyewe.
Viwango hivyo vinatokana na uchezaji wa kihistoria na wa hivi majuzi wa timu, huku mtindo ukizingatia nguvu ya wapinzani na ugumu wa njia yao ya kufika fainali kwa kutumia uwezekano wa matokeo ya mechi, muundo wa vikundi na hatua ya muondoano.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati utabiri wa Opta ukiiweka England katika nafasi ya kwanza, ni Ufaransa - timu iliyowaondoa kwenye Kombe la Dunia la 2022 – ndio wanaopigiwa upatu kushinda kombe hilo kwa kiwango cha
Ikiwa na nafasi ya 19.1% kwa kikosi cha Didier Deschamps kushinda Euro 2024, kuna uwezekano mkubwa ya wawili hao kukutana kwenye fainali.
Kwa hakika, Opta inakadiria kuwa timu zote mbili zina takriban nafasi moja kati ya mbili za kutinga nusu fainali, huku Uingereza ikiwa na 48.2% na Ufaransa 48.1% mtawalia, kuwa kati yatimu nne bora.
Zaidi ya hao, wenyeji Ujerumani ndio timu inayomaliza tatu bora kwa wawaniaji hao.
Kikosi cha Julian Nagelsmann kina nafasi ya 12.4% ya kuwa washindi nyumbani, na ni timu ya mwisho kati ya timu hizo tatu kuwa na uwezekano wa zaidi ya 10% kunyakua kombe.
Kwa wale ambao wanaonekana kuwa na uhakika zaidi kuwika katika hatua ya mtoano, England, Ufaransa, Ujerumani, Uhispania na Ureno ndizo timu tano zinazopewa 50% au nafasi nzuri zaidi ya kutinga angalau robo fainali.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwengineko kwa mtazamo wa Uingereza, timu ya taifa la Uskochi haionekani kuwa na matumaini ya kupiga hatua.
Vijana wa Steve Clarke watalazimika kutumia kila mbinu kufuzu katika Kundi A, ambalo linaonekana kuwa moja ya makundi yenye ushindani mkali katika mashindano hayo kwa ujumla.
Kulingana na mtabiri, Uskochi ina nafasi ya 58.9% ya kufika hatua ya 16 bora, iwe ni kumaliza katika nafasi mbili za juu au kama moja ya timu bora zilizomaliza nafasi ya tatu.
Tatizo kubwa kwao ni kwamba, pamoja na timu zinazopendwa zaidi za Kundi A, Ujerumani, Uswizi (61%) na Hungary (59.3%) ziko katika nafasi sawa za kufuzu kwa hatua ya mtoano.
Ushindani utakuwa mkali kwa Jeshi la Tartan, na mambo yatakuwa magumu kuanzia mwanzo huku mchuano wao na wenyeji Ujerumani ukianza Juni 14.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












