Je, umri gani ni sahihi wa kumpatia simu mtoto wako?

yyy

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kujadili ni programu gani watoto wanaweza kuwa nazo na jinsi wanavyotumia simu zao kunaweza kuwaruhusu wazazi kuunga mkono matumizi ya simu ya mtoto wao

Simu janja zimekuwa kitu cha kawaida miongoni mwa watoto, huku hadi 91% ya watoto wa miaka 11 wakimiliki simu. Lakini je, watoto wanapata faida gani?

Je, unapaswa kumpa mtoto wako simu janja, au kumweka mbali na vifaa hivo kadri iwezekanavyo?

Kama mzazi, unasamehewa kwa kufikiria simu janja kama aina ya kisanduku cha Pandora chenye uwezo wa kuachilia maovu yote ya ulimwengu kwenye maisha mazuri ya mtoto wako.

Vichwa vya habari vingi vya kutatanisha vinavyohusiana na athari inayoweza kusababishwa na matumizi ya simu za watoto na mitandao ya kijamii vinatosha kumfanya mtu yeyote kutaka kujiondoa.

Inavyoonekana, hata watu mashuhuri hawana kinga dhidi ya tatizo hili la ulezi wa kisasa: Madonna amesema kwamba alijuta kuwapa watoto wake wakubwa simu wakiwa na umri wa miaka 13, na hatofanya hivyo tena.

Kwa upande mwingine, labda una simu ambayo unaichukulia kama nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku -kuanzia kusoma barua pepe na manunuzi ya mtandaoni, hadi simu za video na albamu za picha za familia. Na ikiwa wanafunzi na marafiki wa mtoto wako wote wana simu, je, watakosa vitu muhimu bila kuwa simu?

Bado kuna maswali mengi ambayo hayajajibiwa kuhusu athari za muda mrefu za simu janja na mitandao ya kijamii kwa watoto na vijana, lakini utafiti uliopo unatoa ushahidi fulani kuhusu hatari na manufaa yake.

Wataalam wanakubaliana juu ya mambo kadhaa muhimu ya kuzingatia unapoamua ikiwa mtoto wako yuko tayari kutumia simu janja na unachopaswa kufanya akishaimiliki.

yyy

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ushahidi kuhusu wakati unaofaa wa kumpa mtoto simu janja ni mbaya, lakini kuna nyakati muhimu ambapo hatari ni kubwa zaidi.

Candice Odgers, profesa wa sayansi ya saikolojia katika Chuo Kikuu cha California, Irvine, nchini Marekani alichanganua kuangalia uhusiano kati ya matumizi ya teknolojia ya digitili na afya ya akili ya watoto na vijana, pamoja na tafiti zingine kubwa hakupata uhusiano thabiti kati ya matumizi ya teknolojia ya vijana na ustawi wao.

"Tafiti nyingi hazioni uhusiano kati ya matumizi ya mitandao ya kijamii na afya ya akili," anasema Odgers. Ukubwa wa athari chanya na hasi zilikuwa ndogo.

"Ugunduzi mkubwa zaidi ulikuwa utengano kati ya kile watu wanaamini, ikiwa ni pamoja na vijana wenyewe, na kile ambacho ushahidi unasema," anasema.

yyy

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakati wa janga la corona simu janja zilitoa njia muhimu kwa watoto kupata masomo mtandaoni wakiwa nyumbani
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa upande mwingine, kwa baadhi ya vijana wadogo, simu inaweza kuwa njia ya kuokoa maisha, sehemu ya kupata njia mpya ya kufikia na mitandao ya kijamii kama mtu mwenye ulemavu, au mahali pa kutafuta majibu ya maswali muhimu kuhusu afya yako.

Hata hivyo, kwa sehemu kubwa, watoto wanapotumia simu zao kuwasiliana, wanazungumza na marafiki na familia. "Ikiwa unachunguza ni nani watoto wanazungumza nao mtandaoni kuna mwingiliano mkubwa sana na mtandao wao wa nje ya mtandao," anasema Odgers.

