UFO: Mambo matano yaliyofichliwa katika kikao cha jopo la NASA

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Mamlaka ya Marekani imechunguza takriban ripoti 800 za kushangaza za vitu visivyojulikana vilivyokusanywa kwa miongo kadhaa - lakini ni sehemu ndogo tu ambayo haijaelezewa, jopo la watafiti linasema.

Nasa ilianzisha jopo mwaka jana kuelezea kazi yake juu ya kile inachokiita unidentified anomalous phenomena (UAP).

UAP inafafanuliwa kama maono "ambayo hayawezi kutambuliwa kama ndege au matukio ya asili yanayojulikana kutoka kwa mtazamo wa kisayansi".

Jopo hilo lilifanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara siku ya Jumatano.

Maoni mengi yanaweza kuelezewa - mengine yanabaki kuwa siri

"Tuna ripoti mpya 50 hadi 100 kila mwezi," Sean Kirkpatrick, mkurugenzi wa Ofisi ya Azimio la Anomaly ya kikoa (AARO), Wizara ya Ulinzi ya Marekani.

Lakini alisema idadi ya walioonekana ambayo "inawezekana kweli isiyo ya kawaida" ni 2% hadi 5% ya hifadhidata yote.

Wakati mmoja wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, video iliyochukuliwa na ndege ya jeshi la majini magharibi mwa Marekani ilionyesha mfululizo wa nukta zikisonga angani usiku. Ndege hiyo ya kijeshi haikuweza kukinasa kitu hicho, ambacho kiligeuka kuwa ndege ya kibiashara iliyokuwa ikielekea kwenye uwanja mkubwa wa ndege.

Kikao cha UFO ni nini?

Ulikuwa mkutano wa kwanza wa hadhara juu ya mada hiyo katika miongo kadhaa ya utafiti wa NASA vitu vya vinavyopaa angani ambavyo havitambuliwi (UFO)

Richard Gray, mhariri wa kitengo cha BBC cha Future , anaripoti kwamba matukio ya (UFOs) yamekuwa yakinyanyapaliwa kwa muda mrefu - watu wengi hawafikirii kuwa yanapaswa kufanyiwa utafiti wa kisayansi wenye mantiki, lakini kuandaa mkutano huo ni wazi kwamba ni ishara kwamba NASA sasa inataka kuchukua somo kwa uzito, na kwamba jumuiya ya wanasayansi inazidi kuwa tayari kuzungumza kwa uwazi na ukweli juu ya uwezekano wa maisha ya nje ya dunia.

  • Hii ni mara ya kwanza kwa NASA kufanya mkutano wa hadhara kuhusu utafiti wa UFO, na ripoti ya kina itatolewa mwezi Julai
  • Kikosi kazi kilichoundwa mwaka jana kinachunguza data ya UAP - inayofafanuliwa kama "matukio yanayozingatiwa angani ambayo hayawezi kutambuliwa kama ndege au matukio ya asili yanayojulikana kisayansi."
  • Utafiti wa NASA unatofautiana na uchunguzi wa Idara ya Ulinzi ya Marekani kuhusu matukio ya angani ambayo hayajatambuliwa, ambayo ni operesheni ya utafiti inayoongozwa na wafanyakazi wa kijasusi wa Marekani.

Maoni mengine ni ya kushangaza zaidi.

Ripoti ya Pentagon mwaka 2021 ilisema kwamba kati ya vitu 144 vilivyoonwa na marubani ,vyote viliweza kuelezewa isipokuwa kimoja na hawakuondoa uwezekano kwamba vitu hivyo ni vya nje ya nchi.

Viongozi hawataki kuondoa uwezekano kwamba kitu hicho kilitoka kwa viumbe vya nje.

Haki za faragha zinazuia uchunguzi wa NASA

Kirkpatrick pia alitaja kuwa faragha inahusu uchunguzi wa NASA.

"Tunaweza kuelekeza zana zetu kubwa zaidi za ukusanyaji kwenye sayari nzima wakati wowote tunaotaka," alisema.

"Mengi tuliyo nayo ni karibu na bara la Amerika," alisema. "Watu wengi ... hawapendi tuelekeze zana zetu za kunasa taarifa karibu na nyumba zao."

g
Maelezo ya picha, Scott Kelly ni mwanaanga wa zamani na rubani mwenye uzoefu wa miongo kadhaa. Alisimulia hadithi kuhusu udanganyifu wa macho.

Microwave na udanganyifu wa macho

Data zinayohusiana na UAP mara nyingi ni ngumu kufafanua na kufasiriwa kwa urahisi.

David Spergel, mwenyekiti wa timu ya UAP ya Nasa, alitaja mlipuko wa mawimbi ya redio yaliyochukuliwa na watafiti nchini Australia.

"Walikuwa na muundo wa ajabu sana. Watu hawakuweza kujua kilichokuwa kikiendelea. Kisha wanaanza kugundua wengi wao wakiwa wamekusanyika karibu na chakula cha mchana," alisema.

Ilibadilika kuwa vyombo muhimu vilivyotumiwa na watafiti vilikuwa vikichukua ishara kutoka kwa microwave inayotumiwa kupasha chakula chao cha mchana.

Unyanyapaa na unyanyasaji huzuia utafiti

Marubani wa vyombo vya kibiashara wanasitasita sana kuripoti kuona vitu visivyoweza kutambuliwa angani, Bw Spergel alisema, kwa sababu ya unyanyapaa unaozunguka vyombo vya angani.

"Moja ya malengo yetu ni kuondoa unyanyapaa," alisema, "kwa sababu kuna haja ya data za hali ya juu za kushughulikia maswali muhimu kuhusu UAPs."

Na baadhi ya wanasayansi wamekumbana na unyanyasaji mtandaoni kwa kazi yao katika eneo hilo.

"Unyanyasaji husababisha tu unyanyapaa zaidi wa uwanja wa UAP, na kuzuiwa kwa kiasi kikubwa mchakato wa kisayansi na kuwakatisha tamaa wengine kusoma suala hili muhimu," alisema mkuu wa sayansi ya Nasa Nicola Fox.

g
Maelezo ya picha, Wamarekani wakielezea hisia zao kuhusu imani yao kwa Nas

Enzi mpya ya uwazi

Mojawapo ya sababu muhimu za kikao cha Jumatano ni mabadiliko ya mtazamo wa Nasa.

Mwisho wa kikao jopo lilichukua maswali kutoka kwa umma. Moja ya maswali hayo lilikuwa "Nasa inaficha nini?"

Dan Evans wa Nasa alijibu kuwa shirika hilo limejitolea kuweka uwazi. "Ndio maana tuko hapa moja kwa moja kwenye TV leo," alisema.