Jinsi Urusi inavyonyakua nyumba za raia wa Ukraine huko Mariupol

Mamlaka ya Urusi imeteka maelfu ya makazi kutoka kwa wakaazi wa Ukraine waliotorioka mjini Mariupol, uchunguzi wa BBC Verify umegundua kuwa jiji hilo linaadhimisha miaka mitatu ya kukaliwa.
Angalau makaazi 5,700 yametambuliwa kutekwa, uchambuzi wetu wa hati zilizochapishwa na mamlaka ya jiji iliyosakinishwa na Urusi tangu Julai 2024 unaonyesha.
Ili kuokoa nyumba zao, raia wa Ukraine wangelazimika kukabili hatari ya kurudi Mariupol kupitia Urusi, kufanyiwa ukaguzi wa usalama unaochosha, mchakato mgumu wa urasimu na shinikizo kubwa la kukubali pasipoti ya Urusi.
Nyingi za mali zilizoathiriwa ziliwahi kukaliwa na Waukraine ambao walitoroka au kufa wakati Urusi ilipozingira mji huo muhimu kwa siku 86 mwaka wa 2022.
Human Rights Watch ilisema vita hivyo viliwaua zaidi ya watu 8,000, lakini ikaongezea kuwa idadi hiyo huenda iko chini mno.
Unyakuzi huo unaonekana kuwa sehemu ya mpango mkubwa wa "Russify" mji wa pwani unaokaliwa, unaojumuisha ujenzi wa vituo vipya vya kijeshi na kubadilisha mitaa kuwa majina yaliyoidhinishwa na Moscow.
Mzingiro wa Urusi uliacha 93% ya majengo ya juu ya Mariupol - minara 443 - kuharibiwa, utafiti wa Human Rights Watch uligundua. Tangu wakati huo, Urusi inadai kuwa imejenga zaidi ya nyumba 70 mpya, lakini wenyeji wanasema uhaba mkubwa wa nyumba unaendelea.

Chanzo cha picha, Anadolu Agency via Getty Images
Kumekuwa na ripoti kwa muda kwamba Urusi imekuwa ikiteka mali katika Ukraine inayokaliwa. Lakini sheria mpya imeharakisha mchakato huo - na kuifanya kuwa vigumu kwa wamiliki wa Ukraine kudai haki zao.
Mbali na nyumba 2,200 zinazotarajiwa kunyakuliwa na maafisa wa jiji, zingine 3,550 zimetambuliwa kwa uwezekano wa kuchukuliwa, hati za jiji zilizochambuliwa na kipindi cha BBC Verify zimeonesha.
Maafisa wa Mariupol walishindwa kujibu walipotakiwa kutoa maoni yao.
Halyna ni miongoni mwa raia 350,000 wa Ukraine wanaokadiriwa kutoroka Mariupol kufuatia uvamizi wa Urusi.
Tumekubali kutotambua jina lake la ukoo kwa sababu ya usalama wa familia yake ambayo imesalia jijini.
Alisema jengo lake la ghorofa katika jiji la bahari - ambalo lilikuwa na wakazi 425,000 kabla ya vita - liliharibiwa na mashambulizi ya vifaru vya Urusi wakati wa kuzingirwa.
Ameambiwa "madirisha na milango" ya ghorofa hiyo imekarabatiwa, na kwamba watu wanaishi humo bila ruhusa yake. Anaogopa jumba lake l itachukuliwa.
"Huu ni wizi uliohalalishwa wa mali," alisema.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Maafisa wa Urusi hutumia neno "isiyo na umiliki" kuelezea nyumba wanazosema hazitumiki au hazina wamiliki halali - mali ambayo haijasajiliwa nchini Urusi.
Lakini nyumba hizi zina wamiliki halali - wakaazi wa Ukraine waliokimbia uvamizi wa Urusi, au warithi wa wale waliokufa katika mashambulio ya Urusi.
Hati rasmi zilizochapishwa kwenye tovuti ya utawala unaounga mkono Urusi zinaonyesha mchakato mgumu - ulioainishwa hapa chini - unaosababisha mali kutwaliwa baada ya kuripotiwa na wakaguzi wa ndani au wakaazi.
Hatukuweza kupata ni rekodi ngapi za Ghorofa zilizopita hatua ya mwisho ya mahakamani.
Lakini katika mkutano wa hivi majuzi Oleg Morgun - meya wa Mariupol aliyewekwa na Urusi - alisema uamuzi wa mwisho wa mahakama ulilenga kuzikamata nyumba 600 .
Kiutendaji ikiwa nyumba yako itaingia katika orodha yoyote kati ya hizo mali yako "haiwezi" kupatikana, Petro Andrushenko, mshauri wa zamani wa meya wa Mariupol, alisema. Mapema mwezi huu, Morgun alisisitiza kwamba nyumba zitaondolewa kwenye rejista "ikiwa mmiliki atakata rufaa".
Mara tu nyumba hizo zimechukuliwa, sheria iliyopitishwa mwishoni mwa mwaka jana inaruhusu mamlaka kuhamisha umiliki kwa watu binafsi.
Wakazi wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk ambao walipoteza mali na kushikilia pasipoti za Kirusi ndio wanaostahili kupata nyumba chini ya mpango huo.