Kwa hakika, ingawa simu janja mara nyingi hulaumiwa kwa watoto kutumia muda mchache kucheza nje, uchunguzi wa Denmark wa watoto wenye umri wa kati ya miaka 11 hadi 15 ulipata ushahidi fulani kwamba simu huwapa watoto uwezo wa kujitegemea kwa kuongeza hali ya usalama ya wazazi na kusaidia kuzunguka katika mazingira wasiyoyafahamu.

Watoto walisema simu ziliboresha uzoefu wao nje kupitia kusikiliza muziki, na kuwasiliana na wazazi na marafiki.

Bila shaka, uwezo wa kuwa katika mawasiliano ya karibu mara kwa mara na wenzao hauwezi kuja bila hatari.

Wakichanganua data kutoka kwa zaidi ya washiriki 17,000 wenye umri wa kati ya miaka 10 na 21, watafiti waligundua kuwa matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii katika umri wa miaka 11 hadi 13 kwa wasichana, na 14 hadi 15 kwa wavulana, yalionesha matumizi ya chini ya mitandao ya kijamii katika umri huu. Wazazi wanapaswa kuzingatia viwango hivi vya umri wakati wa kufanya maamuzi kwa ajili ya familia zao lakini inafaa kufahamu kuwa mabadiliko ya ukuaji yanaweza kuwafanya watoto kuwa makini zaidi na upande hasi wa mitandao ya kijamii.

Katika miaka ya ujana, kwa mfano, ubongo hubadilika sana, na hii inaweza kuathiri jinsi vijana wanavyotenda na kuhisi ikiwa ni pamoja na kuwafanya wawe makini zaidi kwa mahusiano ya kijamii na hadhi.

yyy

Chanzo cha picha, Richard Baker/Getty Image

Maelezo ya picha, Wazazi wengi huchagua kuwatambulisha watoto wao kwenye mitandao ya kijamii tangu wakiwa wadogo (Mikopo: Richard Baker/Getty Images)

"Kuwa kijana ni wakati muhimu sana wa maendeleo," Orben asema. "Unaathiriwa zaidi na vijana wenzako, unavutiwa zaidi na kile watu wengine wanachofikiri kukuhusu. Na muundo wa mitandao ya kijamii jinsi inavyotoa mawasiliano ya kijamii na maoni kuhusu, zaidi au kidogo, kubofya kitufe - kinaweza kuleta msongo wa mawazo zaidi wakati fulani."

Pamoja na umri, mambo mengine yanaweza kuathiri athari za mitandao ya kijamii kwa watoto na vijana - lakini watafiti ndio wanaanza kuchunguza tofauti hizi za watu binafsi.

"Hili ni eneo la msingi la utafiti sasa," Orben anasema. "Kutakuwa na watu ambao wana athari mbaya zaidi au chanya katika nyakati tofauti. Hiyo inaweza kuwa ni kwa sababu ya kuishi maisha tofauti, kupitia maendeleo katika maeneo tofauti, wanaweza kutumia mitandao ya kijamii tofauti. Kwa kweli tunahitaji kutania mambo hayo.” Ingawa utafiti unaweza kutoa mawazo kwa familia zinazoamua kumnunulia mtoto wao simu janja, hauwezi kutoa majibu mahususi kwa swali la "lini?".

Swali muhimu ambalo wazazi wanapaswa kuuliza, anasema Odgers, ni: "Je, inafaa kwa mtoto na kwa familia?" Kwa wazazi wengi, kumnunulia mtoto simu ni uamuzi wa vitendo. “Katika hali nyingi, wazazi ndio wanaotaka watoto wadogo wawe na simu ili waweze kuwasiliana siku nzima, waweze kuratibu muda wa kuwapitia kuwachukua,” anasema Odgers. "Nadhani kwa watoto inawapa hisia ya uhuru na uwajibikaji," anasema Anja Stevic, mtafiti katika idara ya mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Vienna, Austria.

"Kwa hakika hili ni jambo ambalo wazazi wanapaswa kuzingatia: je, watoto wao wako katika hatua ambayo wanawajibika vya kutosha kuwa na kifaa chake?"

