'Mariupol ni makaburi': Waliookolewa wasimulia shambulio la kutisha la Warusi

Mariupol imekuwa ikikabiliwa na mashambulio makali ya Warusi kwa wiki tano, lakini wakazi wamefanikiwa kukimbilia katika miji mingine nchini Ukraine. Wanaiambia BBC juu ya hali katika mji huo uliokumbwa na mapigano-na wapendwa wao waliowaacha nyuma.
Watu wanaowasili katika mji wa Zaporizhzhia, ambao ni kama kitovu cha wakimbizi, wanaelezea mashambulio ya bila huruma dhidi ya Mariupol ambako mashambulio ya ndege na makombora yameporomosha majengo yote ya wilaya za mji huo.
Wamechukua safari za hatari kupitia kwenye maeneo ya mapambano ya Urusi na na Ukraine ambayo Kamati ya msalaba mwekundu (ICRC) yameyaelezea kama ''uokoaji wa kutoka kuzimu".
Akizubiri ndani ya moja ya majengo alikuwa Yuliia, mabinti zake wawili na mama yake Tatiana. Walitoroka tarehe 4 Aprili.
"Ni watu wenye njaa kali… watu wana matatizo ya kiakili. Watu wanazikwa kwenye mitaa ," Yuliia alisema, akizungumza na BBC kwa sharti kwamba jina lake halitumiki, ombi ambalo wakazi wamekuwa wakiliomba, mara kwa mara ambao bado wanahofia juu ya usalama wao.
Mama yake, Tatiana, aliongeza: "[ Kuna] makaburi mafupi, yenye kimo cha nusu mita, baadhi yenye udongo mchache juu yake. Miili ya wafu , kweney mitaa yote."

Chanzo cha picha, Reuters
Fursa ya kufika nje ilififia haraka kwa wakazi wengi.
"Wakati tulipokuwa katika Mariupol, Wachechnya walikuwa wanapora. Walikuwa wanachukua dhahabu za watu. Hali ilikuwa inakuwa hatari kusema kweli, tulisikia walikuwa wanawabaka wanawake ," alisema Yuliia.
"Ilikuwa inaogofya kwa Watoto wangu na nikagundua lazima tuwaondoe nje yam ji cha njia yoyote ile ".
BBC binafsi haiwezi kuthibitisha madai haya. Wanamgambo wa Chechnya wanaoinga mkono Urusi wamekuwa wakipigana nchini Ukraine tangu mwanzo wa uvamizi na wanaripotiwa kuhusiska kwa kiasi kikubwa katika mashambulizi ndani ya mji wa Mariupol.
Kwingineko katika Zaporizhzhia, wafanyakazi wa misaada wamekuwa wakitafuta nyumba na kutoa pesa kwa familia zilizookolewa.
Katika kituo kimoja cha wakimbizi, Liubov, mwenye umri wa miaka 61, alikuwa akimsubiri mwanawe wa kiume
Amekwamba katika Zaporizhzhia,na hajasikia taarifa zozote juu ya mke Svetlana tangu alipowasiliana naye mara ya mwisho mapema mweszi Machi.
"Ujumbe wake wa mwisho kutoka kwake ulikuwa …tunapigwa mabomu ," alisema.
Alipitia jumbe za simu za mawasiliano na mke wake, akimuuliza yuko wapi, alimtumia picha ya jingo la makazi wayokuwa wakiishi , ambalo lilikuwa limepigwa kwa makombora ya anga.