Chanzo cha picha, Reuters
Mamlaka zinaonekana kutaka kufanya iwe vigumu kwa Waukraine kudai haki zao. Nyumba zote katika maeneo kama Mariupol lazima zisajiliwe nchini Urusi - lakini amri iliyotiwa saini na Rais Vladimir Putin mnamo Machi ilipiga marufuku raia wa nchi "zisizo na urafiki" - pamoja na Ukraine - kusajili mali katika maeneo yanayokaliwa hadi 2028 bila idhini maalum.
Kwa kweli, inawaacha Waukraine na chaguo lisilowezekana: usalama wao na utambulisho wao, au nyumba zao.
Pavlo alisema alilazimika kusalia Mariupol katika kipindi chote cha kuzingirwa baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Urusi.
Alifanikiwa kuzuia nyumba yake kukamatwa kwa kupata pasipoti ya Kirusi na anasema kwamba "asilimia 95 ya mazungumzo yote katika jiji ni kuhusu mali".
BBC imekubali kuficha jina lake halisi ili kulinda utambulisho wake.
Katika mazungumzo ya Telegram yaliyokaguliwa na BBC Verify - baadhi yakiwa na maelfu ya watumiaji - wenyeji wengi walionekana kuchanganyikiwa na mchakato huo na wakati fulani hawakuelewa jinsi mali yao iliishia kutangazwa kuwa "bila umiliki".
"Sheria haziko wazi na hazijachapishwa popote," Halyna alisema. "Unaweza kushtakiwa kwa chochote katika simu yako au katika rekodi zako walizo nazo juu yako."
Diana Berg pia alitoroka jiji hilo ili kukwepa kukaliwa na Warusi, akiacha nyumba ya familia yake. Na sasa yuko eneo jingine huko Ukraine.
Ili kuzuia mali kumilikiwa na jiji, jamaa ya Diana angelazimika kurudi Mariupol. Njia pekee ya kufanya hivyo ni kwenda hadi uwanja wa ndege wa Sheremetyevo wa Moscow, ambapo wangekabiliwa na ukaguzi wa usalama wa Shirikisho la Usalama (FSB) - unaojulikana kama "filtration".
Diana alisema "hakuna njia" familia yake inaweza kusafiri kwenda Mariupol. "Utaratibu wa 'kuchuja'... unaweza kudumu hadi wiki. Hujafungwa, lakini unawekwa katika kituo hiki huku wakikuchunguza."
Mipango ya ujenzi wa nyumba inaonekana kuwa sehemu ya kampeni kubwa inayolenga "Russifying" mji wa kusini mwa Ukraine.
Picha za satelaiti na ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha kuwa chuo kipya cha wanamaji na ukumbusho mkubwa wa vita vinajengwa.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