Jambo moja ambalo wazazi hawapaswi kupuuza ni jinsi wanavyojisikia vizuri mtoto wao akiwa na simu janja. Katika utafiti mmoja wa Stevic na wenzake, wazazi walipohisi kukosa udhibiti wa matumizi ya simu janja za watoto wao, wazazi na watoto waliripoti mizozo zaidi juu ya kifaa hicho.

Inafaa kukumbuka, hata hivyo, kwamba kuwa na simu janja hakuhitaji kufungua milango kwa kila programu au mchezo unaopatikana. "Ninazidi kusikia, ninapohoji watoto, wazazi wanawapa simu lakini wanatoa mahitaji ya kuangalia na kujadili ni programu gani wanapata na nadhani hiyo ni busara kweli," anasema Livingstone. Wazazi wanaweza pia, kwa mfano, kutumia muda kucheza michezo na watoto ili kuhakikisha kuwa wamefurahishwa na maudhui, au kutenga muda wa kupitia kile kilicho kwenye simu pamoja. "Kuna kiasi cha usimamizi, lakini lazima kuwe na mawasiliano haya na uwazi kwake, ili kuweza kuwaunga mkono kwa kile wanachokiona na kupitia mtandaoni, kama ilivyo kwa nje ya mtandao," anasema Odgers.

yyy

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati wa kuweka sheria za nyumbani za matumizi ya simu janja- kama vile kutoweka simu katika chumba cha kulala cha mtoto usiku kucha wazazi pia wanahitaji kuangalia kwa uwazi matumizi yao ya simu janja.

"Watoto wanachukia unafiki," anasema Livingstone. "Wanachukia kuhisi kwamba wanazuiwa kwa jambo ambalo wazazi wao hufanya, kama vile kutumia simu wakati wa chakula au kulala na simu."

Hata watoto wadogo sana hujifunza kutokana na matumizi ya simu ya mzazi wao.

Ripoti ya Ulaya kuhusu matumizi ya teknolojia ya kidijitali miongoni mwa watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka nane iligundua kuwa kundi hili la umri lilikuwa na ufahamu mdogo au halina kabisa juu ya hatari hizo, lakini kwamba watoto mara nyingi waliakisi matumizi ya teknolojia kwa wazazi wao.

Baadhi ya wazazi hata waligundua wakati wa utafiti kwamba watoto walijua manenosiri ya kifaa chao na hivyo wanaweza kuingia bila usimamizi Lakini wazazi wanaweza kutumia hii kwa manufaa yao kwa kuwashirikisha watoto wadogo wakati wa kazi zinazotegemea simu janja na kuiga matumizi mazuri.

"Nadhani ushiriki huu na matumizi ya pamoja, hiyo ni njia nzuri kwao kujifunza nini kinatokea kwenye kifaa hiki, na ni cha nini," anasema Stevic.

Hatimaye, wakati wa kumnunulia mtoto simu janja huja kwa uamuzi wa thamani kwa wazazi. Kwa wengine, uamuzi sahihi hautakuwa kununua moja na, kwa ubunifu kidogo, watoto wasio na simu janja hawatakiwi kukosa.

"Watoto ambao wanajiamini ipasavyo na wanaopenda urafiki watapata suluhisho na kuwa sehemu ya kikundi," anasema Livingstone. "Baada ya yote, maisha yao ya kijamii ni shuleni, kwakuwa wanaonana kila siku."

Kwa kweli, kujifunza kukabiliana na woga wa kukosa wanahisi kwa kukosa simu kunaweza kuwa somo muhimu kwa vijana wakubwa ambao bila kulazimishwa tena na wazazi wao bila shaka watajinunulia na watahitaji kujifunza jinsi ya kuweka mipaka.

"Shida ya kuogopa kukosa ni kwamba haina mwisho, kwa hivyo kila mtu anapaswa kujifunza kuchora mstari mahali fulani," anasema Livingstone. "Vinginevyo, utakuwa unasogeza 24/7."