Chanzo cha picha, Reuters
"Warusi walikuwa wakiwachukua nje ya makazi hayo, na kuchukua pichaa za watu hao na kusema , 'tulikuja hapa kuwakomboa nyinyi '. Watu walikuwa wakili, wakiogopa kujibu lolote. Wakiogopa kuwa wanaweza kunyingwa au kupigwa risasi.
"Warusi walikuwa wanasema: 'Tazama, haya ni machozi ya furaha. Watu wanafuraha kuwa huru dhidi ya mafashisti '."
Katika kituo cha wakimbizi, Liubov aliangua kilio alipokuwa akionyesha picha kwenye simu yake huku akirejelea tena na tena kusimulia masaibu waliyoyapitia katika Mariupol: haja ya mazishi ya watu wengi waliokufa.
Waliipiga makombora na kuangamiza soko la kati kati mwa Mariupol, kwahiyo watu walichimba shimo ardhini ambako watakuwa wanaleta miili ya wafu ," alisema. "Tuliambiwa watakuwa wakizikwa pale. Lakini hajui bado kama hilo lilifanyika."
Wanaume wote katika kituo cha wakimbizi waliripoti taarifa zinazofanana na anazosema na Liubov

Chanzo cha picha, Reuters
Jumatano, mabasi manane yaliyowabeba watu waliookolewa yalisindikizwa na ICRC hadi katika mji wa Zaporizhzhia.
Waliwasili na vitu ambavyo wangeweza kuvibeba. Walionekana wachovu na wenye mshituko kutokana na mashambulio ya makombora.
Baadhi walisema kukatika kwa mawasiliano katika Mariupol lilikuwa ni jambo baya sana kiasi kwamba walikaa wiki kadhaa bila kujua iwapo maeneo mengine ya nchi yamechukuliwa na Warusi.
Moja ya watu walioondoka katika mabasi ya kwanza alikuwa ni Anna. Alikuwa ameweza kufika katika mji wa Berdyansk yapata maili 50 (80km), Eneo ambako mabasi ya ICRC yangeweza kufika katika Mariupol.
"Mariupol kwa sasa ni makaburini. Maeneo yote yamefunikwa na makaburi ya raia," alisema.
"kwa bahati mbaya, sio kila mtu aliondoka. Tuna ndugu katika Mariupol ambao hatujaweza kuwasiliana nao tangu mwishoni mwa mwezi wa februari . hatujui kama wanaishi au hapana," aliongeza.

Moscow inadai imewaokoa raia waliokuwa wameshikiliwa na "wapiganaji wa batalioni ya Nazi " katika Mariupol. Ukraine inasema watu wapatao 40,000 wamelazimishwa kupelekwa Urusi, huku baadhi wakiwa wameshikiliwa katika "kambi za uchujaji" ambako wanapelelezwa.
Watu wengi wamepoteza mawasiliano na ndiugu zao wa karibu na hawana njia ya kujua iwapo wangali hai au la.
Yevhenii Lysenko pia anasubiri katika kituo cha wakimbizi mjini Zaporizhzhia. Aliondoka Mariupol kwa ajili ya safari ya kikazi kabla vita havijaanza. Uvamizi ulifanyika siku moja kabla ya kurejea nyumbani.
Amekwama katika Zaporizhzhia, na bado hajasikia taarifa zozote kumuhusu mke wake Svetlana tangu walipowasiliana kwa mara ya mwisho mapema mwezi Machi.
"Ujumbe kutoka kwake ulikuwa kwamba walikuwa wanapigwa mabomu, alisema.
"Mara ya mwisho nilipozungumza naye ilikuwa tarehe 2 Machi. Kwahiyo kwa mwezi mzima sijaongea naye. Sifahamu ni nini kilichomtokea. Sijui kama bado yuko hai."
Alikuwa amefikiria uwezekano wa kusafiri kwenda Mariupol,kurudi akipitia maeneo ya mapambano yanayoshikiliwa na Warusi.
"Lakini kama nikijipata katika wapiganaji wanaotaka kujitenga watanikabidhi silaha na kuniambia niende niwapige risasi watu wangu … au waninyonge kama nikikataa kufanya hivyo," alisema.
Nilimuuliza ni nini anajua kuhusu nyumba yake.
Alijibu: "Haipo tena. Iliangamizwa na makombora au mashambulio ya ndege. Kwa ufupi hakuna mahala pa kwenda mimi ."
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine












