Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii (30.08.2022)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kuhusu kusajili kiungo anasema:
"Ni kweli, lakini muda unavyokwenda, ndio inavyozidi kuwa ngumu (kukamilisha usajili). Hatujakata tamaa. muda upo, tusipata bado ninakifurahia kikosi tulichonacho"
Frenkie de Jong wa Barecelona na Moises Caicedo wa Brighton wamekuwa wakihusishwa kutua Anfield (Klopp Presser).

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal watalazimika kuingia sokoni kusaka kiungo wa kukaba baada ya Mohamed Elneny kuumia kwenye mchezo dhidi ya Fulham utakaomuweka nje kwa muda mrefu. Elneny alikuwa mbadala wa kiungo namba moja Thomas Partey ambaye naye ni majeruhi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Fulham wanakaribia kukamilisha usajili wa winga wa zamani wa Chelsea na Arsenal Willian, kwa mkataba wa mwaka mmoja. Mbrazil huyo yuko London sasa anafanyiwa vipimo (The Athletic).
Mazungumzo yaliyo katika hatua za mwisho yanaendelea kati ya Chelsea na Barcelona kuhusu uhamisho wa Pierre Aubameyang (Romano).
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu za Ajax na Manchester United zimetoa taarifa rasmi kuhusu Antony: "Ajax na Manchester United zimekubaliana kuhusu uhamisho wa Antony Matheus dos Santos." Ada yake inafikia €100 million.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2