Sayari ambayo mwaka mmoja ni sawa na miaka 84 ya Dunia

Chanzo cha picha, Getty Images
Pete za mwanga kuzunguka sayari hii katika mfumo wa jua hazijawahi kuonekana kwa uwazi hapo awali. Inapotazamwa kwa mbali, sayari inaonekana imefungwa katika halo ya mviringo ya mwanga.
Shirika la anga za juu la Marekani NASA limeshiriki picha mpya za Uranus. Picha hizi zilichukuliwa kutoka kwa darubini ya anga ya James Webb.
Uranus ni sayari ya saba ya mfumo wetu wa jua.
Wakati chombo cha anga za juu cha Voyager 2 kilipopita Uranus mnamo 1986, kamera yake ilinasa picha ya mpira wa buluu-kijani ya Uranus. Hakuna pete za mwanga zilizoonekana ndani yake.
Lakini kwa mujibu wa NASA, picha za hivi karibuni za James Webb za Uranus kwa kutumia urefu wa mawimbi ya infrared zinaonesha pete angavu kuzunguka sayari.
Uranus ina kipengele maalumu kinachoiweka tofauti na sayari nyingine katika mfumo wa jua. Ni sayari pekee inayozunguka kwenye mhimili wake kwa kuinamisha takriban digrii 90.
Kwa sababu ya hii, misimu kwenye sayari inabaki katika hali mbaya zaidi. Hapa katika maeneo ya juu na chini ya dunia kuna mwanga wa jua kwa miaka na kisha giza kwa idadi sawa ya miaka.
Mwaka mmoja ni sawa na miaka 84 ya Dunia

Chanzo cha picha, WEBBTELESCOPE.ORG
Siku kwenye Uranus ni saa 17, dakika 14. Hiyo ni, kwa wakati huu inakamilisha mzunguko wa mhimili.
Lakini, mwaka wake mmoja ni sawa na miaka 84 ya Dunia yaani siku 30,687. Hiyo ina maana kwamba inachukua miaka 84 kwa sayari hii kuzunguka jua.
Uranus inaaminika kuwa na pete 13, na picha kutoka kwa James Webb zinaoyesha 11 kati ya hizo. Baadhi ya pete hizo zinang'aa sana kiasi kwamba zinaonekana kuunda pete kubwa zaidi.
Wanasayansi wanatumai kuwa pete mbili zaidi zinaweza kuonekana kwenye picha za siku zijazo. Pete hizi zilipatikana mnamo 2007.
Picha hii pia inatoa taarifa kuhusu baadhi ya miezi 27 inayojulikana ya Uranus. Hata hivyo, baadhi ya miezi hii ni midogo sana kiasi kwamba haiwezi kuonekana.
Gamba la theluji juu ya uso

Chanzo cha picha, WEBBTELESCOPE.ORG
Mara nyingi kuna theluji nyepesi inayoyeyuka. Neptune (Sayari ya Varuna) na Uranus pia huitwa sayari zilizofunikwa na barafu. Kwa sababu hutengenezwa kwa maji yaliyoganda, methane na amonia. Hatahivyo, sayari hizi mbili pia ni sayari za gesi kama Jupiter na Zohali.
Rangi ya samawati ya Uranus inayoonekana kwenye picha inategemea data iliyokusanywa kupitia vichungi viwili.
Maeneo angavu inayoonekana kwenye picha hii inaelekea Jua. Sehemu hii ni upande wa kulia wa sayari.
Kofia hii inaonekana wakati eneo la polar linakabiliwa na jua na kutoweka wakati jua linapozama. Jinsi hii hutokea bado haijulikani.
Nguzo ya kusini ya sayari ni giza kwenye picha na kwa hivyo haionekani.
Kwa muda gani ilionekana kwenye kamera?
Kuna wingu angavu kwenye mhimili wa kofia ya polar na wingu jingine angavu upande wa kushoto wa sayari. Wingu hili labda linahusishwa na wingi wa theluji.
Kwa mujibu wa NASA, picha hii ilinaswa wakati Uranus ilikuwa ikitazamana na kamera na vichungi viwili kwa dakika 12. Lakini kulingana na NASA, habari iliyopokelewa kutoka kwa darubini ya James Webb bado ni ndogo sana kuelewa sayari hii.
Darubini ya James Webb yenye thamani ya dola bilioni kumi ilizinduliwa mnamo Desemba 2021. Ni ya juu zaidi kuliko darubini maarufu ya Hubble.
Ina malengo mawili. Kwanza, kuchukua picha za nyota za kwanza katika ulimwengu, miaka bilioni 13.5 iliyopita, na pili, kutafuta sayari ambapo kuna tumaini la uhai.